Rais Samia kuwa kinara wa afya ya Mama na mtoto Afrika ni heshima kwa Tanzania

Rais Samia kuwa kinara wa afya ya Mama na mtoto Afrika ni heshima kwa Tanzania

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
Mshauri wa Rais kuhusu Afya ya uzazi na afya ya Mama, Ummy Mwalimu amesema Afrika imepiga hatua katika kupunguza vifo vya kina Mama ambapo ameongeza kuwa Suala la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa kinara wa Afrika afya ya Mama na mtoto ni heshima kubwa kwa Tanzania na kuongeza kuwa uamuzi na utashi wa kisiasa wa Rais Dkt. Samia ndo umepelekea Afrika kumtambua na kumpa jukumu hilo la kuwa kinara Afrika wa afya ya Mama na mtoto.

Aidha Ummy amesema kupitia Mkutano Maalum wa Ngazi ya Juu wa Kundi la Afrika la IPU wamepata heshima ya kuweza kuongea na wabunge wanaotoka katika bara la Afrika ( African Geopolitical Group) ili kuwapitisha katika mpango elekezi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa sifuri tatu ili kutokomeza vifo vinavyozuilika vya Mama na mtoto.

 
Hii habari imekaa kiudaku sana
bi chura ni kinara wa kuua watoto wetu ananuka damu hilo lipo wazi kabisa!
 
Alijali afya ya Maiti zetu wakati wakiwa hai.
Pongezi kwake.

Tunataka kuzika.
Acheni maisha ya Netflix Qmmmk.
 
Back
Top Bottom