Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 32,639
- 42,908
Vita dhidi ya nani?Tunarembesha rembesha maneno wakati wanajeshi wanakufa huko eti "kwa ukarimu" huu ni wakati wa vita
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vita dhidi ya nani?Tunarembesha rembesha maneno wakati wanajeshi wanakufa huko eti "kwa ukarimu" huu ni wakati wa vita
Hapo ndiyo pa kuhakikisha Marshall Mothers A Real Slim Shady Eminem anarudi kwao akiwa kwenye sanduku la postaUthibitisho wa wawili hao kukutana umetolewa na Rais William Ruto wa Kenya, Februari 3, 2025.
Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Paul Kagame wa Rwanda, wanatarajia kukutana jijini Dar es Salaam, Februari 8, 2025 kujadili mustakabali wa hali ya usalama katika eneo la Mashariki mwa DRC.
Taarifa iliyotolewa na Rais wa Kenya William Ruto, wawili hao watakutana katika mkutano wa pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), baada ya Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kuridhia nchi yake kuwa mwenyeji wa mkutano huo.
Hatua hiyo inafuatia makubaliana kati ya mwenyekiti wa SADC Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe na Rais William Ruto wa Kenya, ambaye pia ni mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya EAC.
“Rais Samia Suluhu Hassan amekubali kuwa mwenyeji wa mkutano huo ambao unalenga kutafuta suluhu ya mgogoro wa Mashariki mwa DRC," alisema Rais Ruto.
Kulingana na Rais Ruto, wawili hao wamethibitisha uwepo wao kwenye mkutano huo wa pamoja ambao utatanguliwa na mkutano wa mawaziri siku ya Ijumaa, kabla ya Wakuu wa EAC na SADC hawajakutana siku ya Februari 8, 2025.
Rais Ruto pia amesemsa kuwa amewashirikisha jambo hilo Marais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Yoweri Museveni wa Uganda na Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia.
Samora alikuwa akitokea Lusaka, Zambia.Tanzania tusingekubali kuhost mkutano huo ili kulinda hadhi na heshima ya Nchi Kimataifa.
Ni vipi kama baada ya mkutano ndege ya Kedi na Rama zikapotea mawasiliano kwenye Rada?. Au ndege ya Kagame?.Nakumbuka ndege ya rais wa Rwanda na Burundi; hata ile ya Samora zilikuwa zinatokea Dar kwenye Mkutano
Sasa suluhu itapatikanaje ilhali wao ndio wahusika wakuu kwenye mgogoro huu?BBC wamesema Tchisekedi akitokea Kagame hatokei Kagame akitokea Tchisekedi hatokei
Nadhani ni kwasababu ni nchi inayoonekana kutofungamana na upande wowote, amani inayosemekana ipo na uimara wa jeshi unaosemekana upo pia.Shamba la bibi wanajua atagharamia Kila kitu
Ameweza kupatanishwa na CHADEMA?03 February 2025
Dar es Salaam, Tanzania
Rais Samia Suluhu Hassan amekubali kwa ukarimu kuandaa mkutano huo kujadili hali ya Mashariki mwa DRC
DAR ES SALAAM KUPOKEA MARAIS WA NCHI ZA SADC NA EAC KUJADILI MGOGORO WA NCHI YA DR CONGO
Mkutano wa pamoja wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) utafanyika Ijumaa na Jumamosi kuhusu mzozo wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Hii inafuatia makubaliano kati ya Mwenyekiti wa SADC Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe na Mwenyekiti wa EAC Rais William Ruto wa Kenya.
"Rais Samia Suluhu Hassan amekubali kwa ukarimu kuandaa mkutano huo kujadili hali ya Mashariki mwa DRC," Rais Ruto alisema.
MORE INFO :
Baada ya M23 Kunyakua pande la jimbo la Kivu ya Kaskazini uliopo mji wa Goma na kuonekana kuelekea Kivu ya Kusini mjini wa Bukavu.
Marais wa kanda za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na wale wa nchi za Kusini SADC wamependekeza pande mbili katika mgogoro wa ndani wa DR Congo wa kujongea katika meza ya mazungumzo kutafuta utatuzi wa kudumu
Pia soma
- Waasi wa M23 sasa waelekea mji wa Bukavu