Rais Samia kuingia na mlinzi wa kiume msikitini, ni jambo la kawaida. Tuache Mihemko isiyo na Tija

Rais Samia kuingia na mlinzi wa kiume msikitini, ni jambo la kawaida. Tuache Mihemko isiyo na Tija

Nchi imejaa vilaza kila mahala
Watawala wa Kiafrika wana uoga wa ajabu sana! Inakuwaje sasa mwanaume avae mavazi ya kike na kujichanganya kwa wanawake ndani ya nyumba ya ibada!!

Yaani ndiyo kusema walinzi wa kike hawana uwezo wa kumlinda Boss wao sehemu kama hiyo!!
Kwa kweli kama ni mwanaume, basi idara imechemsha. 😂
 
Rais SSH kuingia na mlinzi wa kiume mskitini ni jambo la kawaida kutokana na sababu mbali mbali , hasa kama kuna tishio la usalama au kutokana na idadi kubwa ya watu wanaokusanyika kwa pamoja.

Tujiepushe na mihemko isiyo na tija na badala yake tufikirie suluhisho zinazojenga na kuheshimu maadili ya jamii husika na kuhakikisha usalama na utulivu wa Rais.

Katika Quran, hakuna aya inayosema moja kwa moja kuwa ni marufuku kwa mwanaume kuingia sehemu ya wanawake msikitini. hadithi za Mtume Muhammad (S.A.W) pamoja na mila na desturi za Kiislamu. Kwa mfano, katika hadithi za Mtume Muhammad (S.A.W), kuna maelekezo yanayohimiza heshima na mipaka baina ya wanaume na wanawake wakati wa ibada ili kuepusha fitna na kudumisha heshima.( kuepusha matamanio ya kimapenzi ndani ya ibada. )

Ibn 'Umar aliripoti kwamba Mtume Muhammad (S.A.W) alisema, "Usiwazuie wanawake wa Allah kwenda kwenye misikiti ya Allah" (Sahih Muslim, Kitabu 4, Hadithi 891). Hadithi hii inaonyesha kwamba wanawake wanaruhusiwa kwenda msikitini, lakini haina amri maalum kuhusu maeneo maalum ndani ya msikiti. Kwa hiyo, mpangilio wa ndani wa msikiti kuhusu maeneo ya wanawake na wanaume unaweza kutegemea mila, desturi, na mantiki za kiutawala za msikiti huo na siyo tamko la S. A. W.

Katika mazingira ambapo kuna haja ya kuwepo na walinzi wa kiume kwa sababu za kiusalama, ni kwamba tunahakikisha hatua hizi zinachukuliwa kwa njia inayoheshimu mipaka ya kijinsia na dini, kulinda usalama bila kuvuruga utulivu wa ibada.( na hiki ndo amefanya RAIS SSH wa JMT)

Mtazamo huu unategemea hadithi kama ile inayosimuliwa na Umm Atiyyah, ambaye alisema kwamba wanawake waliokuwa kwenye hedhi waliambiwa wakae mbali na mahali pa kusalia/swalia wakati wa sala za Eid (imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim)

Surah Al-Baqarah (2:222), "Wanakuuliza habari ya hedhi. Sema: Huu ni unajisi. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi, wala msiwakaribie mpaka watwahare.( Tusilaumu sana yawezekana mlinzi wa kike alikuwa kwenye Surah Al-Baqarah 2:222 ).

Pia soma: Mlinzi wa kiume wa Rais kuvaa juba (vazi la kike) na kuketi msikitini sehemu ya wanawake ni sawa?
Kweli kujadili hili pia ni ushamba!! Masuala nyeti ya nchi yanahitaji wakati mwingine watu wafikie kuvaa hivyo. Mi sioni shida na ningekuwa ndo mlinzi wake hadi wanja ningeweka na lipstick plus hinna
 
Watawala wa Kiafrika wana uoga wa ajabu sana! Inakuwaje sasa mwanaume avae mavazi ya kike na kujichanganya kwa wanawake ndani ya nyumba ya ibada!!

Yaani ndiyo kusema walinzi wa kike hawana uwezo wa kumlinda Boss wao sehemu kama hiyo!!
Tumetia aibu sana mkuu
 
Ndo available hijab 🧕 1
Kweli kujadili hili pia ni ushamba!! Masuala nyeti ya nchi yanahitaji wakati mwingine watu wafikie kuvaa hivyo. Mi sioni shida na ningekuwa ndo mlinzi wake hadi wanja ningeweka na lipstick plus hinna
sasa ndo sheikh ikitokea kamuelewa akamtongoza ingekuwaje?
Haya mwamba na hijab yake tumbo la kuhara limemshika atakwenda choo gani.kwani usalama wa kike hamnaa.basi angevaa hata NINJA.
😃😃😃😃
 
Ukiachana na mwanaume kuswali na akina mama .

Pia katika uislam ni makosa mwanaume kuvaa mavazi ya kike.

Katika zama hiz za mapambano ya ushoga Ikulu inatoa ujumbe gani kwa kumvalisha mwanaume mavazi ya mwanamke?

Kuvaa vile ni kutaka aonekane yeye ni mwanamke kitu ambacho si kweli na ni maigizo ,,, maigizo kwenye nyumba ya ibada?
 
Wagalatia ndio wanapata tabu , mpaka nashangaa na hawana elimu ya uislamu....Wanawake mule hawapo uchi .

Kule Mecca walinzi ni wakina sehemu zote?
 
Ingekua kwa JPM kelele zingekua nyiingii oohoo anaogopa mpaka analindwa sana. Ukweli usemwe jamaa kaharibu kuvaa ushungi
Ebu niambie alicho haribu ni nini...???
 
Kidini sio sawa hizo ni element za Ushoga, kwanini mwanaume avalishwe mavazi ya kike. Mbona Gadafi ulikua analindwa na walinzi wa Kike ?
 
Kama sheria za Mungu zinavunjwa namna hii vipi kuhusu sheria za binadamu ?
Ni lini mungu ameleta sheria hapa duniani??

Misikiti na makanisa ni nyumba kama nyumba zingine tu.( unaweza kugeuza kuwa ghala la kuwekea mahindi pia)
 
Back
Top Bottom