Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,637
- 8,947
Ndio umejua Leo?Kwani nani kaianzisha!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio umejua Leo?Kwani nani kaianzisha!
Wewe ni chizi, ndio nimejua leo.Ndio umejua Leo?
Hili ni la kuzingatia sana, sana, sanaMagufuli aliwadhibiti vizuri sana Manyang'au..
Samia asilegeze
Jambo la kwanza, nadhani mama ni lazima aambiwe kwamba Kenya sio majirani zetu pekee, kiasi cha kumchukulia muda wake mwingi kushughulika nao.Hili ni la kuzingatia sana, sana, sana
Hawa Wakenya wanataka kumlainisha Mama ili afuate wanayotaka wao kwa faida yao.
Kwakweli Mama Samia anapaswa aendelee kukaza kama JPM alivyowafanya na sio kulegeza
Wewe ni yoghurt ?Wewe ni chizi, ndio nimejua leo.
Jambo la kwanza, nadhani mama ni lazima aambiwe kwamba Kenya sio majirani zetu pekee, kiasi cha kumchukulia muda wake mwingi kushughulika nao.
Tunao majirani zetu wengine ambao kwa kweli hatujafanya juhudi kubwa za kushirikiana nao. Hata Uganda mwenyewe, nchi ambayo tumeimwagia damu zetu, mpakani kuna njia moja tu hapo Mtukula inayotuunganisha, Kenya karibuni tunazo njia nne kuu za mwingiliano kati yetu; tena barabara zote zimechongwa vizuri.
Kwa nini sasa tuingie gharama nyingine tena kujenga barabara ya kuambaambaa pwani toka Malindi hadi Bagamoyo?
Kwa nini, angalao tusitumie pesa ya namna hiyo kuimarisha bandari ya kutuunganisha kwa uhakika zaidi na DRC ambao hatuna hata njia moja ya moja kwa moja kati ya nchi hizi?
Ninachoona kilichobaki kati yetu na Kenya, ni wao kutusambazia uchafu wao wa rushwa na ufisadi ili vishamiri zaidi hapa kama vilivyo huko kwao.
Hii ndiyo hatari kubwa tunayoweza kukumbana nayo kama tutalegeza misimamo aliyokuwa ameiweka marehemu Magufuli.