Pre GE2025 Rais Samia: Kuna watu wanapita huku na huko na kusema Serikali hii inafuja fedha Kwa kununua Magari ya kifahari badala ya Matrekta!

Pre GE2025 Rais Samia: Kuna watu wanapita huku na huko na kusema Serikali hii inafuja fedha Kwa kununua Magari ya kifahari badala ya Matrekta!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hahaha Magari yana leta Tija gani huko Serikalini? Zaidi ya Watawala kula raha sioni kazi na wajibu wa magari serikalini.
 
Hotuba hazimfanyi rais akaonekana anatosha kuwa ikulu. Wapo wenye uwezo wa kuweka data majukwaani lakini hawana uwezo wa kufufua mahusiano ya kimataifa kati ya TZ na nchi zilizoendelea,
Unaweza kufufua mahusiano lakini huwezi kijenga uchumi Imara Kwa rasilimali zako...we una kuza mahusiano Kwa ajili ya kutembeza bakuli ili kuomba fedha.
 
Umaridadi huficha umasikini...Tatizo la nchi Yetu ilikua miundombinu mibovu, Magu aka sortout...nunua tu mama, trekta haifai kwa bata, na mjini hakuna mashamba!
 
Rais Samia amesema kuna watu wanapita huku na huko na kusema serikali hii inafuja fedha Kwa kununua Magari ya kifahari badala ya Matrekta kumbe hawajui serikali ina mipango yake

Rais Samia amesema hawazuki Tu na kuanza kununua Magari bali ni mipango iliyopangwa vizuri sana mapema

Source: EATV

Pia, soma: Je, Msafara wa Rais wenye Magari 118 ni Uwajibikaji?
Hatujasema serikali inunue matrekta, bali serikali itumie pesa kwa makini kwa kuachana na matumizi yasiyokuwa ya lazima ili kupunguza mikopo. Ni aibu kwa serikali kuwanunulia maofisa wake magari ya kifahari kwa hela ya kukopa, ambapo maofisa wa serikali zinazotukopesha hawatumiii magari kama hayo.

Najua kuna watakaotetea kuwa siyo hela za kukopa lakini bado swali liko pale pale kuwa kama tuna hela zetu tunazotumia hovyo namna hiyo, kwa nini tukakope hela za miradi mingine badala ya kutumia zetu hizo?
 
Vitu vingine ni kunyamaza siyo lazima aongee kujidhalilisha hivi Huwa mpango wa kununua magari ya kifahari nao ni wa kujivunia?
 
Mama kwa hili UMETELEZA..tunachosema ni kwamba, kutokana na hali yetu ya kiuchumi ni TIA MCHUZI PANGU PAKAVU, basi hata ununuzi wa magari uangalie hili..
Tunaweza nunua Landlover za kawaida, Toyata Prado za kawaida, hata Van guard or RAV 4 zinatosha sana, uzuri kwa sasa tuna barabara za lami sehemu kubwa ya nchi, bila kusahau barabara nyingi za changarawe chini ya TARURA, mwisho tuna train ya kisasa ya SGR
 
Rais Samia amesema kuna watu wanapita huku na huko na kusema serikali hii inafuja fedha Kwa kununua Magari ya kifahari badala ya Matrekta kumbe hawajui serikali ina mipango yake

Rais Samia amesema hawazuki Tu na kuanza kununua Magari bali ni mipango iliyopangwa vizuri sana mapema

Source: EATV

Pia, soma: Je, Msafara wa Rais wenye Magari 118 ni Uwajibikaji?
Mama kwani ni uongo ungewanunulia, hata Klugger tu m bona inafika huko kwenye miradi? Just 25m kuliko hizo gari 300m tunahumia, sana. Aidha tunakuongezea, ubuyu kuwa Mwigulu ameiba sana, pesa za, serikali na kuanzisha, timu na, kununua, mabasi mengi yanaitwa, Easter. Mama tafadhali sisi tunasema ukweli tupu. Pesa inaibiwa, nyingi sana.
 
Unaweza kufufua mahusiano lakini huwezi kijenga uchumi Imara Kwa rasilimali zako...we una kuza mahusiano Kwa ajili ya kutembeza bakuli ili kuomba fedha.
Kufufua mahusiano ni hatua ya kwanza, unafuatia mjadala wa namna za ushirikiano za kutengeneza uchumi mzuri.

Huwezi kumkwepa mgeni hata siku moja, akili mbili tofauti zinapounganika zinafanya kitu cha maana.

SSH anaweza kuondoka akifanya makubwa kuliko watangulizi wotano walioongoza nchi kabla yake.
 
Vijana kama wee huwa tunawaombea dua tu, kiza kiwatoke, nuru ya Uislam iwaingie. Huwa mnakuwa Waislam wazuri sana.
Natamani sana kuwa Muislamu, sijajua taratibu za kufuata tu. Kwa sasa naishi kwa imani zangu za jadi tu.
 
Natamani sana kuwa Muislamu, sijajua taratibu za kufuata tu. Kwa sasa naishi kwa imani zangu za jadi tu.
Hakuna taratibu ya kufata, ni kushahadia tu mbele ya mashahidi japo wawili.

Kazi ya nusu dakika. Ingia msikiti au madrasa yoyote ya karibu yako. Utasilimu ndani ya nusu dakika.
 
Hili swala la Matumizi limekua tatizo kubwa hasa kwenye uongozi wa Africa.

Kuna vitu vya muhimu lakini havipewi kipaumbele. Na hii imetokana viongozi kujibatiza jina la Uheshimiwa Na kulikataa jina la Ndugu.

Unapo jiita MH maana Yake unajitengenezea kadunia kako pekeyako Na kujitenga Na watu kwa levo ya Ukwasi Na fahari.

Mimi ni likuwepo Awamu ya kwanza mpaka hii ya mama.

Katika Awamu ya kwanza ilijikita sana kupeleka maendeleo kwa wananchi. Utawala ule ulijinyima mambo ya kifahari ili kuwapelekea wananchi wake maendeleo.

Nimalizie kwa kusema. Wananchi kwanza serikali inaweza kupunguza Matumizi ya gharama Na fedha zikaokolewa nyingi zikaelekezwa kwenye vitu muhimu vya wananchi.
 
Rais Samia amesema kuna watu wanapita huku na huko na kusema serikali hii inafuja fedha Kwa kununua Magari ya kifahari badala ya Matrekta kumbe hawajui serikali ina mipango yake

Rais Samia amesema hawazuki Tu na kuanza kununua Magari bali ni mipango iliyopangwa vizuri sana mapema

Source: EATV

Pia, soma: Je, Msafara wa Rais wenye Magari 118 ni Uwajibikaji?

Sometimes Maza akiwa anaongea unagundua kuwa ule Ukatibu Masijala bado haujamtoka.
 
Back
Top Bottom