Rais Samia kushuhudia utiaji wa saini wa Mkataba SGR

Rais Samia kushuhudia utiaji wa saini wa Mkataba SGR

Elitwege

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
5,294
Reaction score
10,970
Mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha kilomita 368 kutoka Makutupora hadi Tabora utatiwa saini leo Ikulu huku rais Samia akishuhudia

Soma pia: Uzi mkuu unaoonesha yaliyojiri kwenye mradi wa SGR tangu kuanza kwake mpaka mradi ulipofikia hivi sasa


20211228_075425.jpg
 
Screenshot_20211227-205111_WhatsApp.jpg


Kwa hilo la mwendelezo wa ujenzi wa reli 'SGR' Rais Samia anahitaji kupongezwa sana kwa uthubutubu wake.

Hatimaye kipande cha Makutupora kuelekea Tabora utiaji wa mkataba wake unafanyika leo na kubaki kilomita 166 pekee katika ujenzi wa Dar es Salaam-Mwanza kukamilika wote.

Kwa dhati ya moyo wangu nakupongeza sana Rais Samia.
 
Nini kinachelewesha, maana ilikuwa ianze mwishoni mwa 2019 na sasa naona wataja 2022
Kwanza huo mradi ni wa kusanifu na kujenga hapohapo tofauti na miradi mingine ya usanifu hufanyika kabla kwa hiyo hiyo nayo ni changamoto.

Pili hilo janga la Corona limeendelea kuleta changamoto kwa kuchelewesha vifaa hasa vya kutoka nje ya Nchi kufika hii ni kwa sababu viwanda vya wenzetu kule nje kuna wakati viliacha kufanya kazi kwa sababu ya lockdown hali iliyopelekea uundwaji wa vifaa hitajiki kwenye mradi.

Kwa uchache hizo juu ndizo changamoto za uchelewaji wa mradi ndugu.
 
Back
Top Bottom