Rais Samia: Lita Milioni 70 za Maji kutoka Kigamboni ziingizwe Dar es Salaam kusaidia upungufu wa Maji

Rais Samia: Lita Milioni 70 za Maji kutoka Kigamboni ziingizwe Dar es Salaam kusaidia upungufu wa Maji

Tumejaza methane kwenye vyoo vyetu tunakosa apparatus tu na mwamko.
 
25 October 2022
Songwe, Tunduma

Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia wananchi wa kitongoji cha Ikanka kijiji cha Itumba wilaya ya Ileje kuendelea kuishi sehemu ya eneo la hifadhi ya msitu wa Ileje Range mkoani Songwe

1667293738633.png


Uamuzi huo unakifanya kitongoji cha Nkanka sasa kutambuliwe ndani ya hifadhi ya msitu wa Ileje Range kutokana na idadi ya kaya 105 zenye makazi zilizopo ndani ya eneo.

Aidha, uamuzi huo pia umegusia mgogoro wa matumizi ya ardhi katika hifadhi za msitu wa Mugombezi uliopo kijiji cha Nyimbili katika kata ya Mlowo, Ilengo Mbozi mkoani Songwe.

Akitangaza uamuzi huo, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula amesema sehemu ya eneo la hifadhi ekari 278 zitamegwa na kubaki kwa wananchi kutoka ekari 414 kwa kuwa eneo hilo limeendelezwa kwa shighuli za kilimo, makazi na kuwekwa huduma za kijamii kama uwanja wa mpira na pump ya maji.

Waziri Mabula amewatahadharisha wananchi walioruhusiwa kuendelea eneo hilo kutojaribu kuongeza maeneo wanayoishi huku akieleleza kuwa, mara baada ya utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi kukamilika maeneo yote ya hifadhi yanatakiwa kulindwa.

Aidha, Dkt Mabula ambaye alikuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ikanka Oktoba 24, 2022 akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta aliagiza Shughuli za kilimo pembezoni mwa vyanzo vya maji nazo zisitishwe ili kunusuru vyanzo vya maji ndani ya hifadhi.

Kwa upande wao Mawaziri walioambatana na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi walisisitiza umuhimu wa kutunzwa mazingira pamoja na kuandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi kwa maeneo yote yaliyomegwa.

Naibu waziri wa Maji Meryprisca Mahundi aliwaambia wananchi wa kitongoji cha Ikanka kuwa, baada ya kuruhusiwa kuendelea kuishi eneo hilo wahakikishe wanatunza na kuhifadhi vyanzo vya maji na kuepuka shughuli zozote zitakazosababisha uharibifu wa vyanzo hivyo.

Khamis Hamza Chilo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira alisisitiza suala la wananchi kupanda miti katika maeneo waliyoachiwa ili kutunza mazingira.

Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde pamoja na Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega walieleza umuhimu wa maeneo yaliyomegwa kupangiwa matumizi ya ardhi na kupimwa sambamba na kuanishwaa maeneo ya kilimo, mifugo pamoja na uvuvi ili kuepuka kutengeneza migogoro mingine.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka viongozi wa mikoa na wilaya kuhakikisha wanatekeleza maamuzi ya baraza la mawaziri kuhusiana na migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 kwa kuweka mpango wa utekelezaji hasa kwa yale maeneo ambayo hayana tathmini ya kina.

Katika maamuzi yake, Baraza la Mawaziri liliamua vijiji 920 kati ya 975 vyenye migogoro katika ranchi, mapori ya akiba, mashamba na vyanzo vya maji kubaki ingawa baadhi ya vijiji vitahusisha marekebisho ya mipaka kwa njia shirikishi,

Hata hivyo, vijiji 55 kati ya 975 vinaendelea kufanyiwa tathmini na kamati na wataalamu wake kutoa mapendekezo kwa ajili ya maamuzi.

Tayari kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta imeshatembelea mikoa kumi na tisa kati 26 kamati imeshapeleka mrejesho wa Maamuzi ya Baraza la Mawaziri na inaendelea na ziara yake kwenye mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na Ruvuma
 
Ujenzi holela wakulaumiwa ni serikali
 
Bei ya Umeme iwe chini 50% ya sasa
Bei ya Gesi iwe chini 50% ya sasa
Bei ya Mkaa iwe zaidi ya Tanzanite maeneo ya miji
Usambazaji wa Umeme na Gesi remote areas uendelee kwa kasi ya Mwanga

Kinyume cha hapo hiki kiangazi ukame cha mtoto kijacho mpaka sisimizi watakimbilia mjini
Tafuta hela bosi
Umeme hautashuka bei
 
Wakulima
Wafugaji
Mabwawa ya samaki kando ya Ruvu hameni mapema kuanzia leo
 
26 October 2022
Mbarali, Mbeya
Tanzania

Mgogoro wa Mpaka wa RUAHA Wafika ukomo,Vijiji vitano na vitongoji 41 vyatakiwa kufutwa na raia wake

Mgogoro wa mpaka wa hifadhi ya RUAHA uliodumu kwa muda mrefu ukiwahusisha wananchi na hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA umefika mwisho.


Hii ni baada ya timu ya Mawaziri nane wakiongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi Mh: Angelina Mabula kufika wilayani hapo na kutoa maamuzi kwa niaba ya baraza la Mawaziri.

Awali kabla ya Utoaji wa Maamuzi timu hiyo ya Mawaziri ilitembelea na kukagua hifadhi ya RUAHA ambapo walibaini ukataji miti hovyo, kilimo na ufugaji holela unaifanywa na wakazi wa eneo hilo.

Baada ya kujiridhisha katika Mkutano wa hadhara uliowakutanisha Mawaziri hao na Wananchi Mh: Angelina Mabula akasimama na kuvitaja vijiji 15 vinavyotakiwa kubaki na vijiji vitano vinavyotakiwa kuondoka kadharika vitongoji 41 vinatakiwa kuondoka na kufutwa kabisaa.
 
Gharama ndio mchawi wa mambo wanayojadili, wanatakiwa kujadili gesi gani inawafaa watanzania wanyonge ni LPG(ya kutoka nje kwa mabeberu) au LNG (ya mtwara) .Hivi serikali ina washauri bora kweli?
 
Wazalishe Bio gas kutokana na waste ya vyakula ambavyo tunatupa tu majalalani kila kukicha
Rahisi tu yaani, unazalisha unatumia? Humu jf Kuna wajinga kuliko Facebook, nimewahi kusema hili mara nyingi
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishiriki ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Nishati Safi ya Kupikia, Leo Novemba 1, 2022



Prof. Anna Tibaijuka
Mbunge mstaafu Profesa Anna Tibaijuka amesema Watanzania wengi wanafahamu umuhimu wa gesi lakini bado wanalazimika kutumia mkaa na kuni kwa kuwa gharama za nishani safi ndio ni tatizo.

Amesema “Moja ya changamoto ya nishati safi ni gharama za vifaa, mfano gesi ndogo ilikuwa inauzwa Tsh. 18,000 sasa hivi inauzwa Tsh. 24,000 hapo ndipo tatizo linapoanzia.”

Amesema Serikali inatakiwa kuingilia na kuweka sawa suala hilo kupitia sera, pia ameshauri EWURA na mamlaka nyingine husika zitengeneze mazingira mazuri kwa watumiaji na wazalishaji wa gesi ambao ndio wawekezaji.
Samia Suluhu Hassan - Rais
Tunapoikata miti sijui uhai wetu uko wapi, ni gharama ya maradhi tunayopata.

Kwenda kutafuta nishati ya kuni kunaleta gender based violence, ukiwa huko unakutana na wachunga mbuzi (wabakaji), ukirudi nyumbani unakutana na kipigo.

Kingine ni kubadili mindset, unapojenga nyumba unajenga na jiko la nje ili utumie kuni. Tubadili hii mindset.

Katika kutafuta afua, kumekuwepo na teknolojia ya biogas, majiko ya gesi, umeme n.k

Takwimu zinasema Kaya zinazotumia gesi ni 5%, umeme ni 3%, bado tunachangamoto ya kutotumia vizuri nishati safi.

Nielekeze kwamba swala hili siyo la muda mfupi, kwamba baada ya muda mfupi watanzania wote wawe na nishati safi. Tuanze sasa, lakini twende na kasi kubwa.

Swala hili ni mtambuka, kianzishwe kikosi kazi kisicho cha kiserikali kitakacho chambua na kutoa mapendekezo ya kisera, kije na mpango kazi utakaoelekeza kwenye kutafuta suluhu ya nishati safi na endelevu.

Ni lazima twende na nishati safi ya kupikia kwa maendeleo ya nchi, jamii na kukinga haki za wanawake ambao wanafanya mambo mengi ya kujiumiza pasipo malipo. Tuwapunguzie mzigo na madhara ya kile wanachofanya tena bila malipo. Pia, tunampa muda zaidi wa kushughulika na mambo mengine ya kiuchumi.

Hadi 2032 tuwe na nishati safi ya kupikia, lengo ni kumtua mama mzigo wa kuni kichwani.

Tunasema mkaa ni rahisi lakini gharama ya mti ule ni kubwa sana. Miti tunayopanda mingi iwe ya matunda maana kukata mti wa matunda utawaza mara nne. Miti ya asili tuitumie kuzalisha asali kwa kuwa ina soko kubwa duniani.

Naipa Wizara Mwaka mzima wa 2023 nataka mjielekeze kwenye hili la taasisi kubwa kutumia nishati safi. Ikifika 2024 nataka nisimame kwa wananchi niseme nimefanikisha hilo kwa kiwango hiki.

Kuhusu Upatikanaji wa maji DSM kwanza ni mabadiliko ya hali ya hewa yenye sura 2 ambayo ni Ki Mungu na kwa sababu ya mambo yetu wenyewe, ukataji wa miti ndiyo sababu kuu, watu wanalima, wameweka vizuizi vya maji kwenda mto ruvu, watu wamejenga ponds wanafuga samaki humo humo. Mkuu wa mkoa na DAWASA nawaagiza mkasafishe mto isaidie upatikanaji wa maji.

Nataka nione lita milioni 70 kutoka kigamboni zinaingia DSM ili kupunguza changamoto ya maji.

DAWASA na Wizara ya maji itazame miundo mbinu, mingine ilijengwa zamani, kingine ni ujenzi holela wa makazi. Waziri mkuu atawasimamia.

Tunalia na gesi na umeme wakati tuna makaa ya mawe yenye uwezo wa kutoa nishati kali zaidi.
Makaa ya mawe yapo kwa wingi sana nchini.
 
Nataka nione lita milioni 70 kutoka kigamboni zinaingia DSM ili kupunguza changamoto ya maji.

13.01.2022
Mradi wa Maji Kigamboni utakamilika Aprili 2022, na tunategemea kuanza kazi ya ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji kwa wananchi mapema wiki ijayo" Mhandisi Cyprian Luhemeja, Afisa Mtendaji Mkuu -DAWASA



MSUMBA ON JANUARY 15, 2022
Ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita milioni 15 Mradi wa DAWASA Kigamboni, Dar es Salaam Tanzania



Na Fredy Mshiu - DAWASA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imesema, mradi wa maji Kigamboni wenye lengo la kutatua changamoto ya maji kwa wananchi utakamilika Aprili mwaka huu.

Haya yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cpyrian Luhemeja alipotembelea na kukagua mradi huo katika siku ya tatu ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya majisafi na usafi wa mazingira.

"Tulikubaliana na mkandarasi kukamilisha ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita milioni 15 ifikapo mwishoni mwa Januari 2022, na maendeleo yake sio mabaya na mwisho wa Januari tunategemea kukamilisha," amesema Mhandisi Luhemeja.

Mhandisi Luhemeja amempongeza mkandarasi anaetoa maji visimani kwa kukamilisha ununuzi wa pampu tatu za kusukuma maji, huku akimuagiza kuongeza kasi katika mchakato wa manunuzi ya pampu za kutoa maji visimani kupeleka kwenye tenki.

"Namuagiza mkandarasi kukamilisha manunuzi hayo mapema ifikapo mwezi wa pili mwaka huu ili kukamilisha mradi huu, endapo ifikapo mwezi wa nne mkandarasi hajamaliza mradi tutamwondoa," amesisitiza Mhandisi Luhemeja.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Luhemeja ameeleza hatua ya pili ya mradi ni kupeleka maji Kongowe kwani ni karibu na maji yapo ya kutosha huku hatua ya tatu itahusisha kupeleka maji Mbagala ambapo yote haya yatafanyika ndani ya mwaka huu kabla ya Disemba.

Shughuli ya usambazaji wa mabomba kupitia mradi huu wa maji Kigamboni inatarajiwa kuanza Jumatatu tarehe 17 Januari mwaka huu huku Afisa Mtendaji Mkuu, Mhandisi Luhemeja akielekeza Menejimenti ya DAWASA kuhakikisha wanaendeleza mapambano kukamilisha mradi huu ndani ya muda


TOKA MAKTABA :

January 24, 2016 by Global Publishers

Matengenezo ya bomba kubwa la maji yaendelea Kawe-Tegeta​


4
Kazi ya Kuunganisha Bomba la Maji kutoka mtambo wa uzalishaji wa Ruvu Chini ukiendelea katika eneo la Wazo Tegeta.
7
Matengenezo ya Bomba hili ndiyo yaliyopelekea kuzimwa kwa mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Chini ambapo kwa muda wa saa 48 huduma ya maji itakosekana katika jiji la Dar Es Salaam na Bagamoyo.
5
Afisa Mtendaji mkuu wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza juu ya matengemezo hayo alipotembelea katika eneo hilo kujionea shughuli zinavyoendelea.
 
28 October 2022
Dar es Salaam, Tanzania

Waziri Aweso atoa maelekezo DAWASA


Video courtesy of Wasafi Media

Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameiagiza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kushirikiana na wadau wengine wenye visima vikubwa vya maji kutoa huduma ya maji kwa kipindi chote cha ukame.

Akikagua zoezi la uunganishaji wa mabomba ya maji eneo la Wazo mkoani Dar es Salaam, Waziri Aweso amesema wizara yake itashirikiana na DAWASA kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji katika kipindi chote cha ukame.

Pia ameielekeza DAWASA kuzingatia vema ratiba ya mgao wa maji na kugawa maji bila ya upendeo.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA mhandisi Cyprian Luhemeja amesema, mradi wa maji ya visima wa Kigamboni utakamilika siku ya Jumapili na hivyo kuwawezesha wananchi kupata huduma ya maji.

Tarehe 25 mwezi huu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla alitangaza kuanza rasmi kwa mgao wa maji mkoani humo na katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Pwani, kufuatia kupungua kwa kina cha maji katika mto Ruvu.
 
Back
Top Bottom