Rais Samia kuwa mwenyeji wa mkutano wa marais wa nchi za SADC na EAC kujadili Mgogoro wa DR Congo

majitu yana uhasama halafu yaje kufanya mkutano kwetu, je yakitunguana angani nchi yetu itaeleweka vipi?
 
Hivi chupi na sidiria na shumizi shingapi madukani siku hizi .
 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambaye pia ni Rais wa Kenya, William Ruto amesema viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na EAC wanatarajiwa kukutana Jumamosi, Februari 8, 2025, jijini Dar es Salaam kujadili mgogoro unaoendelea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Rais huyo wa Kenya amesema Miongoni mwa waliokubali kuhudhuria mkutano huo ni Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa DRC, Felix Tshisekedi, Rais wa Rwanda Paul Kagame, Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Yoweri Museveni wa Uganda na Hassan Mohamud wa Somalia.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi na Rais wa Rwanda Paul Kagame wameingia kwenye Mjadala Mzito kutokana na Mapigano ambayo yanendelea Mashariki mwa Kongo (DRC) kati ya Vikosi vya waasi wa M23 dhidi ya Serikali ya Kongo (DRC) ambapo kwa asilimia kubwa Rais Felix Tshisekedi anatuhumu Majeshi ya Rwanda kushirikiana na Waasi wa M23.

🇹🇿🙏
 
Tusianze kufungiana tena barabara kama juzi
 
Kagame asiwekwe siti ya karibu na Ramaphosa wanaweza pigana ngumi live wale
Watafutiwe chumba, Kagame na Ramaphosa wayajenge. Ruto akiwa Referee.

Kagame lazima ajibu swali kwanini ameua watu waliokuwa hawapigani. Lengo lake lilikuwa nini hasa. Kama anataka kupigana wamuahidi ataletewa waliojiandaa kupigana ili iwe fair fight. Na mshindi ashinde kilahali sio kuwavizia watu waliokuja kwa amani. Au aombe msamaha na kuwathibiti watu wake M23.
 
DRC na Rwanda ilipaswa wakutanishwe na kiongozi asiye na maslahi pande zote, na mbabe anayeweza kuwapiga biti wote...
 
Huyu kiongozi wa m23 watuambie vizuri hiko kiswahili cha sinza kabisa amejifunzia wapi

KiSwahili lugha ya kimataifa, lugha ya wapambanaji / wakombozi kama rais Cornielle Nangaa wa muungano wa, AFC / M23, Mkuu wa kitengo cha siasa Bertrand Bisimwa wa M23 , Mzee Laurent Kabila rais wa Kongo & jenerali Joseph Kabila wa Congo rais wa Kongo , jenerali Paul Kagame wa Rwanda, jenerali Yoweri K. Museveni wa Uganda, Colonel Dr. George Garang' wa South Sudan, rais Chiluba wa Zambia, marais Felipe Nyusi & Chissano wote wa Msumbiji, jenerali Idd Amin, makamanda wa majeshi ya Ukombozi South Africa (MK)uMkhonto weSizwe ya ANC, PAC, Communist Party of South Africa, rais Munangangwa wa Zimbabwe n.k kwa kuwataja kwa uchache...

Sources :

2013 15 Disemba
Maveterani wa Vita vya Ukombozi South Africa wamshangilia kwa nderemo Jakaya Kikwete

View: https://m.youtube.com/watch?v=IDYpZEee7SwMajonzi ya Afrika Kusini kufuatia kifo cha rais wa zamani Nelson Mandela yalishirikiwa na Tanzania, Rais Jakaya Kikwete alisema Jumapili. Jakaya Mrisho Kikwete ni Rais wa 4 na wa sasa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anaeleza kumbukumbu zake kuhusu Madiba... Source : SABC News

 
Na iwe hivyo.. Historia ijirudie..
 
Hawa waru wanachezea sana pesa zetu, hawa watawala juzi walikuwa hapa kwenye mkutano wa nishati, wakakutana ikulu ya dar kwa dharura kujadili huo mgogoro, juzi walikuwa Zimbabwe kama Sadc kujadili huo mgogoro, leo tena wanajadili warudi Dar kujadili huo mgogoro.

Jamani wanatumia pesa zipi zisizo wauma wao?

Hawana Zoom?

M23 wachapwe watulie, hii kilasiku kujadili hata sielewi wanajadili nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…