Yaani najiuliza hivi kweli tupeleke waliokaribu na kupumzika ndo wakweli active? Harafu tunajiuliza eti wapo wapo tu!Mnapeleka wazee waliostaafu, muda wa kupumzika nyie mnawapa kazi tena halafu mtegemee ufanisi kwenye kazi loooh!🥱
Akili ndogo sana hizi, kuchukulia kila kitu kwa mtazamo hasi.Faida zake ni zipi na zimeandikwa wapi ,mtu asiyejua kutumia hata Google unawezaje kumwamini kha
Nasikia wakisha teuliwa na Rais huwa wanapigwa msasa wa kidiplomasia kwa miezi mitatu pale chuo Cha Deplomasia Kurasini! Ngombe analazimishwa kunenepa siku ya mnada!![emoji1][emoji2][emoji1787]Wengi wanachaguliwa bila kuwa na sifa na uzoefu wa Diplomasia........yaani mtu anachaguliwa hana exposure yoyote ya international relations,siku ya kwenda kazini ndiyo mara ya kwanza kusafiri nje ya nchi........tuache kuchaguana Kwa ukada,chagueni watu wenye weledi na Diplomasia
Ok kuna nafasi Sudani, vp uko tayari kwenda tupeleke jina lako kwa Mama!!?Mojawapo ni yule Balozi aliyetenguliwa Brazil.
Rais Yuko sahihi wengine wanachakalika kutafuta soko nk ila wengine wapo wapo tuu.
Mh.Rais naomba Mimi hiyo Kazi kwenye Nchi yeyote kasoro Urusi nikufanyie kazi na nifanyie kazi Nchi yangu.
Hapana,sitaki kwenye vita sikuapa kuwa MwanajeshiOk kuna nafasi Sudani, vp uko tayari kwenda tupeleke jina lako kwa Mama!!?
Sasa analalama ni wakati ni yeye mwenyewe anawateua kishikajiRais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaapisha Mabalozi Wateule Ikulu Chamwino Dodoma leo August 16,2023 ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba ni kwamba kuna Mabalozi ni kama vile hawajui wanachokifanya kwakuwa wapowapo tu na hawafanyi kazi kwa ufanisi.
“Katika Nchi nyingine Mabalozi wetu sijui niseme hawajui wanachokifanya, wapo tu, nilishakutana na Rais mwenzangu ndani ya Nchi za Afrika, ndani ya SADC akaniambia nibadilishie Balozi uliyeniletea hata kazini haendi, mikutano hashiriki yupoyupo tu hatuelewi, Tanzania hatujawazoea hivyo sasa labda ubadilishe nikamwambia nimekusikia”
“Lakini Mabalozi wengine unawaona pale ambapo Ujumbe wa Tanzania umekwenda kwenye Nchi hiyo, au siku za kisherehe za Kitaifa za Nchi hiyo anakwenda kuwakilisha Nchi yake lakini mengine hakuna, au labda Watanzania wafanye ukorofi wakamatwe huko ndio utaona taarifa ya Balozi lakini vingine huoni”
“Sasa inawezekana pia labda na aina ya Mabalozi tunaowapeleka inawezekana, karibuni hivi nilitengeneza Kamati ipitie Wizara hii ya Mambo ya Nje iniletee kasoro zilizopo, nimepokea draft ya kwanza nimewarudishia wanaendelea kufanyia kazi nadhani ripoti itakapokuja itasaidia turekebishe Wizara yetu”
Chanzo: Millard Ayo
Hata wakuu wa wilaya wengi na mikoa hawajui kazi zaoRais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaapisha Mabalozi Wateule Ikulu Chamwino Dodoma leo August 16,2023 ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba ni kwamba kuna Mabalozi ni kama vile hawajui wanachokifanya kwakuwa wapowapo tu na hawafanyi kazi kwa ufanisi.
“Katika Nchi nyingine Mabalozi wetu sijui niseme hawajui wanachokifanya, wapo tu, nilishakutana na Rais mwenzangu ndani ya Nchi za Afrika, ndani ya SADC akaniambia nibadilishie Balozi uliyeniletea hata kazini haendi, mikutano hashiriki yupoyupo tu hatuelewi, Tanzania hatujawazoea hivyo sasa labda ubadilishe nikamwambia nimekusikia”
“Lakini Mabalozi wengine unawaona pale ambapo Ujumbe wa Tanzania umekwenda kwenye Nchi hiyo, au siku za kisherehe za Kitaifa za Nchi hiyo anakwenda kuwakilisha Nchi yake lakini mengine hakuna, au labda Watanzania wafanye ukorofi wakamatwe huko ndio utaona taarifa ya Balozi lakini vingine huoni”
“Sasa inawezekana pia labda na aina ya Mabalozi tunaowapeleka inawezekana, karibuni hivi nilitengeneza Kamati ipitie Wizara hii ya Mambo ya Nje iniletee kasoro zilizopo, nimepokea draft ya kwanza nimewarudishia wanaendelea kufanyia kazi nadhani ripoti itakapokuja itasaidia turekebishe Wizara yetu”
Chanzo: Millard Ayo
Mkuu haya mambo hajijengi siku moja wala hayaji yenyewe. Ngoja nikupe mfano. Unapotokea wizi wa kura na rais na baadhi ya wabunge wakapata nafasi kwa wizi wa kura vijana wanaona na kuelewa kilichofanyika. Unapotokea mkataba mbovu kama huu wa bandari na ukatetewa na viongozi kwa nguvu bila hoja vijana wanaona na kuelewa kinachoendelea. Sasa vijana wa aina hiyo hata wakipewa nafasi hawatawatii wale waliowateua kwa sababu wanajua tabia zao. Kwa kifupi mwizi au mzazi mwenye tabia mbaya mtoto wake atamdharau na hatamtii au atamwonyesha utii wa kinafiki. Hili ndilo linalotukuta. Huwezi kupata cream nzuri kwenye society kama yetu unless viongozi wetu waanze kubadilika wao.Ni kweli vijana wana matatizo lakini wakipewa mafunzo na kuwa wafauatiliwa kwa KPIs kama alivyosema mwenzetu hapo juu, tunaweza kupata ile cream nzuri kwa ajili ya kazi.
Hivyo ndivyo wenzetu wanavyofanya bila hivyo hakuna maendeleo yoyote yale khasa kwenye diplomasia ya kiuchumi.
Ndo maana ni lazima wizara ifanyiwe mabadiliko na ukipata waziri ambae ajitambua basi mabalozi wote watawajika uzuri tu.
Kwa hiyo ni Mkataba wa Bandari tu watu wasijadili mambo mengine? Hao Dp world wamekuchanganyeni kweli kweli inaonyesha hata munapolalla munawaotaMambo ya mabalozi kwa sasa sio ishu. mkataba wa Bandari ndio habari! Tanzania ya leo kuna "wahaini" duuuuuh!
Mbona tayari hizo zimeendaBandari zetu ni URITHI wetu, hazitauzwa, kubinafsishwa Wala kugawiwa Bure!!!
Kununua bandari zetu ni sawa na kununua UPUPU na kujipaka ukidhani ni PAWDER, hakutalalika!!!
Kataa wahuni!!!
Thubuutuu!!Mbona tayari hizo zimeenda
Hizo zako wewe zinaitwa ndoto za Ali NachaThubuutuu!!
Mwiba umekwaa kooni, kutapika ndo only choice!!
Ni matumizi mabaya ya Rasilimali cos kuna watu wengi wanaujuzi wao na wangeweza kutoa mchango chanya Kwa taifa, inasikitishaNasikia wakisha teuliwa na Rais huwa wanapigwa msasa wa kidiplomasia kwa miezi mitatu pale chuo Cha Deplomasia Kurasini! Ngombe analazimishwa kunenepa siku ya mnada!![emoji1][emoji2][emoji1787]
DP wameshatupiga tukubali tu, maana kuvunja Mkataba ni gharama sana afadhali zowezi liendelee huku tunagugumia maumivu ya kupigwa!!Thubuutuu!!
Mwiba umekwaa kooni, kutapika ndo only choice!!
Si Kweli, mapungufu ya contract hiyo ni makubwa mno, tukiwa na Nia ya dhati hata 100 hatutolipa tukivunja.DP wameshatupiga tukubali tu, maana kuvunja Mkataba ni gharama sana afadhali zowezi liendelee huku tunagugumia maumivu ya kupigwa!!
Tatizo Sheria za kimataifa ndiyo zinatumika na si Sheria zetu hapa Tz!!Si Kweli, mapungufu ya contract hiyo ni makubwa mno, tukiwa na Nia ya dhati hata 100 hatutolipa tukivunja.
Kwa Mfano unaelewa nini kiongozi wetu kusaini Kwa niaba ya Tz na DP world Dubei? Hapo Kuna mkataba?
Wapi, ni Rahisi tu, Bunge linabatilisha tu asimio lake kuomba mchakato uanze UPYA, biashara iishie hapo.Tatizo Sheria za kimataifa ndiyo zinatumika na si Sheria zetu hapa Tz!!