Rais Samia kufanya ziara ya kikazi Ufaransa na Ubelgiji

Rais Samia kufanya ziara ya kikazi Ufaransa na Ubelgiji

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Rais wa Tanzania, Samia anatarajia kuelekea Nchini Ufaransa na baadaye Ubelgiji kikazi. Akiwa Ufaransa, atahudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaojadili kuhusu Rasilimali Bahari Duniani.

Aidha, atashuhudia utiaji Saini baina ya Serikali ya Tanzania na Ufaransa katika sekta za Miradi ya Maendeleo, ushirikiano katika Masuala ya Uchumi wa Buluu, usalama wa Bahari, Sekta ya Usafiri na Maendeleo endelevu.

Taarifa zaidi:


1644410847256.png

 
Samia ameshindwa kuushawishi Ulimwengu kwenye kuzingatia haki. Ameshindwa kupata mwaliko wa nchi yoyote miongoni mwa yale mataifa yanayozingatia haki na demokrasia.

Amebakia tu kuvizia mikutano ambayo hata haina umuhimu mkubwa, sawa na alivyokuwa akifanya Robert Mugabe miaka ya mwisho ya utawala wake.

Hakika Samia, anasubiria kwa hamu kubwa kwisha kwa kesi ya Mbowe ili aweze kujikosha kwa kuwachukulia hatua maofisa wa polisi walioandaa hiyo kesi. Na baada ya hapo atapokelewa na mataifa mengi, akiwaacha polisi na uchafu wao huku yeye akimwagiwa sifa.

Hii kesi ya Mbowe, kuna baadhi ya maofisa wa Polisi, hawataisahau maana utakuwa ndio mwisho wao katika utumishi wa umma.
 
Rais wa Tanzania, Samia anatarajia kuelekea Nchini Ufaransa na baadaye Ubelgiji kikazi. Akiwa Ufaransa, atahudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaojadili kuhusu Rasilimali Bahari Duniani...
Naona barua ya kwanza ya Zuhura Yunus 😁😁
 
Je,Tanzania ingekuwa wapi kama ingepata kiongozi mzalendo?

1: Uchumi wa Tanzania ungekuwa wa kati daraja la juu tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Tanzania imeporomoka kutoka nafasi yake ya 8 kati ya nchi 10 zenye uchumi bora Africa mpaka nje ya top 10 na kuzidiwa na vinchi kama Ghana na Angola....hudia wale waliowachagua wakikata keki ikulu!

Wacha kazi iendelee!
Ingekuwa huku 🚮🚮
 
Back
Top Bottom