Rais Samia kuanza safari ya kikazi nchini DR Congo

Mkuu hebu niambie unaelewaje hiyo kauli ya kipaumbele chenye tija?

Yaani kwenda kuwabembeleza majirani waendelee kutumia bandari yako na kufanya biashara na wewe sio kipaumbele chenye tija kwa definition yako? Ila kwenda china kuwaomba wafungue kiwanda cha bajaji na bodaboda kwako ndiyo kipaumbele chenye tija au sikuelewi vizuri?
 
Hizi tantarira tu
 
Mkuu hebu niambie unaelewaje hiyo kauli ya kipaumbele chenye tija?
Kila Taifa duniani lina nchi ambazo ni muhimu sana kwake kiuchumi,kisiasa na kijamii na pia lina nchi ambazo siyo muhimu sana kwake kiuchumi,kisiasa na kijamii.Ninavyosema kuwa Rais wa nchi anapaswa aanze kutembelea kwanza nchi ambazo ni kipaumbele namaanisha zile nchi ambazo ni muhimu sana kwa Taifa lake kiuchumi,kisiasa na kijamii.
Yaani kwenda kuwabembeleza majirani waendelee kutumia bandari yako na kufanya biashara na wewe sio kipaumbele chenye tija kwa definition yako?
Umetumia data gani au statistics gani au credible source gani kujua kuwa Burundi,Congo,Kenya na Rwanda zina tija kuliko nchi zingine kama vile Marekani,Uengreza,Japan,China na kadhalika kwa mfano?
Ila kwenda china kuwaomba wafungue kiwanda cha bajaji na bodaboda kwako ndiyo kipaumbele chenye tija au sikuelewi vizuri?
Halafu unaanza kuniboa.Wapi nimesema kuwa China ni kipaumbele chenye tija kwa Tanzania?Tokea nimeanza kucomment kwenye huu uzi hakuna sehemu yoyote ambayo nimetaja kuwa nchi fulani ni kipaumbele chenye tija kwa Tanzania.

Msingi wa mazungumzo yote haya ni swali ambalo nimeuliza mwanzoni kabisa mwa huu uzi kuwa Rais anapotoa kipaumbele katika kuanza kuitembelea Congo,Rwanda na Burundi hizi ndiyo nchi duniani ambazo ni kipaumbele chenye tija kwetu?Hili ni swali ambalo niliuliza watu kama wewe ili mnipe majibu ila mpaka sasa hivi hakuna mtu alienipa jibu.
 
Hilo wasema wewe, mimi nilijibu swali lako la awali. Sijui unalikukmbuka!? Hili la sasa ni swali jingine jipya na linahitaji majibu mengine mapya.
Swali nililouliza awali ndiyo hilihili labda uwe hukunielewa na ndiyo maana sasa hivi nikatumia lugha inayoeleweka zaidi ili unielewe.
 
Huyu bibi kwa umri wake mkubwa hivi hachoki kusafiri?
 
Hakuna lolote ni matumizi mabaya ya fedha za umma, toka ameshika madaraka hajawahi hata kufika Mbeya lakini tayari Rwanda na Uganda keshaenda mara 2
 
Bora afanye haya, kuliko kuuwa watu, kubambija kesi watu. In short kuonea watu kama mtangulizi wake.
 
yaani watanzania tumejisahau sana nafikiri ni kutokana na hii amani tuliyo nayo ndiyo maana kila rais anayeingia madarakani sasa hivi munamuona ana kasoro yaani sijui mnataka rais wa namna gani ? aliingia magufuli hataki safari za nje mkaanza kusema rais gani hasafiri ? amejitahidi kufanya kazi kizarendo kwa muda mchache amefanya makubwa lakini bado mnamsema vibaya mzee wa watu mpaka akaamua kurudi kwa baba yaani siku itafika nchi itakapo kua kama somalia au hata kama kenya tu kila siku tuwe tunasikia sehemu alshababu wamelipua sehemu wamekaba nafikiri ndiyo akili zitawakaa sawasasahivi bado mnaona kila kitu ni rahisi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…