Rais Samia: Kuna Mabalozi hawajui wanachokifanya, wapo tu

Mojawapo ni yule Balozi aliyetenguliwa Brazil.

Rais Yuko sahihi wengine wanachakalika kutafuta soko nk ila wengine wapo wapo tuu.

Mh.Rais naomba Mimi hiyo Kazi kwenye Nchi yeyote kasoro Urusi nikufanyie kazi na nifanyie kazi Nchi yangu.
 
Wale mnaowahofia kisiasa ndo mnawapa ubalozi , hlf unategemea wawe na ufanis ? Wkt wanajuwa lolote wanalofanya halitaonekana maana tyr kwenu ubaloz ndo kifungo cha mnaowahofia
 
Kama hawapewi KPI za kuja kuwapima mwisho wa mwaka watafanyaje kazi?

Hao mabalozi wapewe malengo na kila mwisho wa mwaka wafanye Presentation hata kwa njia ya mtandao kuwasilisha walicho achieve

Rate ya Watanzania kwenda Nje ya Nchi kufanya uwekezaji na utafutaji imekuwa ndogo ukilinganisha na Wenzetu Wakenya ama Wanyarwanda.

Ukija kwenye kutoa Hati za Kusafiria (Passport) imekuwa ubabaishaji tupu
 
Mnapeleka wazee waliostaafu, muda wa kupumzika nyie mnawapa kazi tena alafu mtegemee ufanisi kwenye kazi loooh!🥱
Umeshawahi kuona mabalozi wa USA? Kimsingi ubalozi unataka watu wenye uzoefu na umri mkubwa na siyo vibaya. Tatizo liko kwenye utamaduni wetu. Tumezoea uvivu na uzembe. Nina uhakika hata wakipelekwa vijana kwenye balozi zote, hali itakuwa mbaya zaidi. BTW Samia naye ni mmoja ya watu ambao wapo wapo tu na hana tofauti yoyote na hao mabalozi.
 
Raisi aondoe mabalozi ambao wamekaa huko ughaibuni kimazoea.

Ateue mabalozi wapya, vijana na wenye ari mpya na hata tovuti zionyeshe wajishugulisha.

Lakini tusisahau suala la Bandari yetu.
Mtanzania hana cha umri wala mazoea. Mtanzania popote alipo ni mtu mvivu na mpenda shortcut. Samia mwenyewe anawasema mabalozi lakini hata yeye hana tofauti nao. Hili la ''ujana'' nalipinga kwa nguvu zote kwa sababu vijana wametokea kuwa kundi lenye tamaa na wazembe kupindukia. Kama unabisha angalia hao waliopo kwenye siasa au mashirika ya umma.
 
Mnapeleka wazee waliostaafu, muda wa kupumzika nyie mnawapa kazi tena halafu mtegemee ufanisi kwenye kazi loooh!🥱
Kama sirro nasikia aligoma kabisa akataka apumzike wakamlazimisha. Halafu unazungumzia ufanisi wakati we mwenyewe huwaweki kwa ajili ya ufanisi. Kufeli kwao wa kulaumiwa ni wewe uliyewaweka.
 
Aibu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…