Rais samia akiwa Washington D.C amesema Tanzania kisiasa tupo Vizuri.
Hali ya Kisiasa Tupo Stable,Hali ya Kisiasa iko Nzuri, tunachukua Hatua za kufanya Vyama vyote vya Siasa vikae Pamoja Kujadili namna ya Kuendesha Siasa zetu Nchini.
"Nimeunda timu ndani ya vyama vya siasa, tumeweka Jeshi la Polisi, viongozi wa dini, taasisi za kijamii, watajadili mambo ambayo wamepanga, kuna chama cha siasa kimoja bado hakijakubali bado naendelea na mazungumzo nao na nawaelewa kwanini hawajakubali" - Rais @SuluhuSamia.
Rais amewaona Vijana wa Marekani walioandamana na Mabango na Fulana wakidai Katiba Mpya na Wabunge wa 19 Wafukuzwe. Amesema ameyaona Mabango na kuyasoma. Ujumbe umefika.
Kuhusu chadema kugomea Vikao vya Baraza la vyama vya siasa, amesema anawaelewa na anaendelea kuzungumza nao ili wajiunge na wenzao.
Rais amewaona Vijana wa Marekani walioandamana na Mabango na Fulana wakidai Katiba Mpya na Wabunge wa 19 Wafukuzwe. Amesema ameyaona Mabango na kuyasoma. Ujumbe umefika
Bila katiba mpya Samia atakuwa ni mkandamizahi mwingine wa demokrasia. Madhaifu ya katiba ya mwaka 1977 yamejionyesha dhahiri kipindi cha utawala wa Magufuli
Sasa hivi anakazana kweli na hizi hadithi za kuwatia watu usingizi akitegemea kwamba ujinga wa waTanzania utaendelea kulinda maslahi yake na ya chama chake.
Kama wapinzani nao watazolewa na hadaa hizi anazowauzia, basi watakuwa hawana tofauti na hao CCM wenyewe.
Mkuu hiyo ni cha mtoto .tafuta clip ya kagame 2014 kama sikosei alienda Oxford university nahsi alipitishwa kwenye ma skip ya uchafu. Viongozi wa kiafrika wanaongoza nafsi zilizogoma japo wanajifanya watukufu.mama yetu ni "dhaifu" period
Hivi unajuaga watanzania wanavyoiga Tabia za kijinga wakienda ughaibuni? Kwanza kabisa lugha, na culture Yao Huwa wanaidharau. Kwa hivyo usingeshangaa kuona hata mayai viza yanatupwa pale Lisa kivuli Cha demokrasia. Sasa USA inarekodi mbaya kabisa ya mauaji yanayotokana na matumizi ya silaha. So huwezi kumtembeza Kwa mguu Rais halafu akajichanganye na watu kama hao. Yes ni haki Yao lakini Kwa Mama huyu Wala haihitaji nguvu zote hizo zaidi ni kujidhalilisha tu. Ikumbukwe jamii ya watanzania haipendi harakati hizi. Yaani huku mitaani hata vijana wa CDM wenyewe wanaponda kitendo hicho labda humu Kwa wafia dini wa JF