Rais Samia: Kuagiza sukari nje ya nchi ni upotevu wa pesa

Rais Samia: Kuagiza sukari nje ya nchi ni upotevu wa pesa

Kuteua mfanyabiashara siyo dhambi ikiwa ana sifa na uwezo wa kiuongozi.kikubwa ni mtu kuzingatia sheria ,kanuni na taratibu zinavyo hitaji ili kutoleta mgogoro wa kimaslahi katika maamuzi . Hata Trump ni mfanyabiashara Mkubwa lakini alichaguliwa na wa Marekani kuwa Rais na kuacha Biashara zake zikisimamiwa na kuendeshwa na Wengine
Hayo yanawezekana Kwa jamii iliyostarabika lakini sio huku kwetu Bongoland

Huku Kiongozi yupo radhi Wananchi wauziwe dizeli shilingi 3,500/Lt ili yeye apate gawio la shilingi 250/Lt itakayouzwa🙌
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameziagiza Wizara ya Kilimo na Wizara ya Biashara kuvipa kazi viwanda vya ndani ya Nchi ikiwemo Kilombero Sugar ili vizalishe sukari ya majumbani na viwandani na ethanol kwa ajili ya nishati ya kupikia huku akisema kuagiza tani 250000 ya sukari nje ya Nchi kwa ajili ya viwanda ni matumizi mabaya ya fedha.

Rais Samia ametoa agizo hilo leo August 04,2024 baada ya kuweka jiwe la msingi la upanuzi wa kiwanda cha sukari Kilombero-K4 Mkoani Morogoro.

“Niwaelekeze Mawaziri wawili wa Kilimo na wa Biashara, katika mahitaji yetu ya sukari Nchini, nimeambiwa tani 650000 ni matumizi ya sukari tunayotumia majumbani lakini viwanda vinahitaji tani 250000, sasa tani 250000 tukiendelea kuagiza ni upotevu wa fedha za kigeni”

“Mimi nina uhakika tukivipa kazi viwanda vyetu vinaweza kutuzalishia sukari ya viwandani, kwa hiyo sasa hiyo ndiyo kazi ninataka mkaitekeleze, angalieni mtawekaje sera zetu ili viwanda hivi viweze kuzalisha sukari ya viwandani lakini pia waweze kuzalisha ethanol kwa ajili ya kupata nishati safi ya kupikia na kwa matumizi mengine”.
---
Ndugu zangu Watanzania,

Hayo ni Maneno ambayo yanetamkwa na Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan,huko mkoani Morogoro hii leo katika muendelezo wa ziara yake na kuzungumza na wananchi.

Ambapo amesema ya kuwa mahitaji ya sukari nchini ni Tani laki 6 na Nusu ,huku mahitaji ya sukari viwandani ni Tani Laki 2 Na nusu. Na hivyo akizitaka wizara husika kuhakikisha kuwa sukari inazalishwa na viwanda vyetu vya hapa hapa Nchini,badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi,jambo ambalo ni upotevu wa pesa za kigeni.


Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili
Duuuh kazi sana aliyeagiza sijui anarubiri nini😂😂
 
Back
Top Bottom