Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaapisha viongozi mbalimbali aliowateua jana huku akisisitiza kuwa mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika maeneo husika.
Rais Samia ameyasema hayo leo Alhamisi Agosti 15,2024 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua jana, Ikulu jijini Dar es Salaam huku akiwataka kujiongeza ili kutumikia wananchi.
“Kwanza ni shukurani kwa Mungu kutujalia kukutana hapa, lakini la pili niwapongeze mlioapa hapa leo mlioaminiwa, la tatu niseme tu mabadiliko haya ni ya kawaida ni kuongezea ufanisi katika maeneo yetu na Makamu wa Rais (Dk Philip Mpango) amesema vizuri tunachotarajia ni kwenda kuongeza ufanisi kwenye maeneo yenu na la nne kiapo.”
‘Mmeapa viapo viwili hapa pale nyuma kimoja cha maadili lakini mbele mliapa maadili na kiapo kwa miungu yenu mnayoiamini au kwa dini zenu mnazoziamini muende mkaishi na viapo hivyo, lakini pia mfuate maadili ya kazi inavyotakiwa