Rais Samia kufanya ziara ya kikazi Ufaransa na Ubelgiji

Rais Samia kufanya ziara ya kikazi Ufaransa na Ubelgiji

Mbona kila mtu humu anakuwa kama haoni kuwa BAHARI ndo ISHAUZWA?

Ze kiki ndo inazungumza kwa sasa!
 
sawa mkuu wacha nifuatilie kuhusu hii idadi
Ngoja nikumegulie kidogo.
Hata gari lake lilisafirishwa kwa ndege kuja huku sasa anakuja mtu mmoja anashangaa eti ziara ya hangaya inakula pesa nyingi.
obama car.jpg

Pia soma hapa
RAIS wa Marekani, Bw. Barack Obama, atakuwa na ujumbe wa watu 700 katika ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania kuanzia Julai Mosi mwaka huu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, aliyasema hayo Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema kutokana na ziara ya kiongozi huyo, alitoa wito kwa wafanyabiashara wenye hoteli, migahawa, magari ya kukodisha waziboreshe biashara zao ili Wizara hiyo iingie mkataba nao.

Aliongeza kuwa, akiwa nchini, Bw. Obama atafanya mkutano na viongozi wa nchi zinazoendelea kwa kuzungumzia umuhimu wa sayansi na teknolojia katika nchi zao.

“Ugeni huo ni mkubwa, ujio wa kiongozi huyu utaisaidia nchi kupata pesa
za Miradi ya Changamoto za Milenia (MCC), ambazo zitatumika katika maji, elimu na barabara.

“Pia Rais Obama atazungumzia jinsi nchi za Afrika zitakavyopata umeme wa kutosha tofauti na sasa...kimsingi tumejiandaa katika mapokezi yake hata kwenye mavazi,” alisema Bw. Membe.

Hata hivyo, Bw. Membe alisema tayari baadhi ya ujumbe ambao ataongozana nao umeanza kuwasili nchini kwa matayarisho
Hapa akiwa na the late Mahiga
Screenshot_20220209-221650.png

Na hapa akiwa na kikwete
Screenshot_20220209-221704.png
 
Mama Kasema ana mpango w Kuleta Satellite [emoji341] mpya kasi ya Mtandao iongezeke data zetu za Anuani ya Makazi ziwe centralized awe anatushughulikia vizuri
 
Kinachouma dharau za watumishi wa serikali zimerudi kwa kasi. Wiki mbili zilizopita nilishuhudia mzee mmoja akifokewa na hakimu mmoja mfawidhi . Niliongea na yule mzee alibaki anasikitika akisema yule binti yaani hakimu ni sawa na binti yangu wa tano hakustahili kunikosea heshima vile. Awamu hii tutashuhudia mengi nidhamu kazini imeondoka na JPM
 
..labda dereva wa Tundu Lissu atakamatwa na kurejeshwa Tanzania.

..serikali sasa haina kisingizio tena kwamba Lissu amsalimishe dereva wake ili ahojiwe.

..Watu wa usalama watakaoambatana na Raisi wanao uwezo wa kuwahoji Lissu na dereva hukohuko Ubelgiji.

Cc Tindo, Erythrocyte, Nguruvi3 , Pascal Mayalla
 
Yanayofanyika huo bara ungeyaona usingeandika huu uharo ulioandika.
Kuongezewa tozo..kuongeza mikopo na kuwapa wazenji mgao mkubwa kupindukia..huku wazenji wakifutiwa ada za kuunganisha umeme wakati watanganyika ada za umeme zikiongezwa..au unaongelea yepi wewe mchamba wima.

#MaendeleoHayanaChama
 
Rais wa Tanzania, Samia anatarajia kuelekea Nchini Ufaransa na baadaye Ubelgiji kikazi. Akiwa Ufaransa, atahudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaojadili kuhusu Rasilimali Bahari Duniani.

Aidha, atashuhudia utiaji Saini baina ya Serikali ya Tanzania na Ufaransa katika sekta za Miradi ya Maendeleo, ushirikiano katika Masuala ya Uchumi wa Buluu, usalama wa Bahari, Sekta ya Usafiri na Maendeleo endelevu.

Taarifa zaidi:


Hivi hu mwaka alikua ajasafiri, ila sio mbaya amekuja na safari mbili KWa mpigo
 
Rais anatekeleza ilani ya ccm. Kwenye ilani ya ccm bara hakuna habari za uchumi wa blue. Habari hizo utazipata kwa Rais mwinyi Zanzibar. So ziara hii inaibeba zanzibar
Unataka kusema ilani ya CCM haijasema chochote kuhusu mambo ya uvuvi ?
Kuhusu kufufua shirika la uvuvi TAFICO, kuhusu kununua meli nane za uvuvi (nne bara, nne Zanzibar), kuhusu kujenga bandari maalum ya uvuvi kule Lindi ?

Hebu kuwa serious mkuu. Au hayo mambo haya uhusiano na uchumi wa bluu ? Ni mambo yanayohusiana na sekta ya madini, mawasiliano au gesi na mafuta ?

Tuache kidogo.
 
Unasafiriji wakati hatuna umeme wakutoshekeza hii nishati inataka uwekezaji mkubwa
Kwamba Rais asisafiri hadi matengenezo ya visima vya gesi vinavyozalisha umeme yakamilike ?

Kwani Mh. Samia ni fundi mchundo kwamba idadi ya washika bisibisi inapungua huko site ?

Ila hii nchi.
 
Je,Tanzania ingekuwa wapi kama ingepata kiongozi mzalendo?

1: Uchumi wa Tanzania ungekuwa wa kati daraja la juu tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Tanzania imeporomoka kutoka nafasi yake ya 8 kati ya nchi 10 zenye uchumi bora Africa mpaka nje ya top 10 na kuzidiwa na vinchi kama Ghana na Angola

2: Nidhamu na uwajibikaji kazini ungekuwepo.Leo hii tunashuhudia wananchi wakihoji kuhusu hali ya umeme nchini pasipokuwa na majibu au majibu yenye uwalakini. Lakini pamoja na hayo bado viongozi wamebaki wakiwa maofisini pasipo kuwajibika kwa namna yoyote.

3: Kwa miaka kadhaa Tanzania imekuwa ikiifanya juhudi kubwa kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa na ya kimkakati. Licha ya kwamba tangu Rais S.S.H aingie madarakani hakuna mradi wowote wa kimkakati ulioanzishwa bali pia hata ile miradi iliyokuwa ikiendelea imekuwa ikisuasua

4: Umeme usingekuwa wa mgao.Tangu Rais S.S.H aingie madarakani hali ya upatikanaji wa umeme nchini imekuwa mbaya sana.Hali hii imepelekea kurejea kwa mgao wa umeme ambao watanzania wengi walishausahau tangu miaka kadhaa iliyopita.Hali inayopelekea kuwatesa wananchi hususan wale wanaotegemea umeme kujipatia vipato katika shughuli zao za kila siku.

5; Hali ya upatikanaji wa maji imekuwa ya kusuasua.Kwa miezi kadhaa hususan katika jiji la Dar es salaam pamekuwa na mgao wa maji.Hali iliyopelekea kukosekana kwa maji kwa muda mrefu katika maeneo mengi.Hali ambayo hakuwahi kushuhudiwa hapo awali.

6: Tozo zisizokuwa na tija na zilizoua uchumi wa wengi.Serikali ya awamu ya sita imedhulumu na kunyang'anya kwa nguvu fedha za wananchi kwa kigezo cha tozo katika miamala ya simu.Mama mjane anapomtumia mgonjwa wake hospitali kwa ajili ya matibabu anakatwa fedha ambayo kimsingi haikuwa ya biashara. Kwa mujibu wa report kutoka Vodacom hivi karibuni miamala ya simu imepungua kwa asilimia zaidi ya 30!.Hili si jambo la kupuuza hata kidogo kwa uchumi wa nchi.Ni sawa na kutoa fedha mfuko wa kushoto na kuhamishia Kulia.

7: Kupanda kwa bei ya Mbolea.Mara tu baada ya awamu ya sita kuingia madarakani bei ya mbolea ilipanda karibu mara mbili ya bei ya awali.Hii ni imepelekea uchumi wa watanzania wengi ambao ni masikini na wanategemea kilimo kudhoofika.

8; Kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia
9; Kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol
10; Kupanda kwa bei ya bidhaa za ujenzi kama cement,Nondo n.k
11; Teuzi za viongozi wasiokuwa na weledi kwa kigezo cha favour/Undugu/Kujuana (Mf. Riziwani Kikwete,Nape Nauye n.k) Tanzania ina vijana wasomi na wenye upeo mpana wa kifikra. Lakini cha kushangaza teuzi zimekuwa hazina matumaini ta kuipeleka Tanzania kule tunapotarajia.

12: Ukosefu wa uzalendo na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma.Siku si nyingi tumeshuhudia kiongozi mkuu wa serikali akiwaasa watumishi wake wale kwa urefu wa kamba zao.Hii inaashiria kwamba hata kiongozi mkuu anashiriki katika ulaji huo.Hali hii ni hatari kwa rasilimali za nchi.

13; Wananchi hususan wa hali ya chini kukosa nafasi katika nchi yao.Siku si nyingi tumeshuhudia wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wakinyanyaswa kwa kuhamishiwa katika maeneo yasiyokuwa tija kwao.Vuta nikuvute hii imepelekea hali ya unyonge na sintofahamu miongoni mwao na kupelekea kuongezeka kwa umasikini miongoni mwa watanzania

14; Mikopo isiyokuwa na tija kwa taifa.Tangu Tanzania ipate uhuru viongozi wake wote walisisitiza kufanya mambo yetu kwa fedha zetu wenyewe bila kutegemea wahisani. Tanzania imebarikiwa rasilimali za kila aina.Mito,Maziwa,Bahari,Madini kama Tanzanite,Mbuga za wanyama,Gesi n.k Inashangaza Sana kuona kiongozi badala ya kusisitiza au kubuni namna ya kuzitumia rasilimali hizi ziweze kuwa na tija kwa watanzania,Badala yake tumekuwa tukijivunia mikopo!

15 ; Kuongezeka kwa gharama za uunganishaji umeme kutoka 27,000 iliyokuwepo mpaka zaidi ya 300,000 ya hivi sasa.Hali hii imepunguza mno kasi ya usambaaji wa umeme

16 ; Muingiliano baina ya mihimili kwa kigezo cha uchama.Inasikitisha kuona kiongozi wa mhimili mmoja anakosa uwezo wa kuikosoa na kuurekebisha mhimili mwingine kwa kuhofia kibarua chake.hili tumelishuhudia baada ya kuona spika wa bunge la JMT kujiuzulu baada ya kuhoji kuhusu mikopo na tozo.

17 ; Safari zisizokuwa na tija wala umuhimu kwa taifa.Tumeshuhudia safari nyingi mno za nje ya nchi,Safari hizi zimekuwa zikiigharimu nchi fedha nyingi.Safari za vikao visivyokuwa na tija kama mkutano wa kujadili athari za gesi ya ukaa sidhani kama ina tija hususan kwa nchi ambazo bado uchumi wake ni mdogo

18 ; Kukosekana uhuru na ukandamizaji wa demokrasia. Tunaweza kusema kwamba pia hata katika awamu zilizopita hili lilikuwepo, Lakini hili la sasa limekuja kwa namna tofauti.Wakati mwingine baba anaweza kumpa mtoto adhabu ya kulima shamba,Mtoto akalia na kulaumu sana,Lakini shamba hilohilo baadaye likaleta chakula mezani wote wakala na kufurahia. Ila tofauti iliyopo sasa,Hakuna chakula kinachokuja mezani!

19 ; Kushughulikia zaidi mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi kuliko yale yenye umuhimu na tija kwa watanzania. Imekuwa jambo la kawaida kwa awamu hii kujihusisha zaidi na makongamano,Semina elekezi,Birthday Party pamoja na hafla mbali mbali badala ya kujikita katika kufufua na kubuni miradi ya kimaendeleo itakayosaidia kuwapunguzia wananchi mzigo wa umasikini na kuinua uchumi.Hafla ya machifu na watemi si muhimu kama hafla ya utiaji saini mradi wa uchimbaji na usambazaji wa gesi ya Mtwara!

20 ; Kukosekana ajira. Ubunifu na uibuaji wa miradi mipya si tu umekuwa na tija kiuchumi Bali umekuwa ukiajiri vijana wengi.Kukosekana kwa ubunifu na sera mbovu za serikali zimesababisha kukoseka kwa ajira miongoni mwa vijana wengi

Hakika ni mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanyika kinyume na matarajio ya watanzania wengi ambao waliwaamini viongozi wao na kuwaweka madarakani huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuondokewa na maradhi, ujinga na umasikini ambao ndio maadui wakuu wa taifa kama ilivyobainishwa na Mwl Nyerere badala yake watanzania hao ambao wengi ni masikini na wameteseka kwa umasikini kiasi cha kusahau tarehe zao za kuzaliwa huku wakishuhudia wale waliowachagua wakikata keki ikulu!

Wacha kazi iendelee!
Punguza sauti, vichaa watakuita Sukuma gang ingawa yumkini unaweza ukawa mmakua wa kule newala
 
Kuongezewa tozo..kuongeza mikopo na kuwapa wazenji mgao mkubwa kupindukia..huku wazenji wakifutiwa ada za kuunganisha umeme wakati watanganyika ada za umeme zikiongezwa..au unaongelea yepi wewe mchamba wima.

#MaendeleoHayanaChama
Unajua muogopeni mungu kwa uongo wa namna hii

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Rais wa Tanzania, Samia anatarajia kuelekea Nchini Ufaransa na baadaye Ubelgiji kikazi. Akiwa Ufaransa, atahudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaojadili kuhusu Rasilimali Bahari Duniani.

Aidha, atashuhudia utiaji Saini baina ya Serikali ya Tanzania na Ufaransa katika sekta za Miradi ya Maendeleo, ushirikiano katika Masuala ya Uchumi wa Buluu, usalama wa Bahari, Sekta ya Usafiri na Maendeleo endelevu.

Taarifa zaidi:



8F8C4FDE-908C-4583-BDF9-5A79D3302266.jpeg
 
Rais kamfukuze huyo mkimbizi feki wa Ubelgiji analelewa na Amsterdam.

Mwambie arudi Singida kula kwa jasho lake kupitia kilimo cha vitunguu
Hadi SSH ameomba kutembelea Belgium unafikiri ni mchezo. Hapo Rais anavizia namna ya kuonana na Lissu. Wait and see. Wewe poyoyo endelea kupiga mikelele huko umatumbini.
 
Nimeona tu sahihi ya Zuhura Yunus, hayo mengine yaendelee
 
Back
Top Bottom