Rais Samia kuwa makini! Kuna genge linakuandama ili uharibu

Rais Samia kuwa makini! Kuna genge linakuandama ili uharibu

Inevitable

Senior Member
Joined
Apr 27, 2012
Posts
123
Reaction score
319
Salaam mama, hongera kwa kuanza kazi vizuri na pole kwa yote utakayokuwa unakumbana nayo katika siku hizi za mwanzo.

Mhe. Rais, naomba nikujuze yafuatayo:
  • Kuna genge flani la waliokuwa wanufaika wa mfumo haramu limekupania na litatumia Media na Mitandao ya kijamii kukuandama ili upate aidha kufungia Vyombo vya Habari au kutoa kauli ya kuwakwaza wananchi na upoteze momentum uliyoanza nayo. Kuna siku tutakufahamisha nani ni nani katika genge hili, nasi wengine tunauangalia upepo wako ndani ya siku 100 za mwanzo
  • Lipo kundi jingine ambalo umeliacha Serikalini tena ukawapa nafasi za uongozi wa juu ambao nikiri huenda hukuwajua kwa uzuri ila ndo maadui zako wakubwa. Kuna watu ulichomekewa, ukawabakiza serikalini. Wana mtandao wao na wanawasiliana kila uchao kukuangusha. Wako heavily financed hawa lakini finances zinakotoka utapajua muda si mrefu. Hofu yangu ni kama wenye mandate ya kukufahamisha juu ya magenge haya watafanya hivyo na ndani ya muda.
  • Kuna kundi ambalo lilihusika na ufisadi wa mali za watanzania na lilikuwa ni mfumo batili ndani ya mfumo sahihi. Hawa walikuwa wanapigana usiku na mchana (baada ya JPM kuwa katika hali iliyowaonyesha wazi haamki tena) kuhakikisha wewe huwi Rais na walikuwa na vikao vya siri, kimsingi walitaka kupundua meza na kufanya mambo yao. Ni bahati kuwa kuna wazalendo ndani ya Vyombo vya Ulinzi waliosimamia show kuhakikisha Katiba inafuatwa (taarifa hii najua umepewa, sina hakika ni kwa kiwango gani ilikuwa detailed)
Natambua kuwa bado unao muda wa kutosha kujipanga, endelea kuchapa kazi na unao uungwaji mkono mkubwa toka kwa wananchi wazalendo ambao tunaelewa dhamira yako njema.

Nasisitiza tu: Usiingizwe mkenge ili magenge haya yafanikishe azma yao. Watajitahidi kupindisha kila kauli yako ili uonekane huna jipya. Watajitahidi kukufanya uonekane dhaifu (weak) kwa kila hatua utakayochukua lakini nikuhakikishie – mpaka sasa unao uungwaji mkono mkubwa toka kwa wananchi, jamii ya kimataifa na wote wanaolitakia Taifa hili mazuri kwa hatua ulizozichukua; ni hadi pale utakapoingizwa mkenge nawe ukajichanganya, hapo utaona wadau mbalimbali wakikugeuka.

To be specific, naomba uchukue tahadhari dhidi ya hawa watu:

1) Rostam Aziz (hata kupitia kwa Hussein Bashe)

2) Makonda Paul (Albert Bashite)

3) Humphrey Polepole

4) Dotto James

5) Bashiru Ally

6) Muchembe Mabula
Watanzania tupo nyuma yako mpaka sasa. Naamini ukishafikisha siku 100 utakuwa umejipanga vema, hapo nasi tutaujua vema mwelekeo wako.

Tutakuanikia yote ambayo hutoamini kuwa yalikuwa yakiendelea nyuma ya pazia. Pia, upigaji mkubwa uliofanywa na zilikowekwa pesa.

Nakutakia utendaji mwema, Mungu akusimamie
 
Mimi nashangaa nani kawazibua Watu. Kuna maneno yanatamkwa hivi sasa ambayo hata kuyaandika kwa siri enzi za Hayati Magufuli ilikuwa ngumu. Kila mtu sasa hivi anaona anaweza kuongea anyhow kuhusu Rais.

Rais anababatizwa mavitu tu mara hiki mara kile, hujafanya hiki hujafanya kile. Tuwe na heshima.
 
Mimi nashangaa nani kawazibua Watu. Kuna maneno yanatamkwa hivi sasa ambayo hata kuyaandika kwa siri enzi za Hayati Magufuli ilikuwa ngumu. Kila mtu sasa hivi anaona anaweza kuongea anyhow kuhusu Rais.

Rais anababatizwa mavitu tu mara hiki mara kile, hujafanya hiki hujafanya kile. Tuwe na heshima
Hata humu wamejaa kupotosha vitu vilivo dhahiri, inabidi mama atoe baadhi sadaka ka mfano kwa wengine, na wengi ni wale waliokuwa wanakula mema ya nchi
 
Maza inatakiwa ayavurumushe masalia ya marehemu dikiteta magufuli ambayo hayana utu na yako radicalized, tena aanze na huyo katibu wa habari.
 
Mama ni mdemokrasia ameacha watu wazungumze wapendavyo..ndio hayo unayoyaona sasa
 
Hata humu wamejaa kupotosha vitu vilivo dhahiri, inabidi mama atoe baadhi sadaka ka mfano kwa wengine, na wengi ni wale waliokuwa wanakula mema ya nchi
Kweli kabisaaa,asipojua kujisimamia mwenyewe akaruhusu kila jambo ashauriwe,ataanguka vibaya sana.
Muhimu asimwache Mungu wake aliyemfikisha hapo,aombe sana hekima,busara na kutafuta maarifa katika kuongoza hii nchi.
Mimi kwangu naona amekuja muda muafaka.
 
Hakuna wa kumkwamisha SASHA atakwamishwa na uwezo wake mdogo kuongoza nchi. Kuongoza nchi sio rahisi kama kuunga unga elimu.

Magufuli alikuwa very strong haikuwa easy kuyumbishwa na fala yoyote alikuwa na misimamo na uthubutu.
 
Hata mimi nimewastukia, wameshaanza kutwist maneno yake na nengine kuyatake out of context ili kuharibu maana na nia nzuri ya raisi Samia
 
Maza inatakiwa ayavurumushe masalia ya marehemu dikiteta magufuli ambayo hayana utu na yako radicalized, tena aanze na huyo katibu wa habari.
Mama bado anawahurumia Ila watamu cost Sana, hata hao mawaziri wako naye kimwili ila kiakili hawako naye
 
Hakuna wa kumkwamisha SASHA atakwamishwa na uwezo wake mdogo kuongoza nchi. Kuongoza nchi sio rahisi kama kuunga unga elimu.
Magufuli alikuwa very strong haikuwa easy kuyumbishwa na fala yoyote alikuwa na misimamo na uthubutu.
Sema alikuwa na msimamo wa kuua na kupoteza watu wasio na hatia bila hofu.
Kama huo ndo ungangari wa kiuongozi basi hatuutaki
 
Kweli kabisaaa,asipojua kujisimamia mwenyewe akaruhusu kila jambo ashauriwe,ataanguka vibaya sana.
Muhimu asimwache Mungu wake aliyemfikisha hapo,aombe sana hekima,busara na kutafuta maarifa katika kuongoza hii nchi.
Mimi kwangu naona amekuja muda muafaka.
Mama anawahurumia inabidi asafishe nyumba hasa maana wengi walitaka awe anatumia biti za mwendazake, Ila kuona uelekeo tofauti wameanza chokochoko, pia aruhusu vyama vya siasa kufanya siasa na huko ccm awaambie kila mtu atapambana jimboni na upinzani na ukishindwa hamna kupewa ushindi wa mezani, ili Sasa ccm waache Vita vya ndani kwa kupambana na upinzani na sio wao kwa wao.
 
Back
Top Bottom