Rais Samia kupokea Gawio na Michango kutoka Mashirika na Taasisi za Umma, Matukio kurushwa live kupitia vyombo vyote vya habari

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan,mama wa shoka , shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge.

Hii leo muda na Majira ya saa tano asubuhi atafanya tukio zito sana lenye maslahi mapana kwa Taifa letu na lenye kuonyesha hali nzuri na yenye Matumaini na ustawi mzuri wa uchumi wetu.

Ni tukio la kupokea Gawio na michango kutoka mashirika na taasisi mbalimbali za umma. Ambapo zitatoa kwa serikali Gawio na michango kutokana na faida iliyopatikana.,inayotokana na mazingira wezeshi na mazuri yaliyowekwa na kuboreshwa na serikali ya Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia. Ni Gawio na Michango halali na siyo Gawio la kulazimishwa au kupika Takwimu.

Ni Gawio na michango inayoonesha na kutoa picha na taswira ya kuongezeka kwa ufanisi katika uendeshaji wa taasisi na mashirika ya umma, hasa baada ya maelekezo Mazito Sanaa ya Mheshimiwa Rais yakutaka kuongezwa ufanisi na ubunifu kwa mashirika na taasisi zote za umma. Ni gawio na Michango inayoonyesha muelekeo mzuri wa kuondoa hasara kwa mashirika na taasisi za umma.lakini pia kuonyesha kuanza kuwa mashirika yenye faida na tija badala ya kuwa mashirika Mzigo ,tegemezi na kupe kwa serikali na kodi za watanzania.

Tutarajie hotuba nzito sana kutoka kwa Amiri Jeshi mkuu Daktari Samia Suluhu Hasssan,yenye kutoa muongoza na Dira pamoja na maelekezo kwa Masuala mbalimbali Mtambuka. Tukio hilo litakuwa live kupitia vyombo vyote vya habari hapa Nchini pamoja na mitandao yote ya kijamii.usipange kukosa wala usisubiri kuhadithiwa maana utakuwa umekosa mambo mengi sana na utajuta sana maishani mwako. Andika historia yako mwenyewe kwa kufuatilia tukio la leo.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mams ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Yanakopa ili yatoe kawio! Hamna kitu
Hakuna kitu kama hicho. Naona mmeanza kuweweseka baada ya kunusa mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia taasisi na mashirika mbalimbali ya umma ,baada ya kuanza kutekeleza kwa ufanisi na ubunifu maelekezo Mazito yaliyokuwa yametolewa na Mheshimiwa Rais wetu mpendwa
 
Waambie ukweli Hawa machawa pro max!
Wivu utawaua mwaka huu kwa mioyo yenu ya kishetani ya kutaka kusubiri na kusikia habari mbaya tu kwa Taifa letu. Mama Anaendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya watanzania kwa mafanikio makubwa yanayoendelea kupatikana katika kila Secta.
 
Tuliambiwa wakati wa Magufuli kuwa Mashirika yalikuwa hayaingizi faida bali hasara na Wakurugenzi walikuwa wanakopa pesa Benki ili wakatoe gawio kwa serikali.Sasa yeye Samia kafanya miujiza gani mpaka Mashirika yamepata faida wakati Management mentality ya Watumishi ni ile ile!!!
Ata Samia wakati nilimsikia akisema Mashirika yalikopa pesa!
 
Chini ya uongozi shupavu, imara na madhubuti wa Rais Samia na maelekezo yake mazito kwa Mashirika na taasisi za umma,kumekuwa na kuongezeka kwa ufanisi pamoja na ubunifu katika uendeshaji wa taasisi na mashirika mbalimbali ya umma.hali iliyoleta tija na kuleta faida baada ya kuondokana na kuziba mianya iliyokuwa ikileta hasara kwa mashirika na taasisi hizo.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan,mama wa shoka , shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge.

Hii leo muda na Majira ya saa tano asubuhi atafanya tukio zito sana lenye maslahi mapana kwa Taifa letu na lenye kuonyesha hali nzuri na yenye Matumaini na ustawi mzuri wa uchumi wetu.

Ni tukio la kupokea Gawio na michango kutoka mashirika na taasisi mbalimbali za umma. Ambapo zitatoa kwa serikali Gawio na michango kutokana na faida iliyopatikana.,inayotokana na mazingira wezeshi na mazuri yaliyowekwa na kuboreshwa na serikali ya Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia. Ni Gawio na Michango halali na siyo Gawio la kulazimishwa au kupika Takwimu.

Ni Gawio na michango inayoonesha na kutoa picha na taswira ya kuongezeka kwa ufanisi katika uendeshaji wa taasisi na mashirika ya umma, hasa baada ya maelekezo Mazito Sanaa ya Mheshimiwa Rais yakutaka kuongezwa ufanisi na ubunifu kwa mashirika na taasisi zote za umma. Ni gawio na Michango inayoonyesha muelekeo mzuri wa kuondoa hasara kwa mashirika na taasisi za umma.lakini pia kuonyesha kuanza kuwa mashirika yenye faida na tija badala ya kuwa mashirika Mzigo ,tegemezi na kupe kwa serikali na kodi za watanzania.

Tutarajie hotuba nzito sana kutoka kwa Amiri Jeshi mkuu Daktari Samia Suluhu Hasssan,yenye kutoa muongoza na Dira pamoja na maelekezo kwa Masuala mbalimbali Mtambuka. Tukio hilo litakuwa live kupitia vyombo vyote vya habari hapa Nchini pamoja na mitandao yote ya kijamii.usipange kukosa wala usisubiri kuhadithiwa maana utakuwa umekosa mambo mengi sana na utajuta sana maishani mwako. Andika historia yako mwenyewe kwa kufuatilia tukio la leo.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mams ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Namba ya simu siku hizi umeisahau. Au walishaisevu kwenye simu zao?
 
Chini ya uongozi shupavu, imara na madhubuti wa Rais Samia na maelekezo yake mazito kwa Mashirika na taasisi za umma,kumekuwa na kuongezeka kwa ufanisi pamoja na ubunifu katika uendeshaji wa taasisi na mashirika mbalimbali ya umma.hali iliyoleta tija na kuleta faida baada ya kuondokana na kuziba mianya iliyokuwa ikileta hasara kwa mashirika na taasisi hizo.
Vipi ATCL itakuwepo kutoa gawio?
 
Back
Top Bottom