Tusirudi nyuma kuhusu kuhamishia serikali Dodoma, hii pia inapunguza presha ya watu na makazi Dar, ukichukulia mfano wa jiji la Lagos nigeria serikali ilihamia abuja nafikri kupunguza presha kwenye hilo jiji kwa sababu limeshakuwa na watu wengi na hivyo movement za watendaji wa serikali zinakuwa ngumu kuweza kutekeleza majukumu yao. Hii pia itasaidia kuendeleza miji mingine, mfano Dodoma yenyewe, na mikoa jirani kama singida na manyara. Pamoja na serikali kuhamia dodoma bado huwezi kumpangia rais sehemu ya kufanyia kazi kwa sababu ana ofisi kila mkoa, nafikiri hata wilayani..