Rais Samia: Kuagiza sukari nje ya nchi ni upotevu wa pesa

Rais Samia: Kuagiza sukari nje ya nchi ni upotevu wa pesa

View attachment 3062110Ndugu zangu Watanzania,

Hayo ni Maneno ambayo yanetamkwa na Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan,huko mkoani Morogoro hii leo katika muendelezo wa ziara yake na kuzungumza na wananchi.

Ambapo amesema ya kuwa mahitaji ya sukari nchini ni Tani laki 6 na Nusu ,huku mahitaji ya sukari viwandani ni Tani Laki 2 Na nusu. Na hivyo akizitaka wizara husika kuhakikisha kuwa sukari inazalishwa na viwanda vyetu vya hapa hapa Nchini,badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi,jambo ambalo ni upotevu wa pesa za kigeni.View attachment 3062107

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili
Kwa sasa kashajua umuhimu wa fedha za kigeni?
 
Aiseee rudi kupitia tena youtube uone malumbano ya Mpina na bashe maana naona kama unapotosha.
Mpina anakubali gap sugar iagizwe nje ila kupitia viwanda vilivyopo na iwe ndani ya gap sugar husika.

Mama samia hapendi tuagize kabisa maana pesa zinapotea kwa makampuni ya nje.

Sasa hayo mawazo mbona hayafanani kabisa?
 
Hata sisi tunajua ni gharama ila yeye ni Rais anatakiwa alete solution in a short term, tusiagize kabisa sukari kutoka nje lakini pia na bei ishuke.

Alete solution sio kuaddress/identify tatizo ambalo wote tunalijua na chanzo chake ni Utawala mbovu wa CCM.
 
Hata sisi tunajua ni gharama ila yeye ni Rais anatakiwa alete solution in a short term, tusiagize kabisa sukari kutoka nje lakini pia na bei ishuke.

Alete solution sio kuaddress/identify tatizo ambalo wote tunalijua na chanzo chake ni Utawala mbovu wa CCM.
Ukiona nchi imetulia na hakuna hata mfumuko wa Bei basi ujuwe ni kutokana na akili kubwa ya Rais Samia.akitoa tamko au maagizo anakuwa ameshafanya utafiti na kila kitu.Rais wetu ni kiongozi mtulivu na siyo wa kukurupuka
 
Too late...

Kauli hiyo hiyo amwambie Tulia amrudishe Mpina bungeni
 
Kwamba mkubwa hakosei sio,

Itisheni pia press kumuomba msamaha Ndugu Mpina.
Hoja ya Mpina uliielewa. Yeye alisema kuwa sukari iliyoagizwa ni nyingi kupita mahitaji na kiwango kinachotakiwa kuagizwa.
 
Weka hilo andiko langu nililo msifia Mheshimiwa Hussein Bashe kwa kuagiza sukari nje ya Nchi.Mimi sijawahi kuzungumza jambo lolote lile juu ya sakata hilo la sukari.

Wakati fulani uwa nacheka sana hasa chawa anapotafuta pisition bila tafakuri ya maana.
 
Ccm walivyo wapumbavu,Kwa Sasa ndiyo wataanza Tena kumsifu luhaga mpina Kwa sababu amesema rais kuwa Bashe alikosea kuagiza sukari nje bila utaratibu
 
Siasa za Tanzania ni kama mazingaombwe. Mwenye dhamana ya kubuni na kusimamia sera na mikakati ya uzalishaji wa sukari anasimama hadharani na kulalamika kuhusu hasara ya kuagiza sukari nje!

Anajiweka kando na kuwaasa kisha kuwaagiza mawaziri wake wahakikishe uzalishaji wa viwanda nchini unaimarishwa! Keshamaliza kazi. Yeye na serikali yake ni pande mbili tofauti!

Tukimhoji inakuwaje wakati wa utawala wake tatizo la sukari limekuwa kubwa na kusababisha matumizi makubwa ya pesa za umma, tunaambiwa hilo si tatizo lake bali ni la mawaziri na watendaji. Yeye alishatoa maelekezo. Watendaji wanamuangusha! The buck never stops with her!

Bila shaka kina Biden, Trump, etc. watamuonea wivu sana Rais wa JMT. Wao mfumuko wa bei ukivuka mpaka au bei ya petroli ikipanda ghafla au hata ya mkate yeye binafsi anapoteza kazi. Na hawezi kwenda kwenda hadharani na kutoa maelekezo au maagizo ya kazi kwa mawaziri wake kwenye vyombo vya habari. Hayo ni mambo ya ndani. Wananchi wanangoja kusikia habari njema tu toka serikali yake.
 
Bwana lucas njoo na uzi wa maoni yako kuhusu utetezi wa wana ccm wenzako walio mponda Mpina .Maana msiwe km bendela fuata upepo.
 
bi chura na mawaziri wako mkajibu kesi ya Mpina mahakamani, hakuna kubadili gia angani hapa
 
Back
Top Bottom