Rais Samia kuwa mwenyeji wa mkutano wa marais wa nchi za SADC na EAC kujadili Mgogoro wa DR Congo

Isije ikatokea kama ile ya wakina habyarimana, maana walitoka dar kana wanavyo kuja hawa.
 
Agenda iwe kumpiga kagame mpaka kigali
 
Na huo ndo ulikuwa ukuu na hadhi ya Dar. Sijui kama DOM wana ubavu huo!
 
Binafsi, siafiki mkutano huu kufanyika Dar, NI kupoteza muda tu na kuchezeana akili. Viongozi watakuja na madege yao, na suti zao, watakunywa chai na sambusa, mkutano utafanyika kwenye ukumbi wenye viyoyozi chini ya ulinzi mkali, utaisha, na maisha yataendelea kama kawaida. Rasilimali za DRC zitaendelea kuporwa huku raia wake wakiendelea kutaabika, kuuwawa kama wanyama. Viongozi wote hao wanajua kabisa kwamba chanzo na kiini kikuu cha mgogoro huu ni Paul Kagame, yeye ni mnufaika mkuu wa mgogoro huu. Anawachezea shere, kiburi chake chote kinatokana na uporaji wa madini anaoufanya DRC na kukingiwa kifua na baadhi ya nchi za magharibi. Kama kweli mna nia ya kweli ya kumaliza mgogoro wa Congo MSHIKISHENI ADABU Paul Kagame mtakuwa mmepunguza sana kama si kulimaliza tatizo la DRC. ACHENI KILA KITU SHUGHULIKENI NA KAGAME,
 
1 February 2025

MUSEVENI ASISITIZA RAIS WA DRC FELIX TSHISEKEDI AFANYE KUZUNGUMZA NA M23 NA MAKUNDI MENGINE PIA YALIYOPO KTK MGOGORO WA CONGO


View: https://m.youtube.com/watch?v=2Le4cSxfmYURais Kaguta Museveni anasisitiza kuwa DRC mheshimiwa Felix Tshisekedi anapaswa kuzungumza na M23 na wadau wengine walio katika migogoro naye.

Pia anapendekeza kuwa na Mkutano wa Wakuu wa nchi za jumuiya ya EAC / SADC ufanyike ili kutafuta kwa pamoja suluhu za kukosekana kwa utulivu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hayo ni maneno rais Yoweri Museveni
 
Hii ni fursa muhimu na adhimu kwa Rais Samia.
PK amehojiwa CNN
View: https://youtu.be/ZrlKvJ--pGo?si=IT2tjMdrZLLScJozKwa hii ya PK, kwanye hili la DRC, mimi nasimama na PK, makamanda wake wanawasaidia M23 ili kulinda usalama wa Rwanda!. M23 ni watoto wa Banyamulenge wazaliwa wa eneo hilo, uwafukuze waende wapi wakati hapo ni kwao?.

Mkutano wa Jumamosi ni fursa adhimu kwa Rais Samia, kuirejesha The past Tanzania lost glory ya nchi ya upatanishi. Rais Samia kama Samia, she is not and has never been a negotiator kama alivyokuwa Nyerere, hivyo she needs a strong back up ya the negotiators, one of the best we have ni Prof. Kabudi!.

Hii sasa ndio fursa ya kweli kumpaisha na kumgarisha Rais Samia kimataifa kama mpatanishi wa kimataifa wa amani kwenye migogoro.
P
 
Lazima ifike mahali PK alazimishwe kuheshimu uhuru wa nchi zingine. Na akome mara moja kuua wanajeshi wetu kwa kisingizio kuwa hawatambua walinda amani wa SADC. Kama akiendelea hivyo, tuanzishe front nyingine, kama Tanzania twende tukampige huko huko kwake.
 

Tanzania ipo katika vichwa vya habari ulimwengu wote kuhusu Summit hii ya kihistoria, WaAfrika kutafuta ufumbuzi wa mipaka ya kikoloni iliyowagawa wanandugu kujikuta ni raia wa nchi tofauti kufuatia rula kupigwa kugawanya mapande ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…