Pre GE2025 Rais Samia: Kuna watu wanapita huku na huko na kusema Serikali hii inafuja fedha Kwa kununua Magari ya kifahari badala ya Matrekta!

Pre GE2025 Rais Samia: Kuna watu wanapita huku na huko na kusema Serikali hii inafuja fedha Kwa kununua Magari ya kifahari badala ya Matrekta!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Attachments

  • images (28).jpeg
    images (28).jpeg
    47.6 KB · Views: 3
Boko za Mama;
Katiba ya Jamhuri (Kijitabu)
Utekaji watu (Drama)
Ulipaji fidia (mpaka serikali imalize ujenzi wa mradi)
..........
 
Weweeeh hawezi kumfikia Chuma ambae aliweza kudhibiti mpaka mishahara hewa...Alikamata Mali za Uma na kukemea waziwazi wahusika alijua kufariji watanzania kwemye janga La Korona.
Hakika hakuna kipindi watu wanazipiga pesa kama asaivi...mpaka wanamiliki Timu za Mpira.
Kufufua mahusiano ni hatua ya kwanza, unafuatia mjadala wa namna za ushirikiano za kutengeneza uchumi mzuri.

Huwezi kumkwepa mgeni hata siku moja, akili mbili tofauti zinapounganika zinafanya kitu cha maana.

SSH anaweza kuondoka akifanya makubwa kuliko watangulizi wotano walioongoza nchi kabla yake.
 
Ni LAZIMA yawe V8? 110 Defender ama Landcluser hard top haziwezi kuwafikia wananchi & wakulima vijijini.
 
Weweeeh hawezi kumfikia Chuma ambae aliweza kudhibiti mpaka mishahara hewa...Alikamata Mali za Uma na kukemea waziwazi wahusika alijua kufariji watanzania kwemye janga La Korona.
Hakika hakuna kipindi watu wanazipiga pesa kama asaivi...mpaka wanamiliki Timu za Mpira.
Kupiga pesa hata wakati ule kina Makonda na Sabaya walizipiga sana japo habari hazikuwekwa wazi.

Samia anaamini katika kuwapa watu uhuru wa kuongea na kujieleza. JPM alipenda mno kusifiwa na siku zote unapotoa uhuru wa habari unaopitiliza idadi ya wale wanaokusifia humezwa na wale wenye kutoa maoni huru ambayo yatakosoa mengi unayoyafanya.

JPM aliwahi kusema mahali fulani kuwa angetamani sana aweze kudhibiti kinachosemwa kwenye vyombo vya habari, hakuwa mwanademokrasia.

SSH ni kinyume chake ndio maana anaonekana hakuna analofanya, ukweli ni kwamba anapiga kazi sana na watanzania wanapenda kuongelea yale mabaya tu.
 
Back
Top Bottom