Rais Samia kufanya ziara ya kikazi Ufaransa na Ubelgiji

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Rais wa Tanzania, Samia anatarajia kuelekea Nchini Ufaransa na baadaye Ubelgiji kikazi. Akiwa Ufaransa, atahudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaojadili kuhusu Rasilimali Bahari Duniani.

Aidha, atashuhudia utiaji Saini baina ya Serikali ya Tanzania na Ufaransa katika sekta za Miradi ya Maendeleo, ushirikiano katika Masuala ya Uchumi wa Buluu, usalama wa Bahari, Sekta ya Usafiri na Maendeleo endelevu.

Taarifa zaidi:



 
Samia ameshindwa kuushawishi Ulimwengu kwenye kuzingatia haki. Ameshindwa kupata mwaliko wa nchi yoyote miongoni mwa yale mataifa yanayozingatia haki na demokrasia.

Amebakia tu kuvizia mikutano ambayo hata haina umuhimu mkubwa, sawa na alivyokuwa akifanya Robert Mugabe miaka ya mwisho ya utawala wake.

Hakika Samia, anasubiria kwa hamu kubwa kwisha kwa kesi ya Mbowe ili aweze kujikosha kwa kuwachukulia hatua maofisa wa polisi walioandaa hiyo kesi. Na baada ya hapo atapokelewa na mataifa mengi, akiwaacha polisi na uchafu wao huku yeye akimwagiwa sifa.

Hii kesi ya Mbowe, kuna baadhi ya maofisa wa Polisi, hawataisahau maana utakuwa ndio mwisho wao katika utumishi wa umma.
 
Rais wa Tanzania, Samia anatarajia kuelekea Nchini Ufaransa na baadaye Ubelgiji kikazi. Akiwa Ufaransa, atahudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaojadili kuhusu Rasilimali Bahari Duniani...
Naona barua ya kwanza ya Zuhura Yunus 😁😁
 
Ingekuwa huku 🚮🚮
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…