Rais Samia: Kuna vijineno Serikalini hakuna hela, ni kweli…

Baadhi ya Miradi ndio itachelewa sio Kukosa salary,hii hauwezi kutokea.

Mwisho tabu hizi anazitaka Rais mwenyewe kwa kuzalisha mashaka mengi kwa sababu sio kila ukweli Ni wa kuusema wazi, mwingine unakanusha hata Kama Ni ukweli ili.ku buy time
 
Mikopo ni mizuri ila usizidishe ukopaji, itafika mahali tutaongezewa nguvu kubwq ya urudishaji na atakae umia zaidini mwananchi maana ataongezea kodi umiza,huwa namshfangaa waziri kusema hakuna mtu atalipa deni ni nani mlipa deni kama sio sisi walipa kodi
 
Hafiki kokote nakwambia Mungu atusaidie muda utaongea mtakumbuka kauli ya Kikwete ya labda mambo yaharibike sanaaa mbele ya safari.

Wanafanya kitu inaitwa Wealth Accumulation kila mmoja anajilia kivyake, siku moja tutaongozaa na Jeshi letu tukufu let's wait.
 
Nchi haiendeshwi kwa mikopo ya kufanya sinking of money, ni uhuni kweli
 
Biased analysis/comment based on your religious belief.

Mlisahau kuwa Marehemu Mwendazake alikopa mikopo ya kibiashara toka mabenki ya kimataifa ya biashara unayo-mature haraka na yenye riba kubwa kisha akasingizia kuwa tunajenga miradi kwa fedha zetu za ndani? Tena wale wahuni/mabepari walimfuata huku huku kumkopesha! Eti' alikuwa anapambana vita vya kiuchumi ilihali hajui nini maana ya uchumi.
Ndio hiyo sasa anayohangaika kuilipa Rais Samia

Kosa alilofanya Kikwete ni kumlinda na mwisho maamuzi yake yanaigharimu taifa kuanzia kulipa fidia kwenye kesi zilizosababishwa na maamuzi yake. Rejea meli ya wachina,kuvunja mikataba ya barabara,kuchukua ardhi bagamoyo,kivuko Cha bagamoyo,kuuza nyumba za serikali n.k
 
Tatizo hao viongozi hawana right idea kuhusu uchumi na maendelo kwenye hizi nchi zetu kiasi kwamba wanafikiri kufanya mega-projects kwa pupa ndo maendeleo kumbe wanaishia kuingiza nchi kwenye madeni.....uchumi ambao hauko centered kwenye hali ya maisha ya watu wengi huo ni uchumi fake. Distribution of wealth kwenye hii nchi imekuwa mtihani kiasi kwamba asilimia kubwa ya wananchi wanashindwa kumudu maisha ya kawaida kabisa huku viongozi wakikanyagana kulamba asali na kujipimia kwa urefu wa kamba.​
 
Jeshi likikuongoza ndio halifanyi ufisadi?

Jeshi ndio litakuletea Maendeleo?

Kwani hata Sasa Pesa za miradi ya jeshi huwa unakagua wewe?

Umewahi kumuona Mwanajeshi wa Ngazi ya Juu Ni maskini?

Jeshi likishika ndio itakuwa mwisho kuhoji huwezi na huna Cha kuwafanya.

Kaulize Sudan, Egypt,Mali,Bukinafaso nk nk
 
Duh!, amethibitisha serikali yetu inaendeshwa kwa mikopo, huku chawa wakiendelea kupiga makofi kwa nguvu, hili taifa la ajabu sana.

Kumbe ndio maana Ndugai yalimkuta, kwsababu kama kile alichoshauri kingefanyika basi serikali yetu inge collapse, ikalazimu aondoshwe kwa misuto!

Hivi zile tozo za kila siku huwa zinakwenda wapi? Mwigulu anatakiwa kuwajibishwa, Waziri wa Mipango asiye na mipango yoyote, ila kwa uzembe wa Samia wacha atambe tu.
 
Hivi unajua Budget ya mishahara ya serikal kwa mwezi ? Au Unasikia Radio mbao tu kuna Tajiri hapa Tz anauwezo kulipa mishahara ya serikali watanzania walio wengi ni wajinga hasa lugha rahisi ni jamii ya hovyo kabisa katika ukanda huu wa mashariki
 
View attachment 2454456

Kuna wakati nikasikia serikali mifumo ya fedha haifanyi kazi imefungwa. Kumbe ilikuwa kweli. Kwa waziri yule Mwingulu Nchemba usishangae Tanzania ikawa kama Ghana au Zambia
ni kweli kabsa Elimu bure mpaka leo fedha ya mwezi wa 11 haijatoka, kawaida huwa inatoka kati ya tarehe 2 mpaka 5 leo ni tarehe 22
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…