Rais Samia kwa upole huo usiokuwa na kauli ya kukemea tegemea kukwamishwa

Ulianza vizuri kwa kauli za kiuongozi lakini sasa umeanza kupoa tena sana kiasi kwamba utachezewa sharubu sana na
1.Wakwepa kodi
2.mawaziri wako

Mama inabidi awe mkali hata kama si kwa kauli basi iwe kwa vitendo!! Siku hizi mpaka mawaziri wanamchezea hijab kwa kuingia Bungeni wamelewa mpaka wanamsahau hata Jina lake!!! Mama tafadhali watumbue hawa kimya kimya bila kuwatangaza!!!
 
Aliwapiga mkwara viongozi wa dini pale Oeysterbay ( st. Peters ) kuvaa Barakoa
Alipoanza kupambana na viongozi wa dini, hapo ndipo mwisho wake ulipoanzia.

Jamaa hakulala usiku mzima viongozi wa dini walipotangaza wenzao kuchukuliwa na corona, kiasi kwamba kesho yake kaenda yeye mwenyewe kutoa semina kanisanai, kuwafundisha dini waliohitimu huko.
 
Unataka Rais awe mkali kwani rais ndo anakamata wahalifu? **** vyombo vya kushughulika na kila aina ya uhalifu...fanya madudu uone utakavyoshukiwa kama mwewe.

Binafsi nadhani transparency ni more powerful kuliko ukali wa Rais. Na Mh. Rais wetu mpendwa yuko open and transparent. Vyombo vya habari vikiwa huru kuandika na watu wakiwa huru kusema, automatically watu watapunguza madudu ya hovyo hovyo.

Kwenye utawala uliopita ulitengeneza misingi ya ajabu sana. Rais aliwalinda watu wake na kuonea watu ambao kwa namna moja au nyingine alidhani anatofautiana nao au ni tishio kwake.
 
Hata Mimi nimeliona mama hana kelele kiukweli na kwa asili viongozi wetu wengi hawaendi bila ya kelele na kuwapa deadline ya kitu Fulani kiishe muda Fulani niletewe report mkimaliza bila hivyo ukiwauliza watasema tuko kwenye mchakato sijui upembuzi yakinifu...wataalamu bado wnashughulikia nk..nk. Vitu vya mzee na heshima makazini vilikuja kwasababu hiyo.. Utasikia hayaaaaShure italetewa madawati 100 mkurugenzi mkuu wa shure mko wapi? Polisi njooni hapa...pesa hizo hapa ore wenu ipite mienzi miwili dawati hazijaingia....sasa kwa biti hiyo nani anapindua?..mama anasema naomba lifanyiwe kazi /kwa upole inaishia hewani bila biti wengi hawaendi kiukweli. Hongera mama kwa mazuri uliyoanza Nayo wazingue kidogo.
 
Umezoea kufokewa fokewa wewe.aliyekwambia kuongoza nchi ni lazima ugombe ni nani.Huu ujinga wakumtaka rais afanye au aseme kila kitu ndo matokeo yake haya mnaona raisi wa sasa afoki kama mtangulizi wake.Mifumo ya utendaji kazi ya nchi ikikaa vizuri wala hakuna haja yakumuona raisi akiongea au kuchukua hatua ya kila kitu kwasababu mambo yote yatakua yanafanywa na mamlaka husika na ikiwa vinginevyo sheria itachukua mkondo wake.Tatizo lakutokua na mifumo thabiti ndiyo inayopelekea watu wanamlalamikia raisi ata kwa mambo madogo madogo yaliyopaswa yafanywe na vyombo husika.Ifike mahali tuziheshimu sheria zetu na tuziache zing'ate uone kama kutakua na haja ya raisi kua mkali,kwahiyo Sio lazima raisi awe mkali ndo mambo yafanyike.akiwekeza kwenye mfumo wa sheria kila kitu kitaenda sawasawa bila ata kunong'ona lolote.
 
Nimekuelewa
 
Kuongoza kwa kupiga kelele na kufoka foka ni ushamba tu.
 
Anao uwezo wa kuwatengua nafasi zao, labda ashindwe hilo.

Ukiona mwenzako ametenguliwa kwa kutokutimiza majukumu yake ni somo tosha kwako.
Pitch INA matter + kutoa deadline ya utekelezaji bila hivyo watamuumiza sana mama.
 
Sasa wewe jaribu kina cha mahi kwa miguu yako ukisima hakuna kitakacho tokea.
 
Veronica france and company
 
Anaongea hivi hv tu lakn..
Sabaya hana kaz..
TAKUKURU Imefuta kesi za uongo na kweli...
Aliekuwa Mkurugenz TPA yupo home tu sa hv..
Bashiru anatembelea IST tu na mwenzie polepole..hv hv..
 
Ongeza 5. Mabeberu!
 
Mama naomba niteue nafas yyte hapo serikalini.
 

Hata mtoto ukimuagiza kitu anakuangalia na userious wako, huenda ikabidi urudie tena ndio atekeleze. Sasa tone pia inaweza kutuma ujumbe wa “seriousness” ya ujumbe wenyewe. Issue sio kwa sababu amesema Rais. Wapo wenye kumdharau Rais. Nchi kubwa hii.
 
Kumuongoza mwafrica kuna wakati ukali wa maneno unatakiwa na hiyo ni hulka ya kizazi chote cha ngozi nyeusi.
Umewahi hata kufika hapo Kenya hata usema kuwaongoza Waafrika unahitaji uwafokee?
Wewe huna AKILI.
 
Kinachotenda kazi ni pitch ya sauti/tone au kusimamia Sheria Taratibu na kanuni za nchi???
Unadhan awam zilizo tangulia kabra ya ile ya 5 hazikua na Sharia taratibu na kanuni ukizingatia utendaji na ufanisi?
 
Siyo kweli, hakuna haja ya kuiga tabia mbovu za yule mropokaji aliyezikwa Chato.

Hekima, busara, kumuogopa Mungu kwa vitendo, kufuatilia maagizo ndizo nyenzo za Rais SSH.

Tusimpotoshe huyu ana akili nzuri siyo kichaa kama Mwendazake
 
Kila rais ana APPROACHES zake katika kuitawala nchi....

Kubwa kuliko tusisahau pia kila rais ana HULKA yake ya kimaumbile....

UPOLE ,UTULIVU NA MANENO MACHACHE si ujinga ,uoga wala UPUMBAVU.....

TUACHE KUKARIRI!!!

#StaunchSupporterOfSSH
#DieHardFanOfCCM!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…