Rais Samia: Kuna Mabalozi hawajui wanachokifanya, wapo tu

Yeye mwenyewe hajui anachokifanya ndo maana mpaka sasa hajui kwa nini nchi yetu ni masikini licha ya kuwa na kila rasilimali inayohitajika. Ni aibu rais anauliza wenzetu wanatumia uchawi gani kuendelea na bado yuko ofisini anakula na kutapanya kodi zetu.
 
Anataka wafanye nini tena ,
 
Bandari zetu ni URITHI wetu, hazitauzwa, kubinafsishwa Wala kugawiwa Bure!!!

Kununua bandari zetu ni sawa na kununua UPUPU na kujipaka ukidhani ni PAWDER, hakutalalika!!!

Kataa wahuni!!!
 
Ni kweli vijana wana matatizo lakini wakipewa mafunzo na kuwa wafauatiliwa kwa KPIs kama alivyosema mwenzetu hapo juu, tunaweza kupata ile cream nzuri kwa ajili ya kazi.

Hivyo ndivyo wenzetu wanavyofanya bila hivyo hakuna maendeleo yoyote yale khasa kwenye diplomasia ya kiuchumi.

Ndo maana ni lazima wizara ifanyiwe mabadiliko na ukipata waziri ambae ajitambua basi mabalozi wote watawajika uzuri tu.
 
Kauli ya kishujaa ya Rais mwenye maono,majitu yamekaa Kaa kama mizigo huko Nje.

Rais amesema Serikali Haina rasilimali za kulisha watu mizigo
 
Na kuna Marais hawajui cha kufanya wapo tu
 
Halafu anaishia kulalamika kama sisi.. c amtimue bc km ana jeuri hiyo!!!!!
 
Sas A mabalozi siyo career diplmats, ni wanajeshi wastaafu, polisi wastaafu, wakuu wa mikoa wastaafu,makada wa chama, wanasiasa wachovu na watu kama hao.
Tunategemea nini?

Malalamiko mengi wale Career Diplomats katika Foreign wanalalamika sana kurukwa kuiwakilisha nchi huko nje.
 
Swala la kuwa mwanajeshi si shida. Kwa taarifa yako mabalozi wengi wa nchi zilizoendelea mfano Marekani uwa ni wanajeshi wastaafu. Tusidhani hatuna wanajeshi wataalamu. Jeshi limekamilika na linawataalamu hadi wa masuala ya diplomasia.

Shida kubwa kwa Tanzania, ubalozi imekuwa sehemu ya kumficha mtu. Ni kama adhabu fulani mtu kapewa ili asijijenge hapa Tanzania.

Au mtu kaharibu sasa katika kulindana inabidi apewe ubalozi. Na wengine upewa ubalozi kama kujuana na si uchapa kazi wa mtu. Unategemea umempa mtu ubalozi ili umpeleka mbali asisikike huko aliko atakuwa na mwoyo wa kufanya kazi kweli? Yaani sana sana atakuwa anakula bata tu.

Mama anaongea na kulalamika, sidhani kiongozi wa nchi unatakiwa kulalamika. Yeye ahakikishe anateuwa watu wenye ari ya kufanya kazi, na si vinginevyo.

Huko balozini wamejazwa watu ambao wanatakiwa kumsaidia balozi na kumshauri lkn wengi wao hawajui chochote. Kazi ni kutafuta mademu. Kuna siku nimeona aibu sana. Katika ubalozi wa Tanzania jamaa anaishi hapo hapo ndani. kazi yake gari zinakuja na mademu zinasimama getini anaondoka nao. Yeye anadhani atamuoni. Ni aibu tu.

Wengine wapo kazi umbea tu hakuna la maana huko balozini. Hata habri za nchi wanamoishi hawazijui vizuri kiundani. Intelijensia ni mbovu. Mfano ktk hiyo nchi niliona kuna fursa nyingi Tanzania kufanya biashara. Lakini wao hizo fursa wala hawaoni. Sana sana niliona Kenya balozi wao kajitahidi ktk diplomasia ya uchumi. Wetu wanabaki kula hela hawana msaada wowote hata kwa watanzania wengi waishio huko nje.
 
Mnapeleka wazee waliostaafu, muda wa kupumzika nyie mnawapa kazi tena halafu mtegemee ufanisi kwenye kazi loooh!🥱
Hii ndio shida kubwa ya Serikali yetu! inawaamini zaidi wazee kuliko vijana, Ktk Historia Mwl Nyerere aliwahi kumteua Salim kuwa Balozi akiwa na umri wa miaka 21 tu.
 
Raisi aondoe mabalozi ambao wamekaa huko ughaibuni kimazoea.

Ateue mabalozi wapya, vijana na wenye ari mpya na hata tovuti zionyeshe wajishugulisha.

Lakini tusisahau suala la Bandari yetu.
Tupo stand by tunasubiria Teuzi, ipo Siku nitapata nafasi ya kulisaidia Taifa langu na kumsaidia Rais wangu na kuwasaidia Watanzania wenzangu! MUNGU nisaidie.
 
Anipeleke Urusi nikabonge na Медведев na Путин [emoji123]
 


Duuuh aiseeee inasikitisha sana....Unakuwaje Balozi wa nchi halafu unakosa cha kufanya? Hivi hawana JDs? Mbona kazi nyingi sana kama balozi? Wamuige Mzee wa Cuba pole Pole naona anapambana sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…