Rais Samia: Lita Milioni 70 za Maji kutoka Kigamboni ziingizwe Dar es Salaam kusaidia upungufu wa Maji

Rais Samia: Lita Milioni 70 za Maji kutoka Kigamboni ziingizwe Dar es Salaam kusaidia upungufu wa Maji

Wananchi wa hali ya Chini ananufaikia vipi na hiyo nishati. au ni uzinduzi tu wa kongamano
Soma maelezo ya Rais ,kasema sio swala la vuupu kama gas bali ni swala mtambuka so lianze na mapendekezo ya kisera kutoka kwa wadau then serikali itafanyia Kazi..

Serikali haizalishi gas mzee
 
Kigamboni sio Daisalaam? Hili taifa wakati mwengine basi tu. Huko maji yalipoanzia haya sambazwi bomba linapita tu.
 
Tatizo sio mto ruvu,,,hivi imagine mtu anae ishi njombe pale penye kila aina ya chanzo cha maji bada hana uhakika wa maji safi na salama,,,tatizo mnajadili tatizo la taifa kama la dasilamu""""embu swala la maji nahiyo nishati tuijadili kitaifa tuje na suluhisho kama taifa sio shida ipo na shinyanga nyie mmekazana tu kwa Aziz ally
 
Dar 70% watumie ges asilia kupikia ziwekwe gas prepaid meters no Mkaa Dar. Pia Moro mjini Tuokoe Misitu ya Pwani na Morogoro. Vinginevyo we are doomed
Morogoro wanachofanyia pale inasikitisha sana leo Moro ni joto jua kali utasema uko Singida huko wanakata hovyo miti na serikali ya mkoa wapo tu wanaona. Mji ulikuwa na hali ya hewa nzuri tu leo hakufai. Pwani ndio usiseme na viongozi wapo wa mkoa. Kuwe na sheria kali kulinda miti na vyanzo vya maji na hawa wanaojenda kiholela Dar na miji mingine kama hawatavunjiwa na fine juu hawataacha hakuna kuonea huruma watu wanaovunja sheria kwa makusudi na kuleta athari kubwa miaka ijayo.
 
Morogoro wanachofanyia pale inasikitisha sana leo Moro ni joto jua kali utasema uko Singida huko wanakata hovyo miti na serikali ya mkoa wapo tu wanaona. Mji ulikuwa na hali ya hewa nzuri tu leo hakufai. Pwani ndio usiseme na viongozi wapo wa mkoa. Kuwe na sheria kali kulinda miti na vyanzo vya maji na hawa wanaojenda kiholela Dar na miji mingine kama hawatavunjiwa na fine juu hawataacha hakuna kuonea huruma watu wanaovunja sheria kwa makusudi na kuleta athari kubwa miaka ijayo.

Tatizo nchi na pia mikoa haina utekelezaji endelevu wa sera wala framework ya jinsi ya kutunza ardhi, pori tengefu, vyanzo vya mito na maji pia upandaji miti.

Answers to Primary Questions by Hon. Japhet Ngailonga Hasunga (CPA) (54 total)​

Print
MHE. RICHARD P. MBOGO aliuliza:-
Katika mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa Mkoa wa Katavi uliofanywa na Halmashauri ya Mpanda mwaka 2004 kwa kushirikisha ngazi ya Mkoa na ngazi ya Wizara, zililipwa sehemu za Hifadhi za Misitu North East Mpanda (JB94) na Msanginia (JB215) na ramani mbalimbali kuidhinishwa ikiwemo 48870, 48893 na 40250.

Je, ni lini Serikali itabadili mipaka hiyo kwa mujibu wa Sheria ya Misitu ya 2002 (Namba 14) Kifungu cha 28?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu naomba nichukue nafasi hii kwanza kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunipa uhai na kuniwezesha kufika siku hii ya leo.

Pili, nimshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli kwa kuniamini na kuniteua katika nafasi hii.

Tatu, nimshukuru Mheshimiwa Spika pamoja na uongozi mzima wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Wenyeviti wa Kamati nilizokuwa Mjumbe kwa malezi yao ambayo wameyatoa kwangu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii naomba kujibu swali la Mheshimiwa Richard Philip Mbogo, Mbunge wa Nsimbo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Misitu wa hifadhi wa Mpanda North East na Msangimya ni misitu ya Serikali inayosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania. Msitu wa North East Mpanda umehifadhiwa kwa tangazo la Serikali Na. 296 la mwaka 1949.

Aidha, Msitu wa Msangimya umehifadhiwa kwa Tangazo la Serikali Na. 447 la mwaka 1954 na inasimamiwa kwa mujibu wa Sheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002 Sura ya 323.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ilipima maeneo ya Hifadhi ya Msitu wa Mpanda North East na Msangimya kupitia ufadhili wa Shirika la Africare chini ya mradi wa Ugalla Ecosystem ili kuanzisha maeneo ya usimamizi wa Wanyamapori (Wildlife Management Area- WMA) na makazi pamoja na kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji. Baada ya upimaji huo ramani 48870, 48893 na 40250 zilichorwa na Halmashauri husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, licha ya nia njema iliyokuwepo ya kuwapatia wananchi makazi yaliyopimwa kwa mujibu wa sheria na uanzishwaji wa maeneo ya usimamizi wa wanyamapori (WMA) na kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji, utaratibu huu haukuzingatia Sheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002 pamoja na Sheria ya Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009.

Na kwa mujibu wa kifungu cha 31(1) cha Sheria ya Wanyamapori, WMA zote zinaanzishwa kwenye misitu iliyoko kwenye ardhi ya kijiji au ardhi ya ujumla na siyo kwenye misitu ya Hifadhi ya Serikali Kuu. Aidha, mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji inafanyika kwenye ardhi ya kijiji husika na siyo kwenye misitu iliyohifadhiwa kisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili ardhi ya msitu wa hifadhi uweze kutumika kwa matumizi mengine, Sheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002 katika kifungu cha 29 inatoa utaratibu wa kisheria wa kufuta hadhi ya msitu wa hifadhi ambapo Waziri wa Maliasili na Utalii anaweza kufuta sehemu ya msitu au msitu wote wa hifadhi baada ya kujiridhisha kuna umuhimu ya kufanya hivyo.

Mara baada ya mchakato huu kukamilika ndipo ardhi ya msitu itatumika kwa matumizi na shughuli zingine za kibinadamu mbali na uhifadhi.

Aidha, Waziri wa Maliasili na Utalii atatoa maamuzi hayo baada ya kushauriana na Kamati ya Taifa ya Ushauri wa Misitu (National Forestry Advisory Committee) ambayo inatajwa katika Sheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002 katika Kifungu cha 10.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mchakato wa kupima sehemu ya misitu ya hifadhi niliyoeleza hapo juu umefanyika kinyume cha sheria na taratibu zilizopo, hadhi ya misitu hiyo ya hifadhi inaendelea kubaki kisheria kama ilivyoainishwa kwa mujibu wa matangazo ya Serikali niliyoyataja hapo juu.

Aidha, Serikali itaangalia kama kunaweza kuwa na uwezekano wa maeneo hayo kutolewa kwa ajili ya matumizi mengine kwa mujibu wa sheria, lakini ikiweka kipaumbele kwanza kitatolewa kwa maslahi mapana ya Taifa na kwa kufuata ushauri utakaotolewa na Kamati ya Taifa ya Ushauri ya Misitu

SOMA ZAIDI : BOFYA : Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi : Bunge Polis
 
10 November 2022

Wakala wa Uchimbaji wa Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA) wajipanga kutatua upungufu wa maji Dar es Salaam pia DCCA wapatiwa mitambo na vifaa vipya vya kufanya kazi



Mtendaji mkuu wa Wakala wa Uchimbaji wa Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA), Simon Ngonyani amewaomba wakazi wa Dar es Salaam kuwa na uvumilivu katika kipindi cha mpito cha adha ya uhaba wa maji wakati wakiendelea na ujenzi wa mabwawa sambamba na uchimbaji wa visima katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Source: Azam TV


Vifaa na mitambo ya kazi DCCA

1668103855784.png

TOKA MAKTABA:​

21 March 2017

DDCA : Sisi ni nani​


Source : DCCA

PREAMBLE

The Government of Tanzania under Civil Service Reform Program decided to transform selected organizations, carrying out essential public functions into Executive Agencies. As a result of these government reforms, the Drilling and Dam Construction Agency (DDCA) was created under the Ministry of Water and Irrigation. DDCA came into existence following the Executive Agencies Act. No. 30 of 1997, and was launched on the 26th of March 1999.

The role of DDCA is to develop sustainable and safe water sources through efficient means and at cost effective price. This objective is in line with the national objective of alleviating poverty and improving the health of people through provision of clean, safe, and adequate water supply to rural and urban population.

Currently only about 58.3% of the rural and 83% of urban population in Tanzania are served with clean water (MOWI, June 2009). As the human population, industries and irrigation schemes increase the demand for water increases too. To arrest this situation, Groundwater Exploration & Exploitation as well as Dam Construction activities are necessary and the Drilling and Dam Construction Agency has to be effective in performing these activities

 
Back
Top Bottom