Rais Samia: Kuagiza sukari nje ya nchi ni upotevu wa pesa

Rais Samia: Kuagiza sukari nje ya nchi ni upotevu wa pesa

View attachment 3062110Ndugu zangu Watanzania,

Hayo ni Maneno ambayo yanetamkwa na Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan,huko mkoani Morogoro hii leo katika muendelezo wa ziara yake na kuzungumza na wananchi.

Ambapo amesema ya kuwa mahitaji ya sukari nchini ni Tani laki 6 na Nusu ,huku mahitaji ya sukari viwandani ni Tani Laki 2 Na nusu. Na hivyo akizitaka wizara husika kuhakikisha kuwa sukari inazalishwa na viwanda vyetu vya hapa hapa Nchini,badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi,jambo ambalo ni upotevu wa pesa za kigeni.View attachment 3062107

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili
Hizi ndio vitu watu wafanye walime NK ,hivyo nategemea watoto wao na Sisi wengine tufanye hivyo badala ya kuwapa watu WA nje. Na Kwa DP weldi na Adinan angefanya hivyo.
 
Bashe: mashamba ya kulima miwa nchini yabadilishwe kuwa mashamba ya mpunga.

Sasa Rais na waziri Wana uono tofauti na waziri Bado Yuko Ofisini.

Kwako Lucas Mwashambwa
 
Hii ndiyo Tanzania na aina ya Viongozi tulionao

Taarifa iliyoenda Bungeni na Waziri mwenye dhamana ilionesha Serikali ilikuwa sahihi kuagiza Sukari nje ya Nchi.

Leo hii Mhe. Rais ameonesha Serikali ilikosea kuagiza Sukari nje

Kwa kauli hii nategemea H. Bashe awajibishwe

Na ingekuwa Nchi za wenzetu Bunge pia lingevunjwa
Bashe alisema afadhali mashamba ya miwa yageuzwe kuwa ya mpunga ili tuendelee kuagiza sukari. Rais anasema kuagiza sukari nje ni upotevu wa pesa. Inafikirisha mtu yule yule aliyetaka mashamba ya miwa yafe, anapewa jukumu la kutayarisha sera ya kuaendeleza. TZ vituko kila kukicha.
 
Bashe alisema afadhali mashamba ya miwa yageuzwe kuwa ya mpunga ili tuendelee kuagiza sukari. Rais anasema kuagiza sukari nje ni upotevu wa pesa. Inafikirisha mtu yule yule aliyetaka mashamba ya miwa yafe, anapewa jukumu la kutayarisha sera ya kuaendeleza. TZ vituko kila kukicha.
Ningekuwa mm ndio Bashe ningejiuzulu hapo hapo.
 
Kitu ambacho Mhe. Waziri wa Kilimo alichokosea ni kuruhusu kuagiza sukari zaidi ya mahitaji ya nchi huku viwanda vya ndani vikikosa mahali pa kuuzia sukari waliozalisha.
 
Back
Top Bottom