Rais Samia kuwa mwenyeji wa mkutano wa marais wa nchi za SADC na EAC kujadili Mgogoro wa DR Congo

Rais Samia kuwa mwenyeji wa mkutano wa marais wa nchi za SADC na EAC kujadili Mgogoro wa DR Congo

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Felix Tshisekedi, na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, wanatarajiwa kukutana Jumamosi, Februari 8, 2025, jijini Dar es Salaam kujadili mgogoro unaoendelea DRC.

Akitoa taarifa hiyo leo Jumatatu, Februari 3, 2025, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Rais wa Kenya, William Ruto, amesema mkutano huo utahusisha marais wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Sadc) na EAC.

"Rais Samia Suluhu Hassan amekubali kwa ukarimu kuandaa mkutano huo kujadili hali ya Mashariki mwa DRC," amesema Rais Ruto.

Ruto ameongeza kuwa Rais Tshisekedi wa DRC na Rais Paul Kagame wa Rwanda ni miongoni mwa waliothibitisha kuhudhuria mkutano huo utakaotanguliwa na mkutano wa mawaziri Ijumaa, Februari 7, 2025.

Soma Pia: Congo DRC yavunja uhusiano na Rwanda kufuatia mzunguko wa Goma unofanywa na waasi wa M23


Pia, amesema wengine waliothibitisha kushiriki ni pamoja na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, na Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia.

Mkutano huo wa dharura unafanyika wakati DRC ikiishutumu Rwanda kuhusika na mgogoro unaoendelea nchini humo ukiongozwa na waasi wa M23, huku Rwanda nayo ikiishutumu DRC kutaka kuipindua Serikali yake.
 
Huyu huyu paulo aje Dar kusuluhisha mgogoro? Ngoja tuone
 
Tafuteni hotuba ya George Bush baada ya tukio la Septemba 11. Kwenye Mambo kama haha inatakiwa kuwa na upande ili uhesabiwe. Ndio hivyo
 
Back
Top Bottom