11 February 2022
Paris, France
LIVE :
Mh. Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya mkutano wa One Ocean Summit
Mh. Rais Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya mkutano wa One Ocean Summit unaoendelea jijini Paris Ufaransa unaozungumzia uchumi wa blue, usalama wa bahari, utunzaji wa mazingira ya bahari ya viumbe bahari, mikoko, matumbawe, mkakati wa kupunguza hewa ya mkaa (carbon), mabadiliko ya tabia nchi yanayotishia kumeza nchi-visiwa za baharini kama Tonga, Fiji, Mauritius, Zanzibar n.k
Mkutano huo upo chini ya uenyekiti wa rais Emmanuel Macron wa France, na nchi hiyo ndiyo inakalia kiti cha urais wa Jumuiya ya Ulaya EU kwa miezi sita kuanzia January 2022 na amechagiza uwepo wa kufuatilia kwa umakini uchumi wa buluu unaoihusu na kuigusa dunia yote.
Mbali ya viongozi wa kisiasa , wanahudhuri viongozi wa makampuni makubwa ya TEHAMA na teknolojia kama Apple, wamiliki wa kampuni kubwa za usafiri wa meli baharini, mabenki makubwa n.k ambao wote wameahidi kuchangia pakubwa katika uchumi wa buluu
LIVE: French President Macron chairs One Ocean summit
French President Emmanuel Macron chairs a segment of the One Ocean Summit, aimed at giving a strong political impetus to maritime issues.
Source : Reuters