Rais Samia Suluhu Hassan amesema “Tulikuwa tunaangalia magereza yetu tukabaini waliofungwa na walio mahabusu idadi yao ni kama ilikuwa sawa, wengi wao ni kesi za kubambikwa ndio maana unakuta mtu yupo ndani miaka mitatu, haendi mahakamani, haulizwi na hakuna kesi ya maana.
“Tulichofanya ni kuwatoa magereza yakapata kupumua, msipofanya haki, mnapochukua rushwa kumtia mtu hatiani ambaye hana hatia na mwenye hatia mkamuacha nje anaendeleza ubabe akiamini pesa yake itambeba, ambaye hana hela anaishia jela.
“Usiangalie Duniani, umechukua fedha sawa, imekufanya umekuwa nani, imekufikisha wapi, matatizo yako ya Dunia yameisha, ni ushawishi tu wa akili, itendeeni haki sheria.”
Amesema hayo Novemba 24, 2022 alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wanasheria wa 27 Afrika Mashariki unaofanyika Jijini Arusha.