Rais Samia lazima awe Mwenyekiti CCM

Rais Samia lazima awe Mwenyekiti CCM

CCM HUWA IMARA ZAIDI INAPOTISHWA KIFO

Na😛hilipo Mwakibinga.
0758910403.

Ndugu zangu Wana wa CCM Kidumu Chama Cha Mapinduzi! Nawasalimu kwajina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naomba niendelee kusisitiza kuwa lazima tuendelee kusimama imara kama sote tunaamini Mungu na tunapokea kila atoalo Mungu na kulipa jina jema la "Baraka." Kamwe tusiwe kama Mpanda gazi hata tukasahau kama kunashuka baada ya Kupanda. Sisi ni Chama Dolla lazima tuwe makini kutokuruhusu kuvunja mila na desturi za CCM.

Ndugu zangu Wana Wa CCM , Baba wa Taifa alikuwa na Jicho kubwa la Tatu hata akaamua kulihali yeye na Wenziwe kuhakikisha RAIS ANAKUA MWENYEKITI WETU. Hii ni muhimu sana kwenye uhai wa Chama,Kwa maana ya Ulinzi na Jeuri ya kuongoza iko hapo. Tusidanganywe kamwe kutawanya kofia hizo mbili kwa vichwa viwili lasivyo tutakua tunalamba asali kwa ncha ya Kisu. Vyama vichanga vinapaswa kutuiga sisi siyo sisi kutafuta busara ya uongozi kwao wakati tunajua kuwa wao walishashindwa hata kabla ya kuanza kushindana.

Ndugu zangu Wana Wa CCM ni bahati sana sana kuwa na Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wetu kwani tunaweza kukutana naye mara mbili wakati wenzetu wanakutana naye mara moja tu. Mosi utakutana naye kama Rais pili Utakutana naye kwenye vikao vya Chama wakati wengine watakutana naye kwenye mosi tu. Yawezekana hatujui umuhimu wa hili sasa lakini tutajuta siku tukipoteza hili. Tuungane pamoja kutetea uhai wa CCM unapotishiwa kukatizwa na hii ndiyo mila na desturi ya CCM hii ambayo kila wakati YAJENGA NCHI.

Ndugu zangu Wana Wa CCM. Makundi na ujuaji usio na maana vitakatisha ndoto za Vizazi vyetu vijavyo kuiona Tanzania yenye maziwa na Asali. Lazima tulinde mazuri na mema waliyotuachia Wazee wetu. Tuhakikishe kuwa mapema sana Rais Wetu Mama Samia anapewa hadhi yake na heshima yake iliyotukuka ndani ya Chama chetu. Mama ndiye Mwenyekiti wetu na anastahili kupewa baraka zetu zote ili kazi iendelee.

Ndugu zangu Wana Wa CCM Rais Mama Samia atakapopewa uenyekiti wa CCM taifa siyo kwaajili yake binafsi ni kwaajili ya CHAMA CHETU. Naomba nieleweke kuwa SISI TUNA MUHITAJI RAIS KUWA MWENYEKITI WETU KULIKO YEYE PENGINE KWAKUA YEYE HAJAOMBA KWAAJILI YA MASLAHI YAKE BINAFSI BALI MILA NA DESTURI ZETU ZINAMPA KWAAJILI YA MASLAHI MAPANA YA TAIFA LETU. TUMPE TUVUKE SALAMA SALIMINI.

CCM tusiingie kwenye mtego waajabu kujifanya tunataka tuende tofauti na tulivyozoea kuwa tutakwama mapema sana. Urais tumeutafuta kwa jasho, kwa kazi na kwaimani kubwa haiwezekani kamwe tukataka utingishwe na CHAMA badala ya kulindwa na CHAMA.
Twende na Mama Rais wetu wa JMT ndiye Mwenyekiti wetu. Watanzania wanajua, Mila na Dasturi zinajua, kamwe tusijechekwa na wajinga kwakutaka kujalibu mifumo ya vyama ambavyo vilishakufa wakati siye tungali hai.

Nawatakia kheri na Fanaka katika kumsimika Mama yetu mpendwa Rais wa JMT Mh SSH kuwa Mwenyekiti Mpya wa CHAMA KIKUBWA CHAMA DUME CHAMA TAWALA CHAMA CHA MAPINDUZI.

Salaam zangu kwa WANA MARUANI msidanganywe na akina KIGOGO wanalipwa pesa kwa kutunga uongo na uzandiki hata hawana uchungu na UWEPO AU KUTOKUWEPO KWA UTULIVU. Hayo Maujinga yalishapitwa na Wakati. Mihemko na Roho mbaya za korosho hazinatija. Mlizingua kwa JK tukawazingua, Mkazingua kwa JPM tukawazingua sasa mnataka kujaribu kuzingua kwa SSH hapa nasema UKIZINGUA TUNAKUZINGUA HALAFU TUNAKUSALIMU KWAJINA LA JMT.

CCM hoyeee!
Unatafuta kick tu mbona hilo liko wazi??
 
Mwakibinga msaka tonge akiwa kazini, mwanaharakati anaeharakatia tumbo lake hawezi kudumu upinzani kwani anakuwa kama demu maharage ya mbeya akiombwa hakatai.
 
Andika kwa kiswahili tuu mkuu.
Kichwa cha makala tuu umechapia. Mods saidieni kuhariri hili bandiko.
 
Automatically Rais Samia ni Mwenyekiti wa CCM ila wale wanaopanic wengi wao ni udini unawasumbua Kuanzia Zitto, Kikwete na hata Lipumba. Hawana lolote zaidi ya Dini. Islam ndugu yake islam.
 
Kuna mabakia na nasalia ya watu wasiohitajika na wanaompinga Mama Samia wazi wazi juu ya Uenyekiti wa CCM.

Masalia hao wa ajulikana, na ni wale wafaidika wakubwa wa teuzi zisizo na tija Awamu uliyopita.
Tunaona waliotumwa wazi wazi kumpinga mama ati oooh, Mzanzibari, mara ooh hawezi!

Mshindwe na mlegee.

CCM Zilipomchagua Mama Samia kuwa Makamu wa Rais walijua uwezo wake.
Wanaompinga Mama Samia Uenuyekiti wa CCM, njooni hapa tupambane kwa hoja!
Mufilisi nyie!
 
Tangu zamani watoto walilala pamoja na wageni; lakini mlawiti mmoja ndiye aliyewafanya wazazi waone umhimu wakutenganisha watoto na wageni!

Unapouliza Kwanini sasa na Mimi nitakuuliza unataka hadi watoto wangapi walawitiwe?
Kutenganisha kofia ya urais na uenyekiti ni mhimu!
 
Kama una uzoefu wa kulawitiwa na viongozi waliopita tafuta ushauri nasaha.
 
Siyo lazima ila katiba za chama ndiyo zinaelekeza ivyo kuwa Rais wa nchi ndiye anayetakiwa kuwa Mwenyekiti wa chama, siyo kulazimisha bali ni wajibu kuwa ivyo
 
Ukishika dola ni lazima uwe mwenyekiti wa chama kilichokufanya ushike dola , Ni falsafa ya baba wa taifa na Ina ukweli
 
CCM HUWA IMARA ZAIDI INAPOTISHWA KIFO

Na Philipo Mwakibinga.
0758910403.

Ndugu zangu Wana wa CCM Kidumu Chama Cha Mapinduzi! Nawasalimu kwajina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naomba niendelee kusisitiza kuwa lazima tuendelee kusimama imara kama sote tunaamini Mungu na tunapokea kila atoalo Mungu na kulipa jina jema la "Baraka." Kamwe tusiwe kama Mpanda gazi hata tukasahau kama kunashuka baada ya Kupanda. Sisi ni Chama Dolla lazima tuwe makini kutokuruhusu kuvunja mila na desturi za CCM.

Ndugu zangu Wana Wa CCM , Baba wa Taifa alikuwa na Jicho kubwa la Tatu hata akaamua kulihali yeye na Wenziwe kuhakikisha RAIS ANAKUA MWENYEKITI WETU. Hii ni muhimu sana kwenye uhai wa Chama,Kwa maana ya Ulinzi na Jeuri ya kuongoza iko hapo. Tusidanganywe kamwe kutawanya kofia hizo mbili kwa vichwa viwili lasivyo tutakua tunalamba asali kwa ncha ya Kisu. Vyama vichanga vinapaswa kutuiga sisi siyo sisi kutafuta busara ya uongozi kwao wakati tunajua kuwa wao walishashindwa hata kabla ya kuanza kushindana.

Ndugu zangu Wana Wa CCM ni bahati sana sana kuwa na Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wetu kwani tunaweza kukutana naye mara mbili wakati wenzetu wanakutana naye mara moja tu. Mosi utakutana naye kama Rais pili Utakutana naye kwenye vikao vya Chama wakati wengine watakutana naye kwenye mosi tu. Yawezekana hatujui umuhimu wa hili sasa lakini tutajuta siku tukipoteza hili. Tuungane pamoja kutetea uhai wa CCM unapotishiwa kukatizwa na hii ndiyo mila na desturi ya CCM hii ambayo kila wakati YAJENGA NCHI.

Ndugu zangu Wana Wa CCM. Makundi na ujuaji usio na maana vitakatisha ndoto za Vizazi vyetu vijavyo kuiona Tanzania yenye maziwa na Asali. Lazima tulinde mazuri na mema waliyotuachia Wazee wetu. Tuhakikishe kuwa mapema sana Rais Wetu Mama Samia anapewa hadhi yake na heshima yake iliyotukuka ndani ya Chama chetu. Mama ndiye Mwenyekiti wetu na anastahili kupewa baraka zetu zote ili kazi iendelee.

Ndugu zangu Wana Wa CCM Rais Mama Samia atakapopewa uenyekiti wa CCM taifa siyo kwaajili yake binafsi ni kwaajili ya CHAMA CHETU. Naomba nieleweke kuwa SISI TUNA MUHITAJI RAIS KUWA MWENYEKITI WETU KULIKO YEYE PENGINE KWAKUA YEYE HAJAOMBA KWAAJILI YA MASLAHI YAKE BINAFSI BALI MILA NA DESTURI ZETU ZINAMPA KWAAJILI YA MASLAHI MAPANA YA TAIFA LETU. TUMPE TUVUKE SALAMA SALIMINI.

CCM tusiingie kwenye mtego waajabu kujifanya tunataka tuende tofauti na tulivyozoea kuwa tutakwama mapema sana. Urais tumeutafuta kwa jasho, kwa kazi na kwaimani kubwa haiwezekani kamwe tukataka utingishwe na CHAMA badala ya kulindwa na CHAMA.

Twende na Mama Rais wetu wa JMT ndiye Mwenyekiti wetu. Watanzania wanajua, Mila na Dasturi zinajua, kamwe tusijechekwa na wajinga kwakutaka kujalibu mifumo ya vyama ambavyo vilishakufa wakati siye tungali hai.

Nawatakia kheri na Fanaka katika kumsimika Mama yetu mpendwa Rais wa JMT Mh SSH kuwa Mwenyekiti Mpya wa CHAMA KIKUBWA CHAMA DUME CHAMA TAWALA CHAMA CHA MAPINDUZI.

Salaam zangu kwa WANA MARUANI msidanganywe na akina KIGOGO wanalipwa pesa kwa kutunga uongo na uzandiki hata hawana uchungu na UWEPO AU KUTOKUWEPO KWA UTULIVU. Hayo Maujinga yalishapitwa na Wakati. Mihemko na Roho mbaya za korosho hazinatija. Mlizingua kwa JK tukawazingua, Mkazingua kwa JPM tukawazingua sasa mnataka kujaribu kuzingua kwa SSH hapa nasema UKIZINGUA TUNAKUZINGUA HALAFU TUNAKUSALIMU KWAJINA LA JMT.

CCM hoyeee!
kwani kuna mtu amekataa?
 
Back
Top Bottom