Rais Samia: Kuagiza sukari nje ya nchi ni upotevu wa pesa

Rais Samia: Kuagiza sukari nje ya nchi ni upotevu wa pesa

Bashe alisema afadhali mashamba ya miwa yageuzwe kuwa ya mpunga ili tuendelee kuagiza sukari. Rais anasema kuagiza sukari nje ni upotevu wa pesa. Inafikirisha mtu yule yule aliyetaka mashamba ya miwa yafe, anapewa jukumu la kutayarisha sera ya kuaendeleza. TZ vituko kila kukicha.
Yaani utasema hawafanyi kazi ndani ya Serikali moja.

Ingekuwa kipindi kile cha Agano la Kale, utasema wanafanya kazi ya kujenga Mnala wa Babeli 🙌
 
Akili za viongozi wa TZ haieleweki kabisa.
Na apo sa100 analalamika badala ya kuonyesha amefanya solutions Gani kam kiongozi.

Ina maana sukari itaendelea kuwa tatizo tz , mpaka mageuzi yenye tija yafanyiwe kazi
Kama Mhe. Rais ataendelea kuwateua Mawaziri na Viongozi ambao ni Wafanyabiashara, tusitegemee Wananchi kupata unafuu wa maisha.

Tutegemee gharama za maisha kuendelea kupanda hadi Siku ya kuondoka Duniani
 
View attachment 3062110Ndugu zangu Watanzania,

Hayo ni Maneno ambayo yanetamkwa na Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan,huko mkoani Morogoro hii leo katika muendelezo wa ziara yake na kuzungumza na wananchi.

Ambapo amesema ya kuwa mahitaji ya sukari nchini ni Tani laki 6 na Nusu ,huku mahitaji ya sukari viwandani ni Tani Laki 2 Na nusu. Na hivyo akizitaka wizara husika kuhakikisha kuwa sukari inazalishwa na viwanda vyetu vya hapa hapa Nchini,badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi,jambo ambalo ni upotevu wa pesa za kigeni.View attachment 3062107

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili
Mwombeni msamaha bwana Mpina.
 
Kama Mhe. Rais ataendelea kuwateua Mawaziri na Viongozi ambao ni Wafanyabiashara, tusitegemee Wananchi kupata unafuu wa maisha.

Tutegemee gharama za maisha kuendelea kupanda hadi Siku ya kuondoka Duniani
Kuteua mfanyabiashara siyo dhambi ikiwa ana sifa na uwezo wa kiuongozi.kikubwa ni mtu kuzingatia sheria ,kanuni na taratibu zinavyo hitaji ili kutoleta mgogoro wa kimaslahi katika maamuzi . Hata Trump ni mfanyabiashara Mkubwa lakini alichaguliwa na wa Marekani kuwa Rais na kuacha Biashara zake zikisimamiwa na kuendeshwa na Wengine
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameziagiza Wizara ya Kilimo na Wizara ya Biashara kuvipa kazi viwanda vya ndani ya Nchi ikiwemo Kilombero Sugar ili vizalishe sukari ya majumbani na viwandani na ethanol kwa ajili ya nishati ya kupikia huku akisema kuagiza tani 250000 ya sukari nje ya Nchi kwa ajili ya viwanda ni matumizi mabaya ya fedha.

Rais Samia ametoa agizo hilo leo August 04,2024 baada ya kuweka jiwe la msingi la upanuzi wa kiwanda cha sukari Kilombero-K4 Mkoani Morogoro.

“Niwaelekeze Mawaziri wawili wa Kilimo na wa Biashara, katika mahitaji yetu ya sukari Nchini, nimeambiwa tani 650000 ni matumizi ya sukari tunayotumia majumbani lakini viwanda vinahitaji tani 250000, sasa tani 250000 tukiendelea kuagiza ni upotevu wa fedha za kigeni”

“Mimi nina uhakika tukivipa kazi viwanda vyetu vinaweza kutuzalishia sukari ya viwandani, kwa hiyo sasa hiyo ndiyo kazi ninataka mkaitekeleze, angalieni mtawekaje sera zetu ili viwanda hivi viweze kuzalisha sukari ya viwandani lakini pia waweze kuzalisha ethanol kwa ajili ya kupata nishati safi ya kupikia na kwa matumizi mengine”.
---
Ndugu zangu Watanzania,

Hayo ni Maneno ambayo yanetamkwa na Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan,huko mkoani Morogoro hii leo katika muendelezo wa ziara yake na kuzungumza na wananchi.

Ambapo amesema ya kuwa mahitaji ya sukari nchini ni Tani laki 6 na Nusu ,huku mahitaji ya sukari viwandani ni Tani Laki 2 Na nusu. Na hivyo akizitaka wizara husika kuhakikisha kuwa sukari inazalishwa na viwanda vyetu vya hapa hapa Nchini,badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi,jambo ambalo ni upotevu wa pesa za kigeni.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili
Akisema Mpina mnamuona sio mzalendo
 
Nimetanguliza vipi uchawa.
Uchawa huu hapa:
1.Hayo ni Maneno ambayo yametamkwa na Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan

2.Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Why all that,ni unafiki tu.
 
Nilichoandika ndio ukweli wenyewe tena ukweli halisia.
 
Mpina alisema tumeagiza kuliko gap sugar na kwamba walioagiza hawana vigezo.

Mama Samia kasema hata hiyo gap sugar hatupaswi kuagiza (Hata kama una vibali au kuagiza ndani ya gap sugar) maana tunapoteza pesa.

Mpina hakupinga sukari isiagizwe ila alipinga utaratibu na kiasi kiliachoagizwa. Mama samia anapinga uagizaji all together so ni mambo mawili tofauti.
You think your telling us the differences from those statements but you end up telling us the similarities 😂😂😂😂! Tell us again the differences! Is Samia Concur with her Minister on importing Sugar?
 
Tusipoondoa mambumbumbu serikalini, huko tuendako ni kugumu sana kuliko hata Bangladesh ya sasa. Rais apate washauri wazuri. Nakumbuka alivyomtukana Prof. Mkenda kwa issue hii na kumtoa uwaziri wa Kilimo.
Mbumbumbu kubwa kuliko vyote na ambacho ni chanzo cha yote ni CCM.
Hao mambumbumbu wa serikalini wametengenezewa umbumbumbu na chama "twawala" ambacho ni CCM,hivyo kufanya mfumo wote kuwa mbumbumbu.
 
Bashe alisema afadhali mashamba ya miwa yageuzwe kuwa ya mpunga ili tuendelee kuagiza sukari. Rais anasema kuagiza sukari nje ni upotevu wa pesa. Inafikirisha mtu yule yule aliyetaka mashamba ya miwa yafe, anapewa jukumu la kutayarisha sera ya kuaendeleza. TZ vituko kila kukicha.
This can only happen in Tanzania.
 
Back
Top Bottom