Rais Samia kufanya ziara ya kikazi nchini Korea Kusini kuanzia Mei 31 - Juni 6

Rais Samia kufanya ziara ya kikazi nchini Korea Kusini kuanzia Mei 31 - Juni 6

Hiyo taarifa inasambaa tu kwenye ukoo wenu na kogonga kwenye vichwa vyenu visivyo na akili timamu,vichwa vilivyorithi kutokuwa na akili
 
Wewe ndiye unadharauliwa na kuonekana huna akili Timamu kwa tabia yako ya kutukanana matusi utafikiri mgonjwa.
Hakuna hata anayesoma hayo magazeti yako ya kusifia,unajipa msongo wa mawazo tu kwani kamwe huwezi kuteuliwa. Wewe ni kichaa fresh. Weka hata post yangu moja tu ambayo nimetukana.
 
Jemedari anakwenda na baiskeli ama toyo? Ingeleta msisimko zaidi na hisia za kizalendo
 
Rais Samia kutunukiwa tena Udaktari wa Heshima kutoka Chuo Cha Anga Korea (KAU)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara katika Jamhuri ya Korea Kusini kuanzia leo tarehe 30 Mei 2024 hadi 6 Juni 2024 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Korea Kusini Mhe. Yoon Suk Yeol.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Jana tarehe 29 Mei 2024, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba amesema Mje. Rais Samia ataanza ziara rasmi ya uwii nchini humo itakayofanyika tarehe 1 na 2 Juni 2024.

Ziara hiyo itafuatiwa na ziara ya kikazi itakayomuwezesha kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kati ya Afrika na Korea utakaofanyika tarehe 3 na 4 Juni 2024.

Mhe. Makamba amesema ziara rasmi ya Mhe Rais Samia nchini humo inalenga pamoja na mambo mengine kukuza na kuimarisha ushirikiano na uhusiano wa kisiasa na kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili ambao umedumu kwa miaka 32 sasa tangu ulipoanzishwa mwaka 1992.

Mhe. Makamba ameongeza kuwa, akiwa nchini humo Rais Samia atakutana kwa mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Mhe. Rais Yoon Suk Yeol yatakayofanyika tarehe 2 Juni 2024.

Amesema mazungumzo hayo yatajikita kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea katika maeneo mbalimbali ikiwemo afya, elimu na miundombinu.

Mhe. Makamba amesema wakati wa ziara hiyo, mikataba saba (7) ya kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya nchi hizi mbili itasainiwa. Ametaja mkataba mmojawapo unahusu msaada wa fedha kati ya Benki ya Exim ya Korea na Tanzania ambao utaiwezesha Tanzania kupata msaada na mkopo wa masharti nafuu wa Dola za Marekani Bilioni 2.5 (sawa na Trilioni 6.5) ambao ni kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo yaani mwaka 2024/2028.

Pia amesema Hati ya Makubaliano kati ya Taasisi ya Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Taasisi ya Sayansi ya Miamba na Madini ya Korea ambayo itahusu ushirikiano katika masuala ya utafiti, uchoraji ramani na shughuli za maabara itasainiwa.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa January Makamba, amesema Dkt Samia akiwa nchini humo, pia atatunukiwa Udaktari wa heshima kutoka Chuo Kikuu cha Anga Korea (KAU) kwa lengo la kutambua mchango wake wa kuleta mabadiliko, sera na uongozi wa kimantiki.
 

Attachments

  • IMG-20240530-WA0004.jpg
    IMG-20240530-WA0004.jpg
    99.8 KB · Views: 2
Wangemfundisha na urubani awe anaendesha mwenyewe maana anapenda sana kukaa angani kuliko ofisini tuliko muajiri.
 
Korea ni kanchi kadogo sana 🤣. Kama mikoa miwili ,korea ina square kilometers laki moja, Tanzania ina square kilometers laki tisa.

Korea 100,339 km²
Tanzania 947,300km²


Anaupiga mwingi mno.
Hicho ndio kipimo, toka lini maendeleo ukubwa ukawa factor.

Tanzania 947,300km²
DRC 2,345,409 km²
 
Wangemfundisha na urubani awe anaendesha mwenyewe maana anapenda sana kukaa angani kuliko ofisini tuliko muajiri.
Lakini atapata 6.5 trillion, kuna hasara gani? Angekaa ofcn angeipata hiyo?
 
Hii ni new version ya JK yaani JK pro max.
Wa Tanzania hatujui tunataka nini. JK alisafiri sana lakini pesa zilikuwepo, watu wakamsema mpaka basi akaja JPM, yeye hakusafiri lakini alisemwa kila kona Rais gani hasafiri leo kaja anasafiri imekuwa shida tena. Nini tunataka? Je miaka ile JPM hasafiri kuna kitu kiliboreka.
 
Huku Rais akienda korea,Serikali itoe ufafanuzi kwa nini watanzania wananyimwa Visa ubalozi wa korea.mfano Mtanzania anayetaka kwenda Korea kwa safari ya biashara inatakiwa hawe na kiasi kisichopungua mil.100,000 Tsh. badala ya $10,000 iliyokuwa ikitakiwa hapo awali.
Mtanzania anayeta kwenda kusoma Korea anatakiwa hawe kiasi cha Tsh.Mil 80,000 badala ya $5,000 ya hapo awali na mengineyo...
Wizara ya Mambo ya nje nafikiri mgetoa ufafanuzi mzuri ni kwa nini watanzania wahahitaji kuonyesha kiasi kikubwa cha pesa katika ubalozi wa wakorea tofauti na hapo awali na hisitoshe unaweza kuonyesha supporting documents zako zote pamoja na hiyo pesa na bado ukanyimwa Visa bila sababu.
Serikali itoe taarifa wa nini kipindi cha nyuma watanzania walikuwa wakipewa visa na kwa sasa wa nini wananyimwa.
Nawakitaka kukunyima wanakuhitisha vitu vingi ili ushidwe kupeleka kwa wakati kisha maombi yako ya visa yanakuwa rejected.
 
Kila siku tunatajiwa mikopo na misaada ya matrillion huku hiyo miradi ya maendeleo ikisimama kwa kukosa pesa!
 
Hivi kwanini kiongozi wa China Urusi au Marekani na hata Brazil hawana ziara nyingi hivi kama hawa wa huku kwetu?
Au ndio huwa wanakwenda kuomba?
Wanasafiri sana kufanya biashara zao binafsi
 
Miaka ya 1960's nchi yetu ilikuwa inakaribiana kabisa kiuchumi na hiyo nchi!! Halafu leo hii tunachukua lidege likubwa, ndani likiwa limejaa wasanii! Kwenda kuomba mkopo wenye masharti nafuu!!

Aisee Waafrika bora mngeendelea tu kutawaliwa.
Miaka hiyo Korea ilikuwa inapigana Vita na Marekani huo uchumi wenu mliokuwa mnashinda uchi hadi watu wazima ilikuwa sawa na taifa kama hilo?
 
Back
Top Bottom