Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea kudumisha diplomasiano na mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Kenya pia Rais Samia Suluhu amezungumza na Rais Mteule wa Kenya, William Ruto na wameafiki kukuza ushirikiano katika biashara, kilimo na usalama kwa manufaa ya nchi zote. Uuzaji wa bidhaa za Tanzania nchini Kenya ulikua kufikia 6.2% mwaka 2021 kutoka 3.8% mwaka 2020.
Baada ya mazungumzo Rais Mteule Ruto amesema, "Tutapanua ushirikiano wetu na Tanzania katika masuala ya biashara, kilimo, usalama miongoni mwa maeneo mengine yenye maslahi, kando na kufanya kazi pamoja katika moyo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa manufaa yetu sisi sote", William Ruto.
Mwaka 2021 Tanzania na Kenya zilitatua vikwazo 56 vya kibiashara, hivyo biashara ikakua kufikia zaidi ya TZS trilioni 2.3.
Hivyo Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea kuimarisha Diplomasia ya Uchumi. Tuendelee kumuombea Rais wetu maana kazi anayoifaya ya kuleta maendeleo ni kubwa sana.