Rais Samia: Kuna Mabalozi hawajui wanachokifanya, wapo tu

Rais Samia: Kuna Mabalozi hawajui wanachokifanya, wapo tu

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaapisha Mabalozi Wateule Ikulu Chamwino Dodoma leo August 16,2023 ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba ni kwamba kuna Mabalozi ni kama vile hawajui wanachokifanya kwakuwa wapowapo tu na hawafanyi kazi kwa ufanisi.

“Katika Nchi nyingine Mabalozi wetu sijui niseme hawajui wanachokifanya, wapo tu, nilishakutana na Rais mwenzangu ndani ya Nchi za Afrika, ndani ya SADC akaniambia nibadilishie Balozi uliyeniletea hata kazini haendi, mikutano hashiriki yupoyupo tu hatuelewi, Tanzania hatujawazoea hivyo sasa labda ubadilishe nikamwambia nimekusikia”

“Lakini Mabalozi wengine unawaona pale ambapo Ujumbe wa Tanzania umekwenda kwenye Nchi hiyo, au siku za kisherehe za Kitaifa za Nchi hiyo anakwenda kuwakilisha Nchi yake lakini mengine hakuna, au labda Watanzania wafanye ukorofi wakamatwe huko ndio utaona taarifa ya Balozi lakini vingine huoni”

“Sasa inawezekana pia labda na aina ya Mabalozi tunaowapeleka inawezekana, karibuni hivi nilitengeneza Kamati ipitie Wizara hii ya Mambo ya Nje iniletee kasoro zilizopo, nimepokea draft ya kwanza nimewarudishia wanaendelea kufanyia kazi nadhani ripoti itakapokuja itasaidia turekebishe Wizara yetu”

Chanzo: Millard Ayo
Mabalozi wa Tanzania huku nje, hawana tofauti na Ma-RPC waliorudishwa Makao Makuu.
Kingine, wao wenyewe wanaoteua ndiyo husababisha yote hayo.
Wanateua watu kuwa mabalozi kama adhabu, sometimes kumuweka mbali na siasa za ndani au kama mnamuona ni threat.
Sasa kwa mtu kama huyo unategemea akafanye nini?
Mabalozi ni watu ambao vichwa vyao vipo full charged.
 
Mm na familia yangu pamoja na ukoo wangu woooote tunasema na WW hatukuelewi elewi pia. Kuhusu bandari yetu.
Asante
 
Nilikwenda kwenye balozi moja nikawa nafanya kikao na balozi na wawekezaji. Honestly nilikuwa naona aibu.
Kuna haja ya kubadili mtazamo kwamba watu wa international relations mostly ndio wanakuwa balozi.
Tuangalie investment au business acumen. Mengine yasaidie hapo
 
Wengi wanachaguliwa bila kuwa na sifa na uzoefu wa Diplomasia........yaani mtu anachaguliwa hana exposure yoyote ya international relations,siku ya kwenda kazini ndiyo mara ya kwanza kusafiri nje ya nchi........tuache kuchaguana Kwa ukada,chagueni watu wenye weledi na Diplomasia
 
Back
Top Bottom