Rais Samia kuwa mgeni rasmi kongamano la BAWACHA siku ya wanawake duniani

Rais Samia kuwa mgeni rasmi kongamano la BAWACHA siku ya wanawake duniani

Naiona serikali ya mseto kwa siku za usooni.

Mbowe Waziri Mkuu

Tundu Lissu Waziri wa Sheria


Godblesss Lema Waziri wa Mambo ya Ndani

Hao ni kwa uchache.

Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ni kabla ya 2025.

Serikali tatu znakuja.

Hata hivyo, Mama awe makini sana CCM hawapendi haya mambo.

Wanasiasa wa upinzani watalazimika kuunda serikali moja na CCM Kama njia ya rahisi ya kupunguza nguvu za dola za CCM na pia ni kwasababu watanzania wamekuwa waoga kupambana na dola kuindoa CCM madarakani

Mtanielewa yakitimia.

Nimemaliza.
Wale wanyama wa serengeti wanaohama hama wanafanana sana na chadema.

Kumbe wanachokitaka wananchi ni mbowe kuwa waziri mkuu???
 
..Samia atakuwa ktk uhalisi wake na kutoa makucha wakati wa Uchaguzi na kutangaza matokeo.

..Sasa hivi Ccm na Cdm wanatumiana tu. Subirini 2024 na 2025 muone kitakachotokea.

..JK mnayemsema ni muungwana si ndio alipora uchaguzi wa Znz akimtumia Bwana Jecha.

..Na unasema Znz hawajazoea ukatili umesahau mauaji ya wakati wa Karume mkubwa?
Exactly, sidhani kama wana fahamu kuhusu habari za mazombie zanzibar.
 
Ni sawa na hakina swala kumualika simba mgeni rasmi kwenye mkutano wao. Interesting kusikia watakachoongea kwenye huo mkutano.

Ingeeleweka kama wanamama wanasiasa wa vyama vyote kufanya kwa pamoja na Bi Tozo kuwa mgeni rasmi. Lakini shughuli ya BAWACHA halafu mgeni rasmi mwenyekiti wa CCM, only in Tanzania.
 
Ni sawa na hakina swala kumualika simba mgeni rasmi kwenye mkutano wao. Interesting kusikia watakachoongea kwenye huo mkutano.

Ingeeleweka kama wanamama wanasiasa wa vyama vyote kufanya kwa pamoja na Bi Tozo kuwa mgeni rasmi. Lakini shughuli ya BAWACHA halafu mgeni rasmi mwenyekiti wa CCM, only in Tanzania.

Leo mnamkana Samiah sio Rais wa nchi. CHADEMA wamemwita Kama Rais sio Kama mwanaccm. Mabadiliko magumu Sana Tanzania.
 
Umesema jambo la msingi sana kuliko hao wanaobeza juhudi za cdm.

Nashangaa sana na watu wa ACT nao wanabeza
Kutokana na katiba yetu ilivyo yatupasa kuwa wapole tu maana wananchi wa kusaidia ipatikane hawapo. Njia pekee ni kukubaliana na CCM tu. Maana tukiwasusia wengine wanakubali
 
Leo mnamkana Samiah sio Rais wa nchi. CHADEMA wamemwita Kama Rais sio Kama mwanaccm. Mabadiliko magumu Sana Tanzania.
Kwakuelewa ni raisi wa nchi na mwanamama ndio maana nikaandika isingekuwa jambo la kushangaza kama hiyo sherehe ingekuwa imeandaliwa na vyama vyote.

Lakini ukishasema ni hafla ya BAWACHA halafu mgeni rasmi ni mwenyekiti wa CCM ni jambo la kushangaza kidogo; na ndio maana binafsi naona itakuwa interesting kusikia hiyo theme ya mkutano wao kesho na kitakachoongelewa.

Unajua psychologically to make something special inabidi uwaaminishe watu it’s special.

Sasa kama mwenyekiti wa chama pinzani ndio mgeni special kwenye mkutano wenu hiyo ni message gani kwa wananchi na wanachama wa CDM.

Keshokutwa viongozi wa BAWACHA wakimkosoa Bi Tozo tukawaita wanafiki kupitia mkutano wao ambao chances watatumia muda mwingi kumpamba utakataa vipi hao watu kuitwa wanafiki wakati mwenyekiti wa CCM ni shujaa wao.
 
kwenda mbele zaidi kwenye umoja kiongozi wa Chadema apande jukwaa la ccm na wa ccm apande jukwaa la Chadema hata atoe salamu tu kwa wanachama
tukifika huko sasa kuelekea katiba mpya na tume huru itakua simple.


Watu wengi hawajamwelewa huyu Mama kashaona wapinzani ni wadau wa maendeleo la sio wanafiki. Huwezi kuchukua mawazo kutoka kwa chawa
 
Kumbuka Samia anatoka Zanzibar hajazoea ujambazi na uhuni wa bara. Dini yake inamfunga kuwa kila mtu ana haki sawa hakuna aliye juu ya mwenzake na ukumbuke ni muislamu siyo dini ya kijinga na ya kijasusi na ya kuuana ya kikristo
Wewe Sasa unatafuta vita na hao wasabato😄
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) lililoandaliwa na Baraza la Wanawake (Bawacha) wa chama hicho.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumapili, Machi 05, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, amesema Rais Samia amethibitisha kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo litakalofanyika Machi 08 Moshi mkoani Kilimanjaro.

“Kongamano hili la siku ya wanawake duniani ni la wanawake wote, lakini hapa Tanzania, Bawacha wamekuwa wakiliandaa kwa mafanikio makubwa kila mwaka na wamekuwa wakitoa hotuba zenye jumbe mbalimbali zinazowahusu wanawake wote bila kujali itikadi za vyama vyao.

“Napenda kuwatangazia kuwa Rais Samia ambaye nilikuwa na mazungumzo naye jana Jumamosi, amekubali kuwa mgeni Rasmi siku hiyo na mimi nitampokea mjini Moshi siku hiyo,” alisema Mbowe

Rais Samia kukubali kuhudhuria na kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano linaloandaliwa na chama kikuu cha upinzani ni matunda ya maridhiano ya kisiasa yanayoendelea kufanywa na chama chake (CCM) na Chadema.


RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKIWAPUNGIA WAJUMBE KWENYE MOJA YA MIKUTANO YA CHAMA CHAKE (CCM) AMBAPO YEYE NI MWENYEKITI TAIFA
Maridhiano hayo awali yalianza baada ya Rais Samia kuunda kikosi kazi cha kuishauri serikali kuhusu mwenendo wa kisiasa nchini.

Lakini maridhiano yalitiwa chachu baada ya kikao cha kwanza kati ya Rais Samia na Mbowe kukutana Ikulu, Machi 04, 2022 siku ambayo Mbowe alitoka gerezani baada ya Serikali kuifuta kesi ya ugaidi iliyokuwa inamkabili mwanasiasa huyo.

Kati ya mambo ambayo Chadema waliyapeleka kwa Rais na kutaka yarekebishwe haraka ni pamoja na kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa wa Chadema, jambo ambalo kwa asilimia kubwa limeshafanyika.

Jambo la pili ni kuweka usalama kwa wakimbizi wa kisiasa waliokimbia nchi. Tayari viongozi wa Chadema waliokimbia nchi wamesharejea. Viongozi hao ni Tundu Lissu, Ezekia Wenje na Godbles Lema.

Jambo la tatu lililodaiwa na Chadema ni kuondoa zuio la mikutano ya hadhara ambapo tayari Januari mwaka huu, Rais Samia ameondoa zuio hilo.

Jambo la nne ni upatikanaji wa Katiba mpya ambapo mpaka sasa mchakato haujaanza.

View attachment 2538065

Loh salalaaah!!
 
Back
Top Bottom