Rais Samia kufanya ziara ya kikazi Ufaransa na Ubelgiji

Rais Samia kufanya ziara ya kikazi Ufaransa na Ubelgiji

Mbona wanaficha ndege? Amechukua DREAMLINER ya ATCL nini? Kama ni hivyo hayo yatakuwa matumizi mabaya ya rasilimali za nchi!! Kuchukua ndege na kwenda kuisimamisha ikingoja mpaka ziara iishe ni gharama kubwa sana jamani.
Bora hata huyu mwaona ndege kwa vipande , Utawala wa Jakaya uliziona wapi ndege alizokua akienda nazo Marekani na Ulaya?
 
Bora hata huyu mwaona ndege kwa vipande , Utawala wa Jakaya uliziona wapi ndege alizokua akienda nazo Marekani na Ulaya?

Kwa spidi anayo kwenda nayo Hangaya ; kuwa kila akifanya ziara ya mkoani akirudi Magogoni lazima aende Ulaya, sina shaka atavunja record ya Jakaya muda si mrefu!! Hangaya anapenda sana bata hivyo kuwapa nafasi watu wake kuongezea urefu wa kamba zao!!!
 
Kama ataleta kikubwa zaidi ya hicho hakuna tatizo. Kumbuka ziara ya obama aliye paa na watu zaidi ya 800 bila kutaja walinzi na wana usalama waliotangulia na vifaa mbalimbali

Unaweza kufananisha uchumi wa Marekani na uchumi wa Bongo? Usijifanye hamnazo Bongo uchumi wake ni sawa na uchumi wa jimbo moja tu la huko Marekani!! Samia ataleta kubwa zaidi kwa kutembeza Bakuri ? Mbona Magufuli alikuwa hazuruli na wao walikuwa wanamfuata Magogoni? Samia ameambukizwa ugonjwa wa Msoga; amelishwa miguu ya kuku!!
 
Unaweza kufananisha uchumi wa Marekani na uchumi wa Bongo? Usijifanye hamnazo Bongo uchumi wake ni sawa na uchumi wa jimbo moja tu la huko Marekani!! Samia ataleta kubwa zaidi kwa kutembeza Bakuri ? Mbona Magufuli alikuwa hazuruli na wao walikuwa wanamfuata Magogoni? Samia ameambukizwa ugonjwa wa Msoga; amelishwa miguu ya kuku!!
Kila mtu anafanya kadri ya uwezo wake wewe huwezi kua mimi and vice versa
 
Pamoja na jitihada za kuifungua nchi bado Tanzania haipo katika nchi kumi bora zenye mazingira mazuri ya uwekezaji Africa kwa mwaka 2022.

 
Kama ataleta kikubwa zaidi ya hicho hakuna tatizo. Kumbuka ziara ya obama aliye paa na watu zaidi ya 800 bila kutaja walinzi na wana usalama waliotangulia na vifaa mbalimbali
mkuu, mbona kama unatupiga na kitu kizito kichwani, yani Air force one ilibeba zaidi ya watu 800 na bado ilitanguliza wengine😁
walinzi walitangulia ndio lakini kwenye jumla ya watu waliopanda Air force one haifiki hata 100
 
Rais wa Tanzania, Samia anatarajia kuelekea Nchini Ufaransa na baadaye Ubelgiji kikazi. Akiwa Ufaransa, atahudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaojadili kuhusu Rasilimali Bahari Dunian...

DDD29CE8-B7D6-4DA3-9BA7-D813F0FE233D.jpeg
 
Uchawi huu sasa,kwa hiyo ukiona neno uchumi wa blue basi unawaza Zenj,kwamba Bara hakuna Bahari sio?
tayari umesema bara, ungesema Tanganyika ungeeleweka. Asante TLS kwa kutunza jina hili, ingawa natamani tuwe na Tanzania yenye serikali moja.
 
Unasafiriji wakati hatuna umeme wakutoshekeza hii nishati inataka uwekezaji mkubwa
 
mkuu, mbona kama unatupiga na kitu kizito kichwani, yani Air force one ilibeba zaidi ya watu 800 na bado ilitanguliza wengine😁
walinzi walitangulia ndio lakini kwenye jumla ya watu waliopanda Air force one haifiki hata 100
Aliambatana na msafara wa zaidi ya watu 800. Kati ya hao kulikuwa na wafanya biashara, viongozi, walinzi wana usalama wapishi madaktari na wafanyakazi wengineo.

Nje ya perimeter ya ikulu kulikuwa na wanajeshi wa majini na vyombo vya huko tulivyo weza kuviona na ambavyo hatukuweza kuviona. Na wengine utakaopenda kujiongezea mwenyewe
 
Unaweza kufananisha uchumi wa Marekani na uchumi wa Bongo? Usijifanye hamnazo Bongo uchumi wake ni sawa na uchumi wa jimbo moja tu la huko Marekani!! Samia ataleta kubwa zaidi kwa kutembeza Bakuri ? Mbona Magufuli alikuwa hazuruli na wao walikuwa wanamfuata Magogoni? Samia ameambukizwa ugonjwa wa Msoga; amelishwa miguu ya kuku!!
Sijafananisha uchumi bali nimelinganisha ziara ambazo zinaweza kuwa na manufaa kwa nchi bila kujalisha atatumia gharama kiasi gani.

Nani alimfuata magufuli ikulu kuja kuwekeza wakati kila uchwao alikua anakopa kimyakimya, anachota fedha za wafanyabishara akishirikiana na kina lengai kupitia vyombo maalumu?
 
Je,Tanzania ingekuwa wapi kama ingepata kiongozi mzalendo?

1: Uchumi wa Tanzania ungekuwa wa kati daraja la juu tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Tanzania imeporomoka kutoka nafasi yake ya 8 kati ya nchi 10 zenye uchumi bora Africa mpaka nje ya top 10 na kuzidiwa na vinchi kama Ghana na Angola

2: Nidhamu na uwajibikaji kazini ungekuwepo.Leo hii tunashuhudia wananchi wakihoji kuhusu hali ya umeme nchini pasipokuwa na majibu au majibu yenye uwalakini. Lakini pamoja na hayo bado viongozi wamebaki wakiwa maofisini pasipo kuwajibika kwa namna yoyote.

3: Kwa miaka kadhaa Tanzania imekuwa ikiifanya juhudi kubwa kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa na ya kimkakati. Licha ya kwamba tangu Rais S.S.H aingie madarakani hakuna mradi wowote wa kimkakati ulioanzishwa bali pia hata ile miradi iliyokuwa ikiendelea imekuwa ikisuasua

4: Umeme usingekuwa wa mgao.Tangu Rais S.S.H aingie madarakani hali ya upatikanaji wa umeme nchini imekuwa mbaya sana.Hali hii imepelekea kurejea kwa mgao wa umeme ambao watanzania wengi walishausahau tangu miaka kadhaa iliyopita.Hali inayopelekea kuwatesa wananchi hususan wale wanaotegemea umeme kujipatia vipato katika shughuli zao za kila siku.

5; Hali ya upatikanaji wa maji imekuwa ya kusuasua.Kwa miezi kadhaa hususan katika jiji la Dar es salaam pamekuwa na mgao wa maji.Hali iliyopelekea kukosekana kwa maji kwa muda mrefu katika maeneo mengi.Hali ambayo hakuwahi kushuhudiwa hapo awali.

6: Tozo zisizokuwa na tija na zilizoua uchumi wa wengi.Serikali ya awamu ya sita imedhulumu na kunyang'anya kwa nguvu fedha za wananchi kwa kigezo cha tozo katika miamala ya simu.Mama mjane anapomtumia mgonjwa wake hospitali kwa ajili ya matibabu anakatwa fedha ambayo kimsingi haikuwa ya biashara. Kwa mujibu wa report kutoka Vodacom hivi karibuni miamala ya simu imepungua kwa asilimia zaidi ya 30!.Hili si jambo la kupuuza hata kidogo kwa uchumi wa nchi.Ni sawa na kutoa fedha mfuko wa kushoto na kuhamishia Kulia.

7: Kupanda kwa bei ya Mbolea.Mara tu baada ya awamu ya sita kuingia madarakani bei ya mbolea ilipanda karibu mara mbili ya bei ya awali.Hii ni imepelekea uchumi wa watanzania wengi ambao ni masikini na wanategemea kilimo kudhoofika.

8; Kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia
9; Kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol
10; Kupanda kwa bei ya bidhaa za ujenzi kama cement,Nondo n.k
11; Teuzi za viongozi wasiokuwa na weledi kwa kigezo cha favour/Undugu/Kujuana (Mf. Riziwani Kikwete,Nape Nauye n.k) Tanzania ina vijana wasomi na wenye upeo mpana wa kifikra. Lakini cha kushangaza teuzi zimekuwa hazina matumaini ta kuipeleka Tanzania kule tunapotarajia.

12: Ukosefu wa uzalendo na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma.Siku si nyingi tumeshuhudia kiongozi mkuu wa serikali akiwaasa watumishi wake wale kwa urefu wa kamba zao.Hii inaashiria kwamba hata kiongozi mkuu anashiriki katika ulaji huo.Hali hii ni hatari kwa rasilimali za nchi.

13; Wananchi hususan wa hali ya chini kukosa nafasi katika nchi yao.Siku si nyingi tumeshuhudia wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wakinyanyaswa kwa kuhamishiwa katika maeneo yasiyokuwa tija kwao.Vuta nikuvute hii imepelekea hali ya unyonge na sintofahamu miongoni mwao na kupelekea kuongezeka kwa umasikini miongoni mwa watanzania

14; Mikopo isiyokuwa na tija kwa taifa.Tangu Tanzania ipate uhuru viongozi wake wote walisisitiza kufanya mambo yetu kwa fedha zetu wenyewe bila kutegemea wahisani. Tanzania imebarikiwa rasilimali za kila aina.Mito,Maziwa,Bahari,Madini kama Tanzanite,Mbuga za wanyama,Gesi n.k Inashangaza Sana kuona kiongozi badala ya kusisitiza au kubuni namna ya kuzitumia rasilimali hizi ziweze kuwa na tija kwa watanzania,Badala yake tumekuwa tukijivunia mikopo!

15 ; Kuongezeka kwa gharama za uunganishaji umeme kutoka 27,000 iliyokuwepo mpaka zaidi ya 300,000 ya hivi sasa.Hali hii imepunguza mno kasi ya usambaaji wa umeme

16 ; Muingiliano baina ya mihimili kwa kigezo cha uchama.Inasikitisha kuona kiongozi wa mhimili mmoja anakosa uwezo wa kuikosoa na kuurekebisha mhimili mwingine kwa kuhofia kibarua chake.hili tumelishuhudia baada ya kuona spika wa bunge la JMT kujiuzulu baada ya kuhoji kuhusu mikopo na tozo.

17 ; Safari zisizokuwa na tija wala umuhimu kwa taifa.Tumeshuhudia safari nyingi mno za nje ya nchi,Safari hizi zimekuwa zikiigharimu nchi fedha nyingi.Safari za vikao visivyokuwa na tija kama mkutano wa kujadili athari za gesi ya ukaa sidhani kama ina tija hususan kwa nchi ambazo bado uchumi wake ni mdogo

18 ; Kukosekana uhuru na ukandamizaji wa demokrasia. Tunaweza kusema kwamba pia hata katika awamu zilizopita hili lilikuwepo, Lakini hili la sasa limekuja kwa namna tofauti.Wakati mwingine baba anaweza kumpa mtoto adhabu ya kulima shamba,Mtoto akalia na kulaumu sana,Lakini shamba hilohilo baadaye likaleta chakula mezani wote wakala na kufurahia. Ila tofauti iliyopo sasa,Hakuna chakula kinachokuja mezani!

19 ; Kushughulikia zaidi mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi kuliko yale yenye umuhimu na tija kwa watanzania. Imekuwa jambo la kawaida kwa awamu hii kujihusisha zaidi na makongamano,Semina elekezi,Birthday Party pamoja na hafla mbali mbali badala ya kujikita katika kufufua na kubuni miradi ya kimaendeleo itakayosaidia kuwapunguzia wananchi mzigo wa umasikini na kuinua uchumi.Hafla ya machifu na watemi si muhimu kama hafla ya utiaji saini mradi wa uchimbaji na usambazaji wa gesi ya Mtwara!

20 ; Kukosekana ajira. Ubunifu na uibuaji wa miradi mipya si tu umekuwa na tija kiuchumi Bali umekuwa ukiajiri vijana wengi.Kukosekana kwa ubunifu na sera mbovu za serikali zimesababisha kukoseka kwa ajira miongoni mwa vijana wengi

Hakika ni mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanyika kinyume na matarajio ya watanzania wengi ambao waliwaamini viongozi wao na kuwaweka madarakani huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuondokewa na maradhi, ujinga na umasikini ambao ndio maadui wakuu wa taifa kama ilivyobainishwa na Mwl Nyerere badala yake watanzania hao ambao wengi ni masikini na wameteseka kwa umasikini kiasi cha kusahau tarehe zao za kuzaliwa huku wakishuhudia wale waliowachagua wakikata keki ikulu!

Wacha kazi iendelee!
These
words are so painful brother...Nchi yetu imekuwa Jehanamu we thought things would be okay but tumeula wa Chuya hatuna cha Kufanya zaidi ya Kuangalia what will happen some years to come
 
Sijafananisha uchumi bali nimelinganisha ziara ambazo zinaweza kuwa na manufaa kwa nchi bila kujalisha atatumia gharama kiasi gani

Utakuwa mbumbumbu sana kama hutajali gharama unazotumia kwenda kutembeza bakuri huku huna uhakika hilo bakuri lako litajaa kiasi gani!! Hiyo waswahili wanaiita" BIASHARA BILA DAFTARI.................."

Wale wawekezazi wa bomba la Mafuta toka Uganda mpaka bandari ya Tanga , hawakufuatwa na Jiwe huko kwao ,walikuja wenyewe!!! Sasa nyie Chawa msivyokuwa na aibu sasa hivi mtaanza kusifia kuwa hilo bomba la Mafuta ni juhudi za Hangaya!!!
 
Ivi hii nafasi yake haina kiapo,ukiteuliwa tu unaanza kazi
Ni hivo mkuu maana nasikia kumbe hata Zuhura mwenyewe bado yuko London na ataungana na hangaya juu kwa juu huko Ulaya. Hii Taarifa kaituma kwa njia ya whatsapp.
 
Utakuwa mbumbu sana kama hutajali gharama unazotumia kwenda kutembeza bakuri huku huna uhakika hilo bakuri lako litajaa kiasi gani!! Hiyo waswahili wanaiita" BIASHARA BILA DAFTARI.................."

Wale wawekezazi wa bomba la Mafuta toka Uganda mpaka bandari ya Tanga , hawakufuatwa na Jiwe huko kwao ,walikuja wenyewe!!! Sasa nyie Chawa msivyokuwa na aibu sasa Hivi mtaanza kusifia kuwa hilo bomba la Mafuta ni juhudi za Hangaya!!!
Ipo hivi
Reli inaendelea kujengwa
Mradi wa umeme rufiji unaendelea.
Ame endorse fedha ili ndege zaidi ziletwe
Wafanyakazi wamepandishwa madaraja ambayo yalishindikana kwa zaidi ya miaka 7
Bandari ya kigoma kupanuliwa na kuboreshwa.
Reli ya kisasa kujengwa hadi kigoma ikichana ardhi ya tabora
Huyo Jiwe wako alifanya hayo kwa namna aliyo ona inafaa. Na huyu anafanya kwa namna anayo ona inafaa

yote YANAFANYIKA BILA KUTUMIA MISIMAMO YA KIKUDA YA AWAMU ILIYO PITA.
 
Back
Top Bottom