Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 20,694
- 32,527
Pesa ya kununua gesi wanaitoa wapi?Dar 70% watumie ges asilia kupikia ziwekwe gas prepaid meters no Mkaa Dar. Pia Moro mjini Tuokoe Misitu ya Pwani na Morogoro. Vinginevyo we are doomed
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pesa ya kununua gesi wanaitoa wapi?Dar 70% watumie ges asilia kupikia ziwekwe gas prepaid meters no Mkaa Dar. Pia Moro mjini Tuokoe Misitu ya Pwani na Morogoro. Vinginevyo we are doomed
Tafuta hela bosiBei ya Umeme iwe chini 50% ya sasa
Bei ya Gesi iwe chini 50% ya sasa
Bei ya Mkaa iwe zaidi ya Tanzanite maeneo ya miji
Usambazaji wa Umeme na Gesi remote areas uendelee kwa kasi ya Mwanga
Kinyume cha hapo hiki kiangazi ukame cha mtoto kijacho mpaka sisimizi watakimbilia mjini
Wazalishe Bio gas kutokana na waste ya vyakula ambavyo tunatupa tu majalalani kila kukichaPesa ya kununua gesi wanaitoa wapi?
Anna tibaijuka bado yupo tu
Nchi hii kuna watu hawataki kuachia
Channel
Ova
Kwenye swala la maji kwanini akosekane?Anna tibaijuka bado yupo tu
Watu wameshalipina posho tayariWananchi wa hali ya Chini ananufaikia vipi na hiyo nishati. au ni uzinduzi tu wa kongamano
Ewaaa acha watu washare keki ya taifaWatu wameshalipina posho tayari
Rahisi tu yaani, unazalisha unatumia? Humu jf Kuna wajinga kuliko Facebook, nimewahi kusema hili mara nyingiWazalishe Bio gas kutokana na waste ya vyakula ambavyo tunatupa tu majalalani kila kukicha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishiriki ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Nishati Safi ya Kupikia, Leo Novemba 1, 2022
Prof. Anna Tibaijuka
Mbunge mstaafu Profesa Anna Tibaijuka amesema Watanzania wengi wanafahamu umuhimu wa gesi lakini bado wanalazimika kutumia mkaa na kuni kwa kuwa gharama za nishani safi ndio ni tatizo.
Amesema “Moja ya changamoto ya nishati safi ni gharama za vifaa, mfano gesi ndogo ilikuwa inauzwa Tsh. 18,000 sasa hivi inauzwa Tsh. 24,000 hapo ndipo tatizo linapoanzia.”
Amesema Serikali inatakiwa kuingilia na kuweka sawa suala hilo kupitia sera, pia ameshauri EWURA na mamlaka nyingine husika zitengeneze mazingira mazuri kwa watumiaji na wazalishaji wa gesi ambao ndio wawekezaji.
Samia Suluhu Hassan - Rais
Tunapoikata miti sijui uhai wetu uko wapi, ni gharama ya maradhi tunayopata.
Kwenda kutafuta nishati ya kuni kunaleta gender based violence, ukiwa huko unakutana na wachunga mbuzi (wabakaji), ukirudi nyumbani unakutana na kipigo.
Kingine ni kubadili mindset, unapojenga nyumba unajenga na jiko la nje ili utumie kuni. Tubadili hii mindset.
Katika kutafuta afua, kumekuwepo na teknolojia ya biogas, majiko ya gesi, umeme n.k
Takwimu zinasema Kaya zinazotumia gesi ni 5%, umeme ni 3%, bado tunachangamoto ya kutotumia vizuri nishati safi.
Nielekeze kwamba swala hili siyo la muda mfupi, kwamba baada ya muda mfupi watanzania wote wawe na nishati safi. Tuanze sasa, lakini twende na kasi kubwa.
Swala hili ni mtambuka, kianzishwe kikosi kazi kisicho cha kiserikali kitakacho chambua na kutoa mapendekezo ya kisera, kije na mpango kazi utakaoelekeza kwenye kutafuta suluhu ya nishati safi na endelevu.
Ni lazima twende na nishati safi ya kupikia kwa maendeleo ya nchi, jamii na kukinga haki za wanawake ambao wanafanya mambo mengi ya kujiumiza pasipo malipo. Tuwapunguzie mzigo na madhara ya kile wanachofanya tena bila malipo. Pia, tunampa muda zaidi wa kushughulika na mambo mengine ya kiuchumi.
Hadi 2032 tuwe na nishati safi ya kupikia, lengo ni kumtua mama mzigo wa kuni kichwani.
Tunasema mkaa ni rahisi lakini gharama ya mti ule ni kubwa sana. Miti tunayopanda mingi iwe ya matunda maana kukata mti wa matunda utawaza mara nne. Miti ya asili tuitumie kuzalisha asali kwa kuwa ina soko kubwa duniani.
Naipa Wizara Mwaka mzima wa 2023 nataka mjielekeze kwenye hili la taasisi kubwa kutumia nishati safi. Ikifika 2024 nataka nisimame kwa wananchi niseme nimefanikisha hilo kwa kiwango hiki.
Kuhusu Upatikanaji wa maji DSM kwanza ni mabadiliko ya hali ya hewa yenye sura 2 ambayo ni Ki Mungu na kwa sababu ya mambo yetu wenyewe, ukataji wa miti ndiyo sababu kuu, watu wanalima, wameweka vizuizi vya maji kwenda mto ruvu, watu wamejenga ponds wanafuga samaki humo humo. Mkuu wa mkoa na DAWASA nawaagiza mkasafishe mto isaidie upatikanaji wa maji.
Nataka nione lita milioni 70 kutoka kigamboni zinaingia DSM ili kupunguza changamoto ya maji.
DAWASA na Wizara ya maji itazame miundo mbinu, mingine ilijengwa zamani, kingine ni ujenzi holela wa makazi. Waziri mkuu atawasimamia.
Nataka nione lita milioni 70 kutoka kigamboni zinaingia DSM ili kupunguza changamoto ya maji.
Mpaka yafike Kagera yatauzwa Sh ngapi?Makaa ya mawe yapo kwa wingi sana nchini.