Rais Samia kusaini EPA huko Brussels?

Rais Samia kusaini EPA huko Brussels?

Status
Not open for further replies.
Hivi vitu vyengine kabla hawaja sign wawe wanatuelimisha kwanza sasa mtu nasikia tu EPA!,faida yake sijui,hasara pia sijui..! Haya vipi kama ni mpango mkakati wa siri ndani yake..?
Tunaambiwa tu nchi inafunguliwa,aisee kunakufunguliwa na kuliwa..😂
🤣🤣🤣kweli
 
Pia kuna mpaka fishing hapo, usisahahu EU kuna overfishing na wameshamaliza samaki wao wote sasa wanakuja kuvua kwenye bahari yetu tax free!
Kwahiyo hako kafaida kadogo tunakokapata kwa kuexport minofu ya samaki ndio wametupora kupitia huo mkataba na ndio Rais kaenda kuusaini??

Duuh, sasa washauri wake wanamshauri nini kama jambo kama hili wanamshauri kulifanya??
 
Pia kuna mpaka fishing hapo, usisahahu EU kuna overfishing na wameshamaliza samaki wao wote sasa wanakuja kuvua kwenye bahari yetu tax free!
Ni kweli. Pia sisi tulikuwa tuna tatizo la kuwa SADC na EAC. Tukiwa SADC, Ulaya hawakutaka kututofautisha na kiwango cha ukuaji wa uchumi wa South Africa na tukiwa EAC hawakututofautisha na Kenya wakati nchi hizi zilikuwa na faida kwenye soko la Ulaya kuliko sisi! Kwa hakika mikataba hii ina maslahi makubwa upande wa Ulaya kuliko nchi zetu. Basi tu watu wameacha kutumia akili na uzoefu nchini.
 
Duuh kama ni kweli hiki nilichokisoma basi huu mkataba hauna faida kwetu maana sisi hatutaweza kushindana na ubora wa bidhaa zao kifupi ni kwamba mkataba huu unaipa faida sana European Union.

Makubaliano ni kwamba parties states zitaruhusu bidhaa kutoka katika nchi husika kuingia na kutoka bila kodi kwa baadhi ya bidhaa na kwa baadhi ya bidhaa punguzo ya kodi kwa asilimia 10-60.
 
Kwanza umekurupuka. Unaongea uvumi, pili unatakiwa kuweka mkataba hapa na sio kuongea kishabiki. Hatuwezi kuchangia uzushi na bila vielelezo. Kama ni mawazo yako binafsi sema kwamba unaongea bila kujua mkataba ukoje.
Ingekuwa vyema wewe ndio uulete huo mkataba ili ukosoe vyema. Otherwise hizi ni pumba tu.
 
Hivi vitu vyengine kabla hawaja sign wawe wanatuelimisha kwanza sasa mtu nasikia tu EPA!,faida yake sijui,hasara pia sijui..! Haya vipi kama ni mpango mkakati wa siri ndani yake..?
Tunaambiwa tu nchi inafunguliwa,aisee kunakufunguliwa na kuliwa..😂

Ni kweli inatakiwa viongozi wa,serikali ya Tanzania kabla hata hawajafika kwenye mkutano watoe taarifa kwa kina wanaenda kufanya nini na nini, pia wakiwasili nyumbani waitishe kikao airport kutueleza wamefanikiwa nini katika safari yao ya kikazi kwa niaba yetu raia milioni 60 wa Jamhuri ya Muungano.

Kutoka maktaba hili suala la EPA:

11 February 2020

Ile Trade Agreement EPA iliyokuwa inapingwa kwa kila hali na CCM sasa kusainiwa na Raisi wa Tanzania Samia huko Brussels kwenye EU- Afrika Union summit.

EPA ni free trade Agreement Kati ya EU na Nchi za Afrika Mashariki zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda.

Tanzania walipinga EPA kwa maana hawakuona manufaa yoyote kwa nchi yetu kwani hatuna cha kuuza EU wakati EU wana kila kitu cha kuuza kwetu.

Je, Viwanda vyetu juice ya Azam na umeme wa mgao vita compete na EU products? Kama hapo Kenya tu au Uganda ni ngumu kushindana tutaweza EU ?

Ikumbukwe sukari kutoka Brazili ni cheaper kuliko ya Tanzania sasa EU products tax free Tanzania, tutaweza?

Tunategemea kuuza nini EU ? Vipi natural resources zetu ?

Kweli ni Vita ya Kiuchumi RIP Magu …
Ni wakati sasa wa serikali kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji ili wazalishaji wa ndani watoe products zinazoweza ku compete na hizo za kutoka ulaya. Ishu za umeme, na bei za pembejeo za uzalishaji hasa upande wa kilimo zinatakiwa kuangaliwa kwa umakini.
 
Kwanza umekurupuka. Unaongea uvumi, pili unatakiwa kuweka mkataba hapa na sio kuongea kishabiki. Hatuwezi kuchangia uzushi na bila vielelezo. Kama ni mawazo yako binafsi sema kwamba unaongea bila kujua mkataba ukoje.
Mkuu na hilo ndio tatizo,hatujui kuna nini ndani ya mkataba.
Kwanini Uganda,Kenya, Rwanda na Burundi walitia sahihi mapema kwani mazingira ya biashara ni tofauti sana na yetu?
Nachojua Tanzania inauza Ulaya minofu ya samaki kutoka Ziwa Victoria kwa kipindi kirefu sasa.Lakini bado ina mazao mengine ya kilimo kama kahawa, Chai,mkonge,sukari,korosho,mhogo,mbao,ngozi, maua,parachichi n.k
Lakini bado kuna bidhaa za madini na vito kama dhahabu,Almasi,Tanzanite n.k
Ukiongezea na bidhaa za Nishati kama Mafuta na gesi asilia hatuwezi kusema hatuna kitu cha kuwauzia.
 
Ile Trade Agreement EPA iliyokuwa inapingwa kwa kila hali na CCM sasa kusainiwa na Raisi wa Tanzania Samia huko Brussels kwenye EU- Afrika Union summit.

EPA ni free trade Agreement Kati ya EU na Nchi za Afrika Mashariki zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda.

Tanzania walipinga EPA kwa maana hawakuona manufaa yoyote kwa nchi yetu kwani hatuna cha kuuza EU wakati EU wana kila kitu cha kuuza kwetu.

Je, Viwanda vyetu juice ya Azam na umeme wa mgao vita compete na EU products? Kama hapo Kenya tu au Uganda ni ngumu kushindana tutaweza EU ?

Ikumbukwe sukari kutoka Brazili ni cheaper kuliko ya Tanzania sasa EU products tax free Tanzania, tutaweza?

Tunategemea kuuza nini EU ? Vipi natural resources zetu ?

Kweli ni Vita ya Kiuchumi RIP Magu …
Kumbe huyu mama ana VISION,
WaTanzania siyo kwamba Europe watauza tu kwetu , vile vile watatumia fursa hii kufanya investment, joint ventuures to process goods from our cottons, fruits, agro products, petrochemicals, metals etc ambavyo vita uzwa kama export kwenda kokote duniani, this is among the biggest achievements kwa huyu mama, kaona mbali!!
 
Kanda Ya Ziwa Kwasasa Cement inatoka Kenya tayari Viwanda Vyetu vya cement vinaipata fresh ikiwemo wafanya biashara wa cement...Kenya Cement iko chini kwasababu ya Ukaribu wa Nairobi kuja Mwanza....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom