Rais Samia kuwa kama Hayati Magufuli, achana na maridhiano na wasiotaka, watakupotezea muda

Magufuli aliweza kufanya vile kwa sababu Wananchi walimwelewa kwa jinsi alivyokuwa akiwashughulikia hata wenzie ndani ya Ccm na ndani ya Serikali !!

Hata sasa akija hardliner mwingine akafanya vile vile mpaka watu wakubwa wakanywea hakik Wananchi watamwelewa sana !!

Je mnataka muanze kutumbuliwa hata mikutanoni ??!!
Naona labda majipu yameshaiva 😅😅😅🙏🙏🙏🔥
 
[emoji1787][emoji1787]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Wapinzani na watz sio wakuwaonea huruma kabisa
 
Ukweli ni lazima usemwe ukipenda vya dezo dezo vina masharti yake mkuu
 
Hamna cha mazingira, Tanzania ilikuwa inaendelea vizuri tu bila hivi vyama uchwara
Tanzania haijawahi kuendelea vizuri, sema CCM mmefaidika na uoga na ujinga wa watanzania wengi, hivyo kunapotokea mabadiliko mnapata shida maana hamko tayari kuendana na mabadiliko. Hata huyo Magufuli unayemsimfia, humsifii kwa ubora wa uongozi bali kwa kiburi cha madaraka. Mtu mjinga tu ndio huona kiburi cha madaraka ndio uongozi.

Iko hivi, sio Magufuli, sio mama Samia au kiongozi yeyote wa CCM atakayeweza kuwaburuza tena watu, maana hiki ni kizazi kingine. Ufahamu kuwa ccm sio chama cha kizazi hiki, hivyo mabavu yenu lazima yafikie mwisho. Nikushauri tu, muda wa CCM kuendelea kukaa madarakani kwa ridhaa ya umma ulishapita, na haya magumu unayoona inakutana nayo ni kwa sababu ya mabadiliko hayo ya kizazi, huku yenyewe ikiwa haikubaliani na ukweli huo.

CDM sio chama cha kuendelea kuwa chini kwa ghiliba za CCM, hiyo mbinu ya kujifanya mnawasikiliza kisha hakuna utekelezaji wowote, hiyo ni kupotezeana muda. Mnaruhusiwa kumshurutisha mama Samia kutawala kama alivyotawala dhalimu Magufuli, lakini mabadiliko ya kuitoa CCM hayataisha hadi itoke madarakani kwa heri au kwa shari.
 
Ndio tunataka dikteta mwingine kama Magufuli wa kufutilia mbali hizi takataka zinazotukana hovyo, hapo ndio Samia kaniangusha basi
Si dictator kama Magufuli, mngempata hata iddi Amini kabisa, kizazi cha CCM kilishapita. Msilazimishe kutawala watu kwa wizi wa kura wakati hakuna anayewataka. Na haya matamanio yenu ya kutaka kuendelea kutawala nchi hii kwa shuruti yatafikia mwisho.

Nenda huko Mbarali kuna kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge, kwakuwa CDM haishiriki uchaguzi umepoa ile mbaya, hiyo ni ishara kuwa CCM mko madarakani kwa wizi wa kura, lakini walio wengi hawawataki.
 
Tanzania ni nchi huru, hakuna cha beberu wala nani atakayetutishia kwenye maamuzi yetu...Kama mikutano imejaa matusi na uchochezi inafungiwa tu, tunachapa kazi... Hatutaki kuwa kama DRC nyingine
DRC haiwez letwa na upinzani wala hakuna mpinzani wa kuleta machafuko hakuna, bali mienendo ya watawala na dhiki za watanzania while kuna rasilimali za kila aina ndio itayofanya wananchi wachoke!! NB: Hamna ubav wa kupingana na MABEBERU mshakubal kua ombaomba imagine hata budget ya serikali mnategemea msaada wa MABEBERU! Ukishakubali kuolewa hakika nakwambia huez lala na chupi!!
 
Kufanya hivyo awe tayari kuishia hivyo hivyo na Makamu wake kushika nafasi, maana mwenyezi Mungu ataamua kesi atakapoendelea kuikanyagia chini Katiba.
 
Mleta mada kumbuka hii nchi sio ya ccm wala mama yake na CCM BALI ni ya watanzania wote!
Msijilimikishe nchi nyie viumbe!
 
Hamna cha mazingira, Tanzania ilikuwa inaendelea vizuri tu bila hivi vyama uchwara

Sasa si katiba ingewekwa chama kimoja tu. Hakuna chama uchwara kama katiba inavitambua na ruzuku wanapewa.
Hautaki katiba itambue cha kimoja vingine vifutwe
 
Magufuli aliwashugulikia mafisadi wote bila kuangalia sura zao. Suala la Bandari pekee limemuweka mbali sana na mtangulizi wake. Uzuri wananchi ni waelewa na wanajua ni wapi watafanya maamuzi.
 
Wengine tulijua honeymoon ikiisha,maigizo yote yataisha pia!

Kila awamu huanza kwa mbwembwe za kutaka kujitofautisha na mtangulizi ila ni wale hardcores tu akina JPM ndiyo hudumu kwenye huo utofauti.

Angalia hata Ruto tu alivyoanza na alivyo sasa baada ya kujua strength ya Raila.
 
Umeme wa uhakika umeshinda.

Huduma ya maji ya uhakika imemshinda.

Wezi waliotajwa kwenye ripoti ya CAG ameshindwa kuwafunga.

Magufuli huko alipo ana yale mabunduki na jamming devices zilizokuwa zinamzunguka na je zilimsaidia vipi asiondoke?

Ndio leo mnamdanganya apambane na wanaomkosoa?
 
Nyie matapeli kama mlishindwa kuitoa CCM pamoja na kumchukua yule fisadi 2015, hamtakaa muitoe tena, maana watanzania ndio waliona sura zenu halisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…