Rais Samia kuwapongeza Tabora United kuwafunga Yanga kwenye mechi ya ndani inaonesha upendeleo

Rais Samia kuwapongeza Tabora United kuwafunga Yanga kwenye mechi ya ndani inaonesha upendeleo

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Pale Ikulu kuna watu wanalipwa mishahara ya bure. Tabora United na Yanga ni timu za nchini inakuwaje moja ipongezwe moja inangwe? Je, ni mara ya kwanza Yanga kufungwa?

Screenshot_20241111_073546_Instagram.jpg

Kama mtu ni mgeni anaweza kudhani labda ilikuwa mechi ya kimataifa kati ya Tabora united na Yanga ya Burundi, kumbe zote ni za humu nchini.

Najua ni mara chache Marais kupost wenyewe mitandaoni, kuna timu hupewa kazi hiyo.

Kwa dhati kabisa niseme mmechemsha, hiyo kazi hamuiwezi, Rais ni mlezi wa vilabu vyote nchini hatakiwi kuonyesha upande kwa mechi za ligi kuu.

Mimi sio Yanga ila nilishangaa sana kwa hizo pongezi dhidi ya Tabora UTD.
 
Kwamba ni shabiki wa mnyama ndani ya ofisi namba 1?!
 
Back
Top Bottom