Rais Samia, kuna Fursa ipo kwetu kwenye Uchumi wa Gesi, ichangamkie haraka

Rais Samia, kuna Fursa ipo kwetu kwenye Uchumi wa Gesi, ichangamkie haraka

Tena hao TOTAL, kabla ya kwenda Msumbiji walianzia hapa, vikwazo vikawa vingi mno kama kawaida yetu!!ndio maana juzi mama Samia alitoa maagizo huo mchakato wa LNG, inabidi serikali ifikie uamuzi liishe!!!na tatizo letu wanasiasa ndio huwa wanajifanya kuwa mbele zaidi kuliko wataalam, kutokana na wataalam wengi kutoaminika!!
Haya mambo ya vikwazo dhidi ya wawekezaji na uwekezaji ndo mambo ambayo mama hayataki. Naamini kwenye bajeti hii ya mwaka huu wizara za Fedha, Uwekezaji pamoja na ya Viwanda na Biashara , watakuja na Dira mpya ili kufanikisha Dira aliyotoa Mama kwenye haya
 
Nani kakwambia Kikwete alimuuzia mchina? Una ushahidi??
Wewe unadhani vitalu vya Gesi huko kusini bado havijauzwa? Kikwete alisaini mikataba na WACHINA under certificate of urgency siku za mwisho wa utawala wake. Hujui Mwendazake ndio maana akakasilika kuona walimaliza vitalu akaona na yeye aanzishe mradi wake wa Stiegler's !!
 
Mkuu mbona unasema mambo ya uongo aisee,una uhakika vitalu vyote vishauzwa?unafahamu kama serikali yenyewe kupitia TPDC wanavisima vyao pia?

Ushahidi ni kama vile vitalu bado vipo havijauzwa na umiliki wake ukawekwa wazi!! Lakini Mwendazake alikuwa na taarifa ya hali halisi ya huko kusini!!
Unakumbuka jinsi Pro. Muhongo wakati huo waziri wa Nishati alipowatukana wazawa walipoomba vitalu akawambia hawana ubavu wa kumiliki vitalu vya gesi ; na kuwa uwezo wao ni viwanda vya Juisi!!! FATHER OF ALL unaitwa huku ,busara zako zinahitajika.
 
Botswana na madini ya almasi.
Nitajie ni nchi gani Afrika ilishanufaika na ikapata maendeleo kwa sababu ina raslimali! Sana sana naona raslimali zinaleta janga la vita! Unajua Total wamewekeza nini Nigeria? Je wanaigeria unaona wananufaika sana?
 
Mkuu mbona unasema mambo ya uongo aisee,una uhakika vitalu vyote vishauzwa?unafahamu kama serikali yenyewe kupitia TPDC wanavisima vyao pia?

Kama vipo vimebaki nini kinazuia kuviendeleza? Mnangoja mpaka gesi inyonywe na Msumbiji? Kwanini Mwendazake developed cold feet kuendeleza gesi ya kusini ?
 
Huko kwenye gesi tulishapigwa kitambo...mikataba ya akina Sospatel (Sospeter) chini ya utawala wa JK walifanya la kutufanya! Acha tuendelee kununua ya Waarabu maana hakuna namna!
 
Nitajie ni nchi gani Afrika ilishanufaika na ikapata maendeleo kwa sababu ina raslimali! Sana sana naona raslimali zinaleta janga la vita! Unajua Total wamewekeza nini Nigeria? Je wanaigeria unaona wananufaika sana?
Nigeria wamenufaika gdp yao inapanda kwa kasi sasa hivi ni no 1 africa . Wamejenga miundombinu mingi na biashara nyingi zimekuwa ikiwemo dangote iliyowekeza miradi mbalimbali africa .

Tatizo Ina viongozi mafisadi
 
Mkuu mbona unasema mambo ya uongo aisee,una uhakika vitalu vyote vishauzwa?unafahamu kama serikali yenyewe kupitia TPDC wanavisima vyao pia?
Ndo mana hata Mie nimemahangaa sana!
 
Nigeria wamenufaika gdp yao inapanda kwa kasi sasa hivi ni no 1 africa . Wamejenga miundombinu mingi na biashara nyingi zimekuwa ikiwemo dangote iliyowekeza miradi mbalimbali africa .

Tatizo Ina viongozi mafisadi
Mifano ya waliofanikiwa ipo mingi sana. Kikubwa tunaweza tukajifunza kuanzia walipofanikiwa wao na tukafanikiwa zaidi. Mapungufu yao pia tunaweza kuyaepuka pia ili tufanikiwe zaidi.
 
Ushahidi ni kama vile vitalu bado vipo havijauzwa na umiliki wake ukawekwa wazi!! Lakini Mwendazake alikuwa na taarifa ya hali halisi ya huko kusini!!
Unakumbuka jinsi Pro. Muhongo wakati huo waziri wa Nishati alipowatukana wazawa walipoomba vitalu akawambia hawana ubavu wa kumiliki vitalu vya gesi ; na kuwa uwezo wao ni viwanda vya Juisi!!! FATHER OF ALL unaitwa huku ,busara zako zinahitajika.
Kwani wewe unaamini kuna mzawa anaweza kumiliki kitalu cha gesi na kufanya exploitation?
 
Kwanini washindwe, inahitaji mtaji kiasi gani kiasi mabilionea wa tz washindwe!?
Sijaweza kupata for now ila nakumbuka mjadala ulivyokuwaga Bungeni ambapo ilibidi Prof Muhongo atoe ufafanuzi kwa jinsi gani uwekezaji kwenye gesi ulivyo High risks kutokana na kuitaji hela nyingi sana ambazo unaweza ukawekeza na still bado ukakosa kiwango cha gesi kinachotakiwa kwa ajiri ya biashara.
Nikipata ile clip au ata hansard za bunge nitashare humu.

For now mwanateknolojia bagamoyo anaweza nisaidia kutafuta ile clip ambayo Sospeter Muhongo alikuwa akielezea Bungeni.
 
Ni mapema mno

Tusije tukaonekana hao WAHUNI tuliwa create sie ili tuvutie miradi kwetu maana inasemakana hao WAHUNI waliopo huko Delta Delgado ( if am not mistaken) ni madharia ya Kibiti.
 
Back
Top Bottom