Rais Samia kuanza safari ya kikazi nchini DR Congo

Rais Samia kuanza safari ya kikazi nchini DR Congo

yaani watanzania tumejisahau sana nafikiri ni kutokana na hii amani tuliyo nayo ndiyo maana kila rais anayeingia madarakani sasa hivi munamuona ana kasoro yaani sijui mnataka rais wa namna gani ? aliingia magufuli hataki safari za nje mkaanza kusema rais gani hasafiri ? amejitahidi kufanya kazi kizarendo kwa muda mchache amefanya makubwa lakini bado mnamsema vibaya mzee wa watu mpaka akaamua kurudi kwa baba yaani siku itafika nchi itakapo kua kama somalia au hata kama kenya tu kila siku tuwe tunasikia sehemu alshababu wamelipua sehemu wamekaba nafikiri ndiyo akili zitawakaa sawasasahivi bado mnaona kila kitu ni rahisi sana
Kwani Kenya inaubaya gani ukilinganisha na TZ?
 
Kwani Kenya inaubaya gani ukilinganisha na TZ?
ndugu huoni wanavyosumbuliwa na magaidi? wewe sasa hivi semea tu huo ushabiki na mimi sijayaandika haya ili kubishana natoa hadhari tu kuwa tuangalie na maisha ya wenzetu tutunze amani yetu tufanye kazi basi
 
Kila Taifa duniani lina nchi ambazo ni muhimu sana kwake kiuchumi,kisiasa na kijamii na pia lina nchi ambazo siyo muhimu sana kwake kiuchumi,kisiasa na kijamii.Ninavyosema kuwa Rais wa nchi anapaswa aanze kutembelea kwanza nchi ambazo ni kipaumbele namaanisha zile nchi ambazo ni muhimu sana kwa Taifa lake kiuchumi,kisiasa na kijamii.
Safi saana mkuu! Hebu nitajie hizo nchi sasa?

Pia nikupe Hint tu kuwa nchi ya kwanza mama kuitembelea ni Kenya ambayo kiuchumi ni miongoni mwa top 5 ya nchi zilizowekeza zaidi Tz, kijamii ndiyo sitaki kabisa kuitaja lakini naamini ndiyo nchi ambayo muingiliano wake kijamii ni mkubwa zaidi na Tz, Kisiasa hapo sina data.
 
ndugu huoni wanavyosumbuliwa na magaidi? wewe sasa hivi semea tu huo ushabiki na mimi sijayaandika haya ili kubishana natoa hadhari tu kuwa tuangalie na maisha ya wenzetu tutunze amani yetu tufanye kazi basi
Kwani ugaidi ni tatizo au ubora wa raisi?
 
1629813583793.png
1629813637378.png
1629813678028.png
1629813835362.png
1629813927741.png
hapo ni mahindra na vieite lipeni tozo tuelndelee kuwatesa
 
Kama mshauri wake ni vasco da gama unategemea nini?

Halafu nchi anazosafiri kwenda zina mchango mdogo kwenye uchumi wetu.

Asafiri kutafta wawekezaji wa maana huko Ulaya walete mitaji kutusaidia ku exploit hizi natural resources tulizonazo.

Sio muda utasikia ana ziara Somalia.

Yaani hapa tumeingia cha kike kweli.
Hii JF sikuhizi imevamiwa na watoto, kwamba DRC haina mchango wa kiuchumi kwa Tanzania? Unajua kuwa DRC ni mshirika wetu mkubwa wa Bandari ya DSM? Nyie watoto mbaki FB huko.
 
Burundi ina mchango mdogo wa uchumi kwetu?

Kenya na Rwanda zina mchango mdogo kwa uchumi wetu?

Hivi yale magari 3000 yaliyopokelewa bandarini YANAPEKEKWA "huko Ulaya usemako"?

Ulaya waje kuwekeza kitu gani?!

Kwa hiyo "REGIONAL ECONOMY" kwako ni kupoteza muda? [emoji44][emoji44]

#NchiKwanza
#KaziIendelee
#SiempreJMT
JF mevamiwa na watoto wa shule brother hawasomi taarifa, wanashinda FB tu.
 
Umetumia data gani au statistics gani au credible source gani kujua kuwa Burundi,Congo,Kenya na Rwanda zina tija kuliko nchi zingine kama vile Marekani,Uengreza,Japan,China na kadhalika kwa mfano?
Zaidi ya misaada na kuimport vitu kutoka nchi hizo ambazo mwisho wa siku wao ndiyo wanafaidika zaidi kwa kuingiza fedha kwenye nchi zao tunapata nini mpaka uone ndiyo nchi zenye kipaumbele chenye tija kwa definition zako?
 
Zaidi ya misaada na kuimport vitu kutoka nchi hizo ambazo mwisho wa siku wao ndiyo wanafaidika zaidi kwa kuingiza fedha kwenye nchi zao tunapata nini mpaka uone ndiyo nchi zenye kipaumbele chenye tija kwa definition zako?
World bank juzi wametoa mkopo wa gharama nafuu kwa Tanzania kwa ajili ya elimu,tehama ambao ni TSH 2.7 trillion.Hii hela ni nyingi sana.Tanzania inachangia nini world bank hadi ipewe hela hizi?Tanzania haichangii chochote huko kwa sababu ni masikini.

Nchi kama Marekani inachangia zaidi ya asilimia arobaini katika bank hii na inakuwa na mamlaka ya kusema kuwa ni nani apewe nini na ni nani asipewe.Sasa kama nchi inapokea mkopo wa 2.7 trillion kutoka kwa wakubwa hawa,hawa siyo kipaumbele cha Taifa?Ni nani mwingine anaweza kukupa kiasi kikubwa cha fedha namna hii?

Kumbuka pia kuwa mkopo kama huu siyo tu kwamba ni wa gharama nafuu lakini pia muda mwingine husamehewa kabisa.
 
Safi saana mkuu! Hebu nitajie hizo nchi sasa?
Nimeshaanza kuzitaja katika comment yako ya nyuma na tutazijadili sana hapa.
Pia nikupe Hint tu kuwa nchi ya kwanza mama kuitembelea ni Kenya ambayo kiuchumi ni miongoni mwa top 5 ya nchi zilizowekeza zaidi Tz, kijamii ndiyo sitaki kabisa kuitaja lakini naamini ndiyo nchi ambayo muingiliano wake kijamii ni mkubwa zaidi na Tz, Kisiasa hapo sina data.
Kwa hiyo unataka kusema kuwa Kenya ndiye kipaumbele chenye tija kwa Tanzania kuliko mataifa yote duniani?🤡🤡🤡
 
Hii ziara inaweza kuwa ya kimkakati na ya muhimu pengine kuliko ziara zote zilizofanyika toka mama aingie ikulu. Ni jambo la wazi kuwa katika nchi zote za maziwa makuu, DRC imejaaliwa kuwa na idadi kubwa ya watu takriban watu 120,000,000.

Itakumbukwa kuwa Tanzania tumejaaliwa kuwa na bandari, ambapo miongoni mwa nchi zinazotumia bandari yetu ni DRC.

Tanzania imekuwa ujenzi mkubwa wa reli ya mwendokasi ambayo inategemewa kuwa msaada mkubwa wa usafirishaji wa watu na mizigo kuelekea nchi za Rwanda, Burundi na DRC. Kimkakati, kama ujenzi huo utakamilika, Tanzania itakuwa imalamba dume kwa sababu tutaweza kujiinua kiuchumi kupitia sekta ya usafirishaji pamoja na kufaidika na masoko ya bidhaa zetu kupitia wato miliuoni miamoja waliopo mashariki mwa Kongo.

Mnyonge mnyongeni lakini haki haki yake apewe. Ziara ya Rais wetu huko DRC haipaswi kubezwa kwa sababu kiuchumi inalipa tofauti na nchi kama Rwanda, Burundi na Uganda ambazo zinapitisha mizigo yao katika bandari yetu ya Dar Es Salaam lakini, mizigo yao kidogo kuliko ile DRC kutokana na idadi ya watu katika nchi hizo ni ndogo.

Hongera Mh. Raisi wetu kwa kupanga ziara ya kimkakati ya DRC ambayo ni muhimu sana kwa musakabali wa uchumi wa nchi yetu.
Bandari kongo wanayo na sasa wamejenga barabara kuunganisha DRC na Angola ili watumie bandari makini ya antlantic
 
Back
Top Bottom