Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
. Kwenye ulinzi lazima kuwe na mkubwa wao, yawezekana jana mtu wa aina hiyo hakuwepo...Maafisa usalama wa kike wana kazi gani Sasa.....ina maana Msikitini kuna usalama mdogo ukilinganisha na anapokuwa nje ya Msikiti. Pengine tunaweza kusema hii ni dharau Kwa walinzi wa kike au wanawake wanasemaje!?
. Siku zote unavyo mlinda Rais akili iamin hali si shwari(kujisahau hakutakiwi),Hakuna sababu yoyote yenye mashiko kuhusu hili. kwa iamni ya kikristo tumekatazwa kuvaa mavazi yampasayo mwamke. kama ni jambo la kawaida kama ulivyosema kwanini asingevaa kawaida tu ama akavaa kanzu?
Kama kulikuwa na tishio la kiusalama kulikuwa na ulazima gani yeye kwenda kwenye mkusanyiko wa wengi huku hali si shwari? kama imani zenu ni haba kwanini muende kuharibu utaratibu wa imani za wengine?
Ungetupia na nukuu aka sura na aya.Assalamu 'alaikum. Kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.), wanaume na wanawake wanasali katika sehemu tofauti wakati wa ibada katika msikiti. Hii ni kwa sababu ya mambo ya utaratibu na adabu katika ibada.
Kuhusu mavazi, Mtume (s.a.w.) ameamuru wanaume wavae kanzu au nguo ndefu zinazofunika kiganja na magoti. Wanawake wamekwishaelekezwa kuvaa hijab, yaani kufunika vichwa, nyuso na mabega yao wakati wa ibada. Hii ni kwa ajili ya heshima na adabu katika kuabudu.
Hivyo basi, wanaume na wanawake wanasali katika sehemu tofauti, na wanaume wanavaa kanzu au nguo ndefu wakati wa ibada, wakati wanawake wanavaa hijab. Haya ni mafundisho yaliyotolewa na Mtume Muhammad (s.a.w.) kwa ajili ya uadilifu na utaratibu wa ibada.
Kweli Wewe ni Vichekesho , cha ajabu ni nini hapo, acha Vichekesho vyako hapa Jf.Mohamed Said , THE BIG SHOW , bila kumsahau bibi FaizaFoxy kumbe dini yenu inaruhusu haya mambo? Dooh, kweli mtume na allah waliwarithisha vitimbi.
Dera na kanzu vyote ni vitambaa, Tofauti ni ushonaji tu..Labda upo sahihi.
Swalo ni je? Kwanini hakuvaa kanzu avae dera?
Usije sema kuvaa deara ni Sunna
😊😊😊, Nalo ni jibu zuri pia... Yawezekana ni sura ya kazi ile,Mijadara imekuwa mingi sana kuhusu rais kuingia na PSU mwanamke ambae anaonekana ni ngangari kweli kweli Na yuko serious Na kazi yake....pale hakuna mwanaume wadau acheni kuwapotosha watanzania....
Mambo mengine kama haya ni kupoteza muda kuyajadili,Rais SSH kuingia na mlinzi wa kiume mskitini ni jambo la kawaida kutokana na sababu mbali mbali , hasa kama kuna tishio la usalama au kutokana na idadi kubwa ya watu wanaokusanyika kwa pamoja.
Tujiepushe na mihemko isiyo na tija na badala yake tufikirie suluhisho zinazojenga na kuheshimu maadili ya jamii husika na kuhakikisha usalama na utulivu wa Rais.
Katika Quran, hakuna aya inayosema moja kwa moja kuwa ni marufuku kwa mwanaume kuingia sehemu ya wanawake msikitini. hadithi za Mtume Muhammad (S.A.W) pamoja na mila na desturi za Kiislamu. Kwa mfano, katika hadithi za Mtume Muhammad (S.A.W), kuna maelekezo yanayohimiza heshima na mipaka baina ya wanaume na wanawake wakati wa ibada ili kuepusha fitna na kudumisha heshima.( kuepusha matamanio ya kimapenzi ndani ya ibada. )
Ibn 'Umar aliripoti kwamba Mtume Muhammad (S.A.W) alisema, "Usiwazuie wanawake wa Allah kwenda kwenye misikiti ya Allah" (Sahih Muslim, Kitabu 4, Hadithi 891). Hadithi hii inaonyesha kwamba wanawake wanaruhusiwa kwenda msikitini, lakini haina amri maalum kuhusu maeneo maalum ndani ya msikiti. Kwa hiyo, mpangilio wa ndani wa msikiti kuhusu maeneo ya wanawake na wanaume unaweza kutegemea mila, desturi, na mantiki za kiutawala za msikiti huo na siyo tamko la S. A. W.
Katika mazingira ambapo kuna haja ya kuwepo na walinzi wa kiume kwa sababu za kiusalama, ni kwamba tunahakikisha hatua hizi zinachukuliwa kwa njia inayoheshimu mipaka ya kijinsia na dini, kulinda usalama bila kuvuruga utulivu wa ibada.( na hiki ndo amefanya RAIS SSH wa JMT)
Mtazamo huu unategemea hadithi kama ile inayosimuliwa na Umm Atiyyah, ambaye alisema kwamba wanawake waliokuwa kwenye hedhi waliambiwa wakae mbali na mahali pa kusalia/swalia wakati wa sala za Eid (imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim)
Surah Al-Baqarah (2:222), "Wanakuuliza habari ya hedhi. Sema: Huu ni unajisi. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi, wala msiwakaribie mpaka watwahare.( Tusilaumu sana yawezekana mlinzi wa kike alikuwa kwenye Surah Al-Baqarah 2:222 ).
Pia soma: Mlinzi wa kiume wa Rais kuvaa juba (vazi la kike) na kuketi msikitini sehemu ya wanawake ni sawa?
Na wewe unavaaga dera?Dera na kanzu vyote ni vitambaa, Tofauti ni ushonaji tu..
Kwa hiyo mfumo wa kiulinzi jana waliamua kutumia dera zaidi. Ila siku zinazokuja watatumia kanzu
Huyo mzilikande mmemfanya reference ya kila jambo 😂,he is no moreIngekua kwa JPM kelele zingekua nyiingii oohoo anaogopa mpaka analindwa sana. Ukweli usemwe jamaa kaharibu kuvaa ushungi
Hoja kuntu ñdugu,naunga mkono hoja yako.Mambo mengine kama haya ni kupoteza muda kuyajadili,
Tujadili mambo ya msingi kama Katiba mpya na mambo ya Tume huru ya Uchaguzi !
Mambo ya Usalama wa Rais tuwaachie wana usalama wenyewe maana sisi ni mbumbumbu Mzungu wa reli kwenye fani hiyo 👍
Huyo mzilikande mmemfanya reference ya kila jambo 😂,he is no more