Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Nakusalimu tena kwa Jina la Jamhuri ya Muungano Tanzania Mama yangu!
Ni nadra sana Mimi Lord Denning kuandika nyuzi mbili humu ndani Ila leo imebidi nikuandikie humu maana nimegundua kuwa wewe ni mwanachama na mpenzi wa hili jukwaa! Nimeandika ushauri wangu kwako juu ya reformation ninayopendekeza Uifanye hasa kwenye ukusanyaji wa kodi (TRA) na sasa naandika hili kuhusu jambo ninaloliona linakuja hivi punde kuwa kama fursa kubwa ya kiuchumi kwa Tanzania.
Leo vyombo vya Habari vya kimataifa, vimetangaza kuhusu Kampuni kubwa ya ufaransa, Total , kusitisha shughuli zake msumbiji kutokana na sababu za kiusalama.
Kwanza kabisa napenda kukiri kuwa hali ya kiusalama msumbiji sio ya kufurahia hata kidogo, Nawapa polee ndugu zetu wale.
Kilichonilazimu kukuandikia humu huu ushauri ni fursa niliyoiona kuwa inakuja Tanzania kutokana na hali ya usalama kule msumbiji.
Ni ukweli usio na shaka kuwa Tanzania na Msumbiji ndo future ya Africa Kwa miaka mingi ijayo kutokana na hazina kubwa ya gesi. Uchumi wa gesi, pamoja na changamoto zote ni uchumi unaotegemewa sana na dunia kwa sababu gesi ni bidhaa adhimu kwa Tanzania, Hivyo kwa yanayoendelea Msumbiji hasa changamoto za kiusalama, ni dhahili kuwa makampuni makubwa ya mafuta, sasa yanaenda kuhamisha interest zao za uwekezaji kuja Tanzania.
kutokana na fursa Hii niliyoiona, napendekeza haya yafanyike kwa haraka ili Tanzania tuikamate hii fursa vizuri na kuitumia vizuri kiuchumi kwa faida ya Taifa letu.
1. Ingawa kiulinzi na kiusalama tuko vizuri na ushahidi wake ni kuwa wale wanaosumbua Msumbiji ni watu ambao vikosi vyetu vya ulinzi na Usalama vilifanikiwa kuwaondoa Tanzania napendekeza ili kuzidi kuimarisha confidence ya hawa wawekezaji kuja kuwekeza kwetu na kuimarisha uchumi na maendeleo ya Taifa letu, Boresha zaidi jeshi letu la wananchi (JWTZ) hasa kizana, kimafunzo na kiteknolojia ili liweze kujiimarisha kiulinzi na kukabiliana vizuri na tishio katika ukanda ule na kuleta confidence kwa hawa wawekezaji walete mitaji yao na pesa zao hapa nchini. Kwenye hili naomba boresha zaidi Navy Kwa kununua meli na boti kubwa za kivita huku ukiimarisha vikosi vingine kama jeshi la anga na la ardhini pia. Nimesema naamini majeshi yetu yako vizuri ila kwa mustakabali wa kukamata huu uchumi wa gesi kwa Africa hii, naomba viimarishe vikosi vyetu kwenye kila nyanja ili tuwe vizuri zaidi na kuondokana na matishio yote.
2. Naomba Kupitia timu zenu za mazungumzo ya mikataba mbalimbali, muweke nguvu kwenye kuweka sawa mikataba ya LNG na uwekezaji mwingine wa Gesi katika ukanda wa LINDI na Mtwara. Nina uhakika wawekezaji waliowekeza msumbiji watakuwa comfortable zaidi kuja kuwekeza Tanzania Kwa sababu haitawagharimu sana kuhamisha mitambo yao na teknolojia yao kutoka pwani ya msumbiji kuja Pwani ya Tanzania kutokana na ukaribu, Hivyo naomba kuanzia sasa serikali yako ianze lobbying kuyaita haya makampuni kuja mezani na kuzungumza kuhusu kuhamishia mitaji yao na uwekezaji wao Tanzania katika terms ambazo zitatufavor sisi na kutengeneza mapato makubwa kwa Taifa letu na ajira.
Naomba kuwasilisha!
SOMA PIA: Mashambulizi yapelekea Total kusitisha shughuli Msumbiji