View attachment 3062110Ndugu zangu Watanzania,
Hayo ni Maneno ambayo yanetamkwa na Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan,huko mkoani Morogoro hii leo katika muendelezo wa ziara yake na kuzungumza na wananchi.
Ambapo amesema ya kuwa mahitaji ya sukari nchini ni Tani laki 6 na Nusu ,huku mahitaji ya sukari viwandani ni Tani Laki 2 Na nusu. Na hivyo akizitaka wizara husika kuhakikisha kuwa sukari inazalishwa na viwanda vyetu vya hapa hapa Nchini,badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi,jambo ambalo ni upotevu wa pesa za kigeni.
View attachment 3062107
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili