Rais Samia kuwa kama Hayati Magufuli, achana na maridhiano na wasiotaka, watakupotezea muda

Nikikumbuka tulikotoka, Samia alivyorekebisha mambo mengi halafu sasa hivi mijitu inatukana familia yake, inamdhalilisha kijinsia, inambagua asili yake, hata dini yake,. Naona hawa watu haina haja ya kuwa muungwana kwao, usiwape uhuru, hawapo responsible katika kutumia huko uhuru
 
Awe mkatili maradufu kumzidi jiwe. Acha kumshauri rais vibaya
 


Kwa akili yako anayafanya sababu kaamua kufanya maridhiano na hayana faida kwake!!!!!! Za kuvuka barabara hizi.
 
Nyie matapeli kama mlishindwa kuitoa CCM pamoja na kumchukua yule fisadi 2015, hamtakaa muitoe tena, maana watanzania ndio waliona sura zenu halisi
Kwa taarifa yako kwa mazingira haya ya uchaguzi, ccm itaendelea kutangazwa washindi na sio kushinda. Lakini mazingira yakibadilika aidha kwa machafuko ama mapinduzi ya kijeshi uje utoe mrejesho. Hakuna wananchi wanaoamua nani awe rais nchi hii, bali kigenge kinachojiita system ndio huamua nani awe rais, bila kujali box la kura linasemaje. Sasa sijui ni wananchi gani unawaongelea.
 
Vyovyote vile, ni afadhali kutawaliwa na CCM, shetani ninayemjua kuliko Chadema, ambayo hata sasa kabla ya kuwa na madaraka wanaonyesha ni wabaya mara 100 kuliko CCM, wakiwa na madaraka sijui itakuwaje
 
Vyovyote vile, ni afadhali kutawaliwa na CCM, shetani ninayemjua kuliko Chadema, ambayo hata sasa kabla ya kuwa na madaraka wanaonyesha ni wabaya mara 100 kuliko CCM, wakiwa na madaraka sijui itakuwaje
Mabadiliko hayakwepeki boss, ndio maana unaona wizi WA kura umebaki kuwa ngao ya CCM kubaki madarakani kwa shuruti. CCM sio chama cha kizazi hiki. Ni sawa na kutaka kizazi hiki kisikilize miziki ya Sikinde na Ottu jazz, badala ya miziki ya kina Ali Kiba na Diamond.
 
Si kweli kwamba Rais Samia amekuwa fair kwa CHADEMA, bali Katiba yetu ndo inayowapa uhuru CHADEMA kufanya mikutano.
 
Tanzania ni nchi huru, hakuna cha beberu wala nani atakayetutishia kwenye maamuzi yetu...Kama mikutano imejaa matusi na uchochezi inafungiwa tu, tunachapa kazi... Hatutaki kuwa kama DRC nyingine
...[emoji848] Hamuamini Mahakama mlizochagua Nyinyi Wenyewe ?? Anayeona ametukanwa SI aende Mahakamani ?? Mnaogopa ??
 
1.Maridhiano maana yake ni nini??

2. Ni kitu/jambo gani linaloridhiwa??
 
Si kweli kwamba Rais Samia amekuwa fair kwa CHADEMA, bali Katiba yetu ndo inayowapa uhuru CHADEMA kufanya mikutano.
Katiba yetu ilikuwa ni hiii hii awamu ya 5 ila walikuwa hawafanyi hiyo mikutano
 
Kwa taarifa yako hata huyo Magufuli kama angeendelea mpaka leo, hayo maridhiano angeyatafuta tu.
Tanzania ni maskini sana kujitutumua eti hujali.
Ilikuwa ni suala la muda tu, mdororo wa uchumi ungemlazimisha na angesalimu amri tu.
Hakuna aliyekuwa na kiburi kama Mwalimu Nyerere, aliyethubutu kutaifisha hata makampuni ya wazungu na waliojaribu kumuingilia kwenye maamuzi aliwatimua nchini kama alivyowatimua raia wote wa iliyokuwa ujerumani ya magharibi enzi hizo miaka ya 70.
Lakini ilifika mahala aliona hawezi kuendelea na aina hiyo ya misimamo na ili asionekane amesalimu amri ilimbidi astaafu na kumuachia Mwinyi ndio akubali yale aliyoyakataa.
Kwa hiyo hakuna ubabe wa kudumu, zaidi utakaribisha kuondolewa kwa nguvu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…