SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Jumatano tarehe 23/03/2022 saa 1:30 asubuhi atakuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa nyumba 644 za wakazi wa Magomeni Kota, Dar es Salaam.
Wananchi wote wanakaribishwa kushiriki.
Ujenzi wa majengo ya kisasa ya ghorofa Magomeni Kota, miundombinu bora ya huduma mbalimbali kama masoko, maduka na viwanja vya michezo umelipa eneo la Magomeni Kota mandhari nzuri na mazingira yenye kuvutia sana.
Mradi wa Magomeni Kota utawapa makazi bora wakazi 644 waliokuwa wakiishi katika eneo hilo kabla ya kuvunjwa mwaka 2009.
Mradi umetekelezwa na kukamilishwa na wakala wa majengo Tanzania (TBA) kwa ubora wa hali ya juu.
Bodi ya ushauri, Menejimenti na watumishi wote wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wanaishukuru na kuipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha fedha za kukamilisha mradi huu wa ujenzi wa nyumba za makazi Magomeni Kota.
TBA ni taasisi Bora na imara ya serikali inayotekeleza miradi ya ujenzi kwa weledi, ubora na gharama nafuu kwa kutumia wataalam wake.
#TBATumekamilisha #MagomeniUshuani #KaziIendelee #TabasamuNaMatumaini