Rais Samia kwa upole huo usiokuwa na kauli ya kukemea tegemea kukwamishwa

Umekuwa kiongozi wa ngazi gani? Jee ulijifunza utaratibu na mbinu za kutoa maelekezo?
 
Kwanza nianze kwa kukiri kwamba mimi ni sio mwanasiasa ila kwa kipindi fulani nilikuwa shabiki mkubwa wa chadema.Kiukweli miongoni mwa wale waliokuwa wakimponda sana na hata kutokuhuzunishwa na kwenda kwa mwendazake na mimi nilikuwemo.Ninakiri wazi kuwa nilifanya makosa makubwa sana na sikujua kuwa nilikuwa nakataa almasi kwa kukusanya kokoto.

Ni miezi miwili sasa mzigo wangu umekwama bandarini kwa madai kuwa taratibu za ushuru kutokukamilika hali ya kuwa risiti zote halali ninazo.Mbaya zaidi ni mzigo wa biashara hivyo kadri muda unavyoenda nazidi kupata hasara.Sikujua kuwa ukali wa kiongozi mkuu unaweza kusaidia watendaji wa chini wakatimiza majukumu yao kwa weledi na uharaka kwa kumjali mwananchi.Pili hali ya umeme huku mtaani kwetu ni tete,Kila mara umeme unakatika,Na mita za luku system hazifanyi kazi mara kwa mara umeme haununuliki.Ninajiuliza mbona kipindi cha mwendazake haya mambo hayakuwepo? Ina maana utendaji wa hawa wafanyakazi unaangalia zaidi kiongozi mkuu aliyepo juu yao?

Kiukweli nimeshuhudia mambo mengi ya hovyo ndani ya muda huu mfupi,Tukiachilia mbali la kuahirishwa mechi ya Simba na Yanga bila kiongozi yoyote kuchukuliwa hatua,Madawa ya kulevya yameongezeka kwa kasi huku mitaani,wizi na ujambazi navyo vinashamiri ndani ya muda mfupi,Kwanini?

Kwakweli niseme tu kuwa ninajuta sana kumponda mwendazake popote alipo anisamehe na Mungu anisamehe.Na ninamuombea azidi kupumzika kwa amani.
 
sio viongozi wa Tanzania yani hawa wateuliwaa usipowaburuzaa kwa amrii mbona utakomaa mambo hayaendiii..
Foka ya mwenda zake ilikuwa ni kudhalilisha watendaji. Lakini na mama naye anaonyesha weakness katika ligha ya kueleza mambo na utatuzi wake. Anakuwa ni kama mchambuzi wa matatizo ya wananchi wa Tz, lakini hatoi command ni kipi kifanyike, mfano ni pale laini za simu hakutoa kauli kuwa mkurugenzi wa tcra nataka ifanyike namna hii. Kuishia kuchambua ni weakness kwa kiongozi wa mwisho wa nchi,tena amiri kesho mkuu. Mama kazoea kwenye harakati za kuitetea haki za raia bado hajajitambua kuwa theory ya haki za binadamu ni kwenye makongamano tu lakini serikali ni utekelezaji tu sio kuchambua. Anaweza la wazirikuu wa Ethiopia ambaye hadi akapata nobel prize, kwa kuheshimu haki za raia. Lakini amekuja kuelewa kuwa kuongoza serikali ni jambo la imaguvu tu. Hata NYERERE aliwahi kusema maelekezo ya serikali ni amri kwenda mbele . Hivi jkimwambia polisi akishika mtu na kosa amuelimishe tu mkosaji does it make sense kweli? Unamuelimisha nini mtu hana bima au leseni imeisha au overspeeding au sight mirror .hivyo vyote uelimishe tu ? Mama ataanza kutuambia mwizi sugu akikamatwa aelimishwe , wakati ameshaua watu kadhaa unampa elimu gani? I am sure with time atajua tu kuwa ngulumbili ni kuburuzana tu. huwezi kuendesha nchi kwa kuelimisha mtu kitu ambacho anakijua na anavunja sheria kwa makusudi. hasa utozaji kodi kama atadhani wafanyabiashara wanaonewa I am sorry she will learn the hard way kwani hapo akicheza atashindwa kuendesha nchi. asifokee watu, lakini. asitoe nadharia kama za darasani eti nchi itaenda, never. Wishing her every success maana bado anajifunza na yeye janani. A week before haijafa JPM hakuwa na ndiyo ya uraia wa JMT, sasa ghafla amekishika , tumsamehe ajifunze atatenda .Mpango na Majaliwa nina imani wanatosha kumshauri tukafika salama. Nawasalimia kwa jina la JMT. Kazi iendelee. wishing her every success madamme president.
 
 
To lead a successful country cannot come by accident, the leader must be prepared to see successes as a the ultimate choice. Those you lead and implement your vision must do what is required of them without a choice of failure.
 
kuna wajinga wanaomuingiza mama chaka,ili akifelishwa 2025 waje wamnange kwa kununua hisia za watu kupitia kumrejea JPM,mama bila kujua masikini anaingizwa shimoni.

kuna wahuni wanaomchochea mama upole ili wawe huru kuiba,kufanya magendo na uhuni mwingine,likiwemo lile kundi maalufu la msoga.
 
Kwahiyo mtoa mada anataka na mama yetu aanze kutufokea? Kweli duniani Kuna mambo!
 
Kwahiyo mtoa mada alitaka mama yetu naye aanze kutufokea ovyo? Kweli duniani Kuna mambo!
 
Ukizoea kufokewa ndio matokea ya dai lako,Billy Gate kuna mtu alimfokea ili atafute na aupate utajiri !!!???
 
Alishasema yeye anatumia kauli ya upole na maelekezo yake anayatoa kwa kuomba lakini ndiyo anamaanisha. Tumpe muda jamani, bado mapema sana kuanza kumhukumu
 
Kinachotenda kazi ni pitch ya sauti/tone au kusimamia Sheria Taratibu na kanuni za nchi???
Hii mijitu ni mijinga kweli ndio hii ukienda kwake yanafokea fokea tu familia yake na mwisho wa siku watoto wake wanaishia kua malaya na wavuta bangi.
 
Alishasema yeye anatumia kauli ya upole na maelekezo yake anayatoa kwa kuomba lakini ndiyo anamaanisha. Tumpe muda jamani, bado mapema sana kuanza kumhukumu
Apewe mda kivip wakati wenzie washa anza ku temper na mifumo huko wanachepusha pesa aisee mama asiwe hivi watamliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…